Wednesday, October 23, 2013

FAHAMU SABABU ZINAZOCHANGIA BENKI YA NMB KUWA NA FOLENI NDEFU KULIKO BENKI ZINGINE.

 Meneja wa NMB kanda ya kati, Gabriel Ole Loibanguti akitoa nasaha zake kwenye simena iliyohudhuriwa na wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB.
 Katibu wa klabu ya wanachama wafanyabiashara wa benki ya NMB tawi la Singida,Welu Daniel akitoa nasaha zake kwenye semina ya wananchama hao siku moja iliyofanyika kwenye ukumbi wa Aque Vitae mjini Singida.
 Mwezeshaji wa semina ya siku moja iliyohudhuriwa na wanachama wa klabu ya wafanyabiasha wateja  wa NMB tawi la Singida, Meneja mikopo makao makuu ya NMB jijini Dar-es-salaam,Prisca Pius akitoa mada zake mbalimbali.
 Baadhi ya wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB tawi la Singida waliohudhuria semina ya siku moja iliyohusu kukumbushwa juu ya haki zao kama wateja.
 Baadhi ya viongozi wa NMB waliohudhuria semina ya siku moja ya wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB tawi la Singida.

Meneja wa NMB benki kanda ya kata,Gabriel Ole Loibanguti amewahimiza wateja kujenga utamaduni wa kutoa mapendekezo,maoni na ushauri juu ya uendeshaji wa huduma mbalimbali,ili ziweze kuboreshwa zaidi ziweze kukidhi mahitaji yao.

Loibanguti ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye semina ya siku moja iliyohudhuriwa na wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wa tawi la NMB Singida. Semina hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque Vitae mjini Singida.

Amesema huduma bora zinazotolewa na NMB ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa wateja wengi kuikimbilia benki hiyo,ubora huo umechangiwa na maoni,mapendekezo na ushauri uliotolewa na wateja.

“Kwa hiyo, mimi nisisitize tu kwamba msichoke kutoa maoni,mapendekezo na ushauri wenu juu ya uboreshaji wa huduma zetu.Niwahakikishie kuwa tunajali na kuyafanyia kazi maoni,mapendekezo na ushauri wenu”,amesema meneja huyo wa kanda.

Aidha,Loibanguti alitumia fursa hiyo kuwashauri viongozi wa vilabu vya wananchama wafanyabiashara wa NMB kutembeleana baina ya vilabu ili pamoja na mambo mengine kubadilishana uzoefu kwa manufaa ya ustawi wa NMB.

Kwa upande wake mwezeshaji wa semina hiyo meneja wa masoko kutoka makao makuu ya NMB jijini Dar-es-salaam, Prisca Pius amesema foleni ndefu zilizopo kwenye matawi ya NMB nchini,zinachangiwa na
huduma bora zinazotolewa na benki hiyo yenye wateja lukuki.

Prisca alitaja sababu zingine zinazovutia wateja wengi kujiunga na NMB ni benki hiyo kuwa na matawi mengi nchini kuliko benki zingine na kwamba ina mashine zaidi ya 500 na kuifanya iongeze kwa huduma hiyo nchini.

“Benki ya NMB ni benki ya watu wa ngazi zote tofauti na benki zingine. Kwa hiyo niwahakikishie wateja kwamba wasiwe na hofu na idadi kubwa ya wateja wa NMB, tumejipanga vema kukabiliana na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya wateja”,amesema meneja masoko huyo.


Katika hatua nyingine,Prisca alikumbusha kwamba benki ya NMB  haitoi mikopo ya kuanzisha biashara isipokuwa inatoa mikopo ya kusaidia tu kuendeleza biashara.

No comments:

Post a Comment