Mwenyekiti wa zamani wa
jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni Hemed Salum Hamad, akitoa nasaha
zake kabla ya kujiuzulu na kamati yake ya zamani ili kupisha uchaguzi
mpya kufanyika.Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Manyoni,Mosses Matonya,anayefuata ni mweka hazina wa CCM wiilaya ya
Manyoni, Hersi, Katibu wa UVCCM na Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Fatuma
Toufik (mwenye miwani).
Mmoja wa wanachama wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni akipiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa jumuiya hiyo.
Msimamizi wa uchaguzi wa jumuiya ya wazazi Manyoni, ambaye ni katibu msaidizi CCM wilaya ya Singida vijijini Johari Seleman,akitoa maelekezo ya mkutano mkuu wa uchaguzi kabla zoezi la uchaguzi halijaanza.
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni Hemed Salum Hamad ambaye alijitoa ghafla,akisaini hati ya kitendo chake cha kutoa jina kwa hiari yake mwenyewe.
Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi aliyepita bila kupigwa,Yahaya Omari Masare akisaini hati ya kuchaguliwa kwake kwenye nafasi hiyo ya uenyekiti.
Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Manyoni,Yahaya Omari Masare akiwapungia kwa furaha wapiga kura wake kwa kitendo cha kumpitisha bila kupingwa.
Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi CCM Yahaya Masare akipongezwa na mwanachama wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya
wazazi CCM wilaya ya Manyoni, Yahaya Omari Masare (kulia) na mwenyekiti
wa zamani wa jumuiya hiyo,mzee Hemed Salum Hamad.
HABARI KAMILI:
Aliyekuwa
mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni mkoani Singida, Hemed
Salum Hamad (65) ameushangaza mkutano mkuu wa uchaguzi kutoka na
kitendo chake cha kujitoa ghafla kutetea nafasi yake.
Kitendo hicho hiyo kitendo kimepelekea mpinzani wake Yahaya Omari Masare (52) kupita bila kupingwa.
Awali
mzee Hemed akiwa na viongozi wenzake wa kipindi kilichopita wakati
wakijiuzulu ili kupisha uchaguzi kufanyika, katika nasaha zake, alisema
atatetea nafasi yake hiyo.
Baada
ya wagombea hao kusimama mbele ya wapiga kura, kwa mshangao mkubwa mzee
Hemed alisema anatoa jina lake katika kinyang’anyiro hicho cha nafasi
ya mwenyekiti wa jumuiya wa wazazi.
Kutokana
na mzee kuondoa jina, msimamizi Johari alimtangaza Yahaya Omari Masare,
kuwa mwenyekiti mpya wa wazazi wilaya ya Manyoni, kwa kipinid cha miaka
mitano ijayo.
Masare
ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Azirona ya Itigi, Juni mwaka huu,
pia alipita bila kupingwa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa wazazi kata ya
Itigi.
No comments:
Post a Comment