Friday, May 17, 2013

Uzembe wa mama lishe kusahau kuzima moto wasababisha Vibanda vinne kuteketea kwa moto mkoani Singida.


Kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake kuhusiana na tukio la moto (Picha zote kutoka maktaba).


Vibanda vinne vya biashara vinavyozunguka soko kuu la Manyoni mjini mkoa wa Singida, vimeteketea kwa moto unaodaiwa kusababishwa na mamalishe kusahau kuzima moto wakati akifunga biashara yake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela amesema mtu wa kwanza kuuona moto huo ulioanzia kwenye kibanda cha mama lishe, ni mlinzi wa soko hilo aliyejulikana kwa jina la Jotamu Daud.

Kamanda huyo amesema moto huo baada ya kupamba zaidi, ulihamia kwenye vibanda vingine vya maduka ya nguo na kuteketeza vibanda hivyo na mali yote iliyokuwa ndani.

Kamanda Kamwele ametoa wito kwa mamalishe na babalishe kuhakikisha wanazima majiko yao ya  moto  mara tu wanapomaliza kufanya biashara zao ili kuzuia uwezekano wa kuwaka wakati wao hawapo.

1 comment: