Sunday, October 20, 2013

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE WAWILI KUJERUHIWA MKOANI SINGIDA



Mtu mmoja amefariki baada ya kupigwa risasi kifuani na mwingine kujeruhiwa mikono yote miwili baada ya watu wasiojulikana kuwavamia na kutaka kuwapora mali katika wilaya ya manyoni mkoani Singida.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Igwamadete kata ya iseke tarafa ya Nkonko wilayani manyoni baada ya mtu aliyejulikana kwa jina la Alody Joshua mwenye umri wa miaka 29 kupigwa risasi na majambazi hao
Aidha Daudi Azaliwa amejeruhiwa mikono yote miwili baada ya kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakitoka kwenye mnada wa Mpapa kuelekea nyumbani ndipo majambazi hao walipoanza kuwapiga na kuwanyanganya  fedha na kusababisha  kifo cha mtu huyo.

Jeshi la polisi wilayani manyoni limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa watu watatu
wanashilikiwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo na kwamba wanatarajiw akufikishwa mahakamani baada ya upelelzi kukamilika

No comments:

Post a Comment