Friday, May 17, 2013

Mtoto wa miaka 3 auawa kwa kushambuliwa na nyuki,Mtu mmoja agogwa na gari,wafanyabiashara 10 wajeruhiwa vibaya Mkoani Singida.

Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP. Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya matukio matatu tofauti yaliotokea Mkoani Singida.

Watu wawili mkoani Singida,wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo la mtoto mwenye umri wa miaka mitatu kushambuliwa na nyuki na kusababisha kifo chake.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Geofrey Kamwela alimtaja mtoto aliyeshambuliwa na nyuki kuwa ni Japhet Mahenda mkazi wa kijiji cha Ighombwe jimbo la Singida mashariki.

Alisema Mei 11 mwaka huu saa nne asubuhi,Japhet wakati akicheza na watoto wenzake, walianza kuua nyuki wachache waliokuwa
katika eneo walilokuwa wakicheza.

Kamwela alisema ghafla nyumi wote waliokuwa kwenye mziga waliwavamia watotro hao na kuanza kuwashambulia.Watoto wengine ambao walikuwa na umri mkubwa kuliko Japhet,waliweza kukimbia na kumwacha Japhet akiendelea kushambuliwa na nyuki.

“Jephet alishambuliwa na kupelekea kuzirai na alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika zahanati ya kijiji cha Ighombwe,” alisema.

Katika tukio jingine,Kamanda Kamwela alisema mkulima mkazi wa kijiji cha Utahao wilaya ya Ikungi Ramadhani Shabani (49) Mei 12 mwaka huu saa 2.30 usiku katika barabara kuu ya Singida-Dodoma, aligongwa na gari ambalo hadi sasa bado halijafahamika.

Alisema Ramadhani wakati akigongwa alikuwa ametumia pombe kiasi cha kutosha.Jeshi la polisi linaendelea kulisika gari hilo.

Wakati huo huo, kamanda huyo alisema wafanyabiashara 10 wa minadani wilayani Manyoni,wamejeruhiwa vibaya baada ya gari T.386 ADK Isuzu mali ya Hezron Ephrem kuacha barabara na kupinduka.

Alisema tukio hilo limetokea Mei 13 mwaka huu saa tatu asubuhi wakati wafanyabiashara hao wakitoka Manyoni kwenda mnada wa kata ya Heka. Dereva wa Isuzu hilo Mathias ametoroka na kukimbilia kusikojulikana mara baada ya ajali hiyo kutokea.

“Majeruhi sita waliweza kutibiwa na kuruhusiwa. Majeruhi ambao hali zao bado sio nzuri ni Lameck Amosi (33), Mahenga John (36) ameumia kichwani na usoni na kuvunjika mkono wa kulia, Amri Lugoya (53) amevunjika mkono wa kulia na Marco Joseph (25) amevunjika mguu wa kushoto, hawa bado wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Manyoni,” alisema Kamanda Kamwela.

No comments:

Post a Comment