Wednesday, October 7, 2015

Msindai awatangazia neema mama ntilie, machinga, waendesha boda boda.

Mgombe Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini (CHADEMA) Mgana Msindai, akizungumza na wafanyabiashara wa soko kuu mjini Singida wakati wa Mkutano wa kampeni kuomba ridhaa ya wananchi kumchagua kuwa Mbunge ili kuondoa kero ndogo ndogo za kutozwa ushuru kwa wamachinga na mama ntilie.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini (CHADEMA ) Mgana Msindai ameahidi kuondoa kero na kodi ndogondogo wanazotozwa wafanyabiashara wadogo wakiwemo mama ntilie.

Akizungumza jana kwenye  Mkutano wa Kampeni wa chama chake eneo la soko kuu, Msindai alisema mojawapo ya kero hizo ni pamoja na kusumbuliwa kwa kina mama lishe bila kujali ugumu wa maisha unaowakabili hivyo akichaguliwa ataziondoa kodi hizo mara moja.

“Hizi kero za mama ntilie kutozwa shilingi 20,000 kwa mwezi na meza ndogo ndogo za matunda na mboga mboga nitazifuta kwa kushirikiana na madiwani wenzangu wa Ukawa, kwani hii sio sheria kuu, ni sheria ndogo ndogo zinazotungwa na madiwani, sisi tutazifuta mara moja  ili watu hawa waweze kubadilika.”Alisema Msindai maarufu kwa jina la CRDB.

Hata hivyo ili kuendena na hadhi ya Manispaa, Msindai ameahidi kushirikiana na madiwani wenzake kujenga soko jipya la kisasa kwa kuvunja
lililopo kwani halina hadhi ya kuwa soko la Manispaa.

 “Hili soko ni chafu sana halina hadhi, halifai, hakuna mitaro ya maji machafu, miundo mbinu ni mibovu mvua zikinyesha hapa watu wanatafuta pa kutokea, kwa ujumla tutalivunja, hata haya mabucha hayana kiwango kinachotakiwa na Manispaa.” Alisema Msindai na kushangiliwa na wafanyabishara.

Aidha aliwataka wananchi kuiondoa CCM madarakani kwani katika kipindi cha mika 54 hakuna mabadiliko yoyote zaidi ya kuimba nyimbo za kuwakebehi wananchi, kuwa CCM ni ile ile na watu wake ni wale wale, eti mtaisoma namba.

“Nyie wenyewe ni mashahidi kwa nyimbo zao wanawaambia mtaisoma namba, huku wao wakineemeka , mimi nimeamua kuondoka huko, Lowasa , Sumaye wameondoka nyie mnangoja nini, mtaisoma namba kweli, badilikeni tupeni sisi miaka mitano muone mabadiliko.” Alisema na kuongeza

“Stendi ya zamani imefungwa bila sababu nilikuwa naipigania sana lakini baada ya kuona hatuendi pamoja nikaamua  kutoka, na kujiunga na chama chenye sera za kweli, na mkinichagua stendi hii itarudi haraka sana , hakuna cha mwekezaji hapa ni ufisadi mtupu na sanaa za Mkurugenzi na madiwani wake wasiokuwa na dira.” Alisema CRDB na kuamsha nderemo.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge wa Viti maalumu CHADEMA, Aisha alisema ni wakati sasa kwa wananchi wa Jimbo la Singida mjini kuipiga chini CCM kwani ni ngonjera tupu wanafanya na kuwaancha wananchi wakipigika kila kona.

Aidha alisema ni jambo la kawaida kuona meli ikiwa ndani ya maji lakini sio jambo la kawaida maji kuingia ndani ya meli , maana yake inataka kuzama, hivyo wananchi wasikubali maji kuingia ndani ya meli kwani ni sawasawa na kuichagua CCM.

“ Msindai aliona meli inaingia maji akaamua kuchupa na kuogelea na kuja UKAWA kwani aliogopa meli hiyo sasa imeingia maji kinachofuata ni kuzama , akawahi na sasa naombeni sana kina baba zangu, kina mama na makamanda wenzangu mchagueni huyo mzee tulete mabadiliko hapa Singida, huyu Musa wa CCM hana jipya zaidi ya kula fedha za walimu wenzake akishirikiana na Mkurugenzi Joseph Mchina, eti fedha za saccos ya walimu zimejenga maabara jamani hii ni akili au matope.” Alihoji Aisha.


Aisha aliwataka wananchi kumchagua Rais Edward Lowasa, Mbunge Mgana Msindai na Diwani wa Chadema Kulaya ili kukamilisha ushindi wa goli 3-0 dhidi ya CCM.

No comments:

Post a Comment