Thursday, August 21, 2014

Zaidi ya wananchi 3,000 Wilaya ya Ikungi Singida kunufaika na soko la asali chini ya mradi wa FU-DI kwa ufadhili wa UNDP.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akizungumza na wanavikundi 49 vya ufugaji wa Nyuki katika Wilaya ya Ikungi wakati wa uzinduzi wa mradi wa FU-DI na ugawaji wa mizinga ya Nyuki pamoja na vifaa.
Meneja wa mradi wa FU-DI BBonifasi Leso akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Ikungi.
Afisa mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyanya akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mratibu wa mradi wa Nyuki Wilayani Ikungi, Jonathan Njau akitambulisha mradi wake kwa mkuu wa mkoa wa Singida.

Wakala wa Nyuki kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Philemon Kiemi akitoa maelezo kwa mkuu wa Mkoa wa Singida na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kwenye moja ya mabanda ya kutunzia mizinga ya yenye Nyuki.
Mkuu wa Mkoa wa Singida akiangalia mizinga ya Nyuki katika kijiji cha mahambe kilomita tatu kutoka Ikungi mjini.
Banda lenye mizinga ikiwa imehifadhiwa tayari kwa ajili ya kuingiza Nyuki eneo la kijiji cha Mahambe.
Hii ni sehemu ya mizinga ya Nyuki iliogawanywa na mkuu wa mkoa wa Singida.
 Mizinga ya kienyeji yenye Nyuki ikiwa juu ya miti.

ZAIDI ya wananchi 3,000 watanufaika na soko la asali kupitia taasisi ya Kijamii  ya fursa za kimaendeleo ‘Future Development Initiatives’ (Fu-DI) Mkoani Singida, kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Wakizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi, ugawaji, usambazaji wa mizinga na vifaa vya kurinia asali kwa Vijiji 49 Wilayani Ikungi, baadhi ya wanakikundi akiwemo Janeth Samwel, Christina Chima na Daudi Petro wamesema mpango huo utasaidia sana kuboresha maisha ya jamii ya Vijijini.

Walisema kuzinduliwa kwa mradi huo kutasaidia vijana kupata ajira ikiwa ni pamoja na kuondokana na ukataji miti hovyo na kuchoma mkaa hali inayoashiria iharibifu wa mazingira.

Manyanya alisema kuwa mradi huo unaenda sambamba na utunzaji wa mazingira , na hivyo kuwepo kwa uoto wa asili na uhifadhi wa misitu.hivyo shirika litaendelea kutoa misaada zaidi katika mkoa wa Singida hasa sekta ya kilimo

Akizindua mradi, kugawa mizinga na vifaa vya kurina asali, Mkuu wa Mkoa Dkt.Parseko Kone amesema asali ni zao lililopewa kipaumbele kwa biashara Mkoani humo, mengine ni Alizeti,Vitunguu na Pamba.

Kone alisema Wilaya ya Ikungi kuna miti aina na mazao mbalimbali yenye maua yanayofaa  kwa chavua kwa ajili ya kuzalisha asali nyeupe, huku uwezo wa Mkoa huo ni kuzalisha tani 11,000 za asali kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment