Picha ya 1 hadi ya 5, Ni gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea
alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Picha ya 6 hadi ya 7, Ni Mbunge wa Jimbo la Muheza Hebert Mtangi akiwasili nje ya jengo la Chumba cha Kuhifadhia Maiti cha Hospitali ya Teule Muheza kwa ajili ya kushuhudia mwili wa msaniii Sharo Millionea aliyekufa katika ajali ya gari wakati akitoka Dar es Salaam kwenda Lusanga, Muheza mkoani Tanga, ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Songa Kibaoni .
Picha ya 8, Ni wakazi wa wilaya ya Muheza na maeneo mengine wakiwa wamefurika nje ya Chumba cha Maiti cha Hospitali Teule Muheza, kusubiri kushuhudia mwili wa Sharo Millionea, aliyefariki kwa ajali ya gari.
Sharo Millionea amezikwa leo saa saba mchana kijijini kwao Lusanga wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga.Mazishi yake yameudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serekali,Vyama vya siasa na wasanii wenzake wa maigizo na mziki.
Innah Lilahi Wainnah Ilahi Raajuun.
No comments:
Post a Comment