Mkuu wa wilaya ya Singida.Queen Mlozi, akizungumza kwenye kikao cha mrejesho wa utafiti uliofanywa na timu ya ufuatiliaji na uwajibikaji jamii (Social Accountability Monitoring-SAM) kilichofanyika mjini Singida.Timu ya SAM kwa kushirikiana na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida,kwa pamoja walifanya utafiti juu ya uwajibikaji kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya.Kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida,Idd Mnyampanda nas kulia ni mwenyekiti wa kikao hicho,diwani wa kuteuliwa, Salma Kundya.
Mkuu wa ofisi ya shirika la Sikika kanda ya Dodoma,Norah Mchaki,akitoa ufafanuzi juu ya utafiti wa uwajibikaji katika vituo vya kutolea huduma vya halmashauri ya Singida.
Diwani wa kata ya Ilongero (CCM) wilaya ya Singida,Ramadhan Samwi, akichangia jambo kwenye kikao cha mrejesho wa utafiti uliofanywa kwa pamoja na timu ya SAM na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Singida, juu ya uwajibikaji katika vituo vya kutolea huduma ya afya.
Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,(wa pili kushoto) akifuatilia taarifa ya mrejesho wa timu ya SAM iliyotafiti uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya katika vituo vya afya vya halmashauri ya wilaya ya Singida.Wa kwanza kulia ni mwenyeiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida,Idd Mnyampanda na kushoto ni mwenyekiti wa kikao cha mrejesho wa utafiti uliofanywa na timu ya SAM chini ya shirika la Sikika.
HALMASHAURI ya wilaya ya Singida, inakabiliwa na upungufu wa watumishi 144 wa kada mbali mbali wa sekta ya afya, hali inayosababisha huduma za afya kutolewa bila kuzingatia ubora unaohitajika
Hayo yalisemwa na Katibu wa afya katika halmashauri hiyo,Severin Sosthenes, wakati akitoa majibu dhidi ya hoja zilizotolewa na timu ya ufuatiliaji uwajibikaji jamii (Social Accountability Monitoring – SAM) katika halmashauri hiyo.
Alisema halmashauri hiyo ina mikakati kadhaa ya kutatua tatizo la upungufu wa raslimali watu katika sekta ya afya.
Katika mikakati hiyo, alisema katika bajeti yao ya mwaka juzi, walitenga fedha kwa ajii ya watumishi wapya 110.
“Baada ya kutenga fedha hizo, tulizunguka vyuo mbali mbali kuhamasisha wanaomaliza masomo, waombe kuja kufanya kazi kwenye halmashauri yetu,na tukawahakikishia kuwalipa stahiki na stahili zao”,alifafanua katibu huyo.
Sosthens alisema pamoja na juhudi hizo, walifanikiwa kupata watumishi 47 wa kada mbali mbali ambao hadi sasa wanaendelea kufanya kazi katika halmashauri hiyo ingawa idadi inayohitajika bado haijafikiwa.
Katika hoja yake hiyo, timu ya SAM ilitaka kujua ni jinsi gani