Monday, September 10, 2012

SERENGETI FIESTA 2012 JINSI ILIVYO TINGISHA SINGIDA

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cirryl a.k.a Kamikazi akikamua jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

             Ni Kushangweka tu ndani ya viwanja vya Singida Motel usiku huu

 Rich Mavoco akiwaimbisha mashabiki wake waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu,ambapo wakazi wa mji huo wamejitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza kwenye tamasha hili

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shillole akijimwaya mwaya jukwaa mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Singida (hawapo pichani),usiku huu. 

  Pichani juu na chini Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye viwanja vya Singida Motel ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea

  Pichani kati ni msanii wa bongofleva kutoka THT,Recho akiwa sambamba na dansaz wake jukwaani wakikamua vilivyo. 

 Baadhi ya wakazi wa Singida waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta wakishangilia jambo.

 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mabeste na msanii mwenzake wakitumbuiza jukwaani usiku huu

 Pichani ni Ofisa Mahusiano wa kampuni  Clouds Fm,Simalenga akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini,Mh Queen Mlozi pamoja na nduguze wakishuhudia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea usiku huu kwenye viwanja vya Singida Motel,Mkoani Singida ambapo wakazi wa mji huo wameitikia wito wa kujitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya

  Anaitwa Ben Paul mmoja wa wasanii mahiri wa Bongofleva katika miondoko ya R&B


 Shillole akiwapa dole mashabiki wake waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu.

 Pichani kulia ni Dj Zero akiwa amepozi mtangazaji wa kipindi cha XXL,wote wafanyakazi wa Clouds FM wakishoo love usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya viwanja vya Singida Motel.

No comments:

Post a Comment