Sunday, May 11, 2014

Waliopoteza maisha katika ajali Ikungi waombewa.

Diwani wa kata ya Mungaa Matheo Alex akizungumza kwenye hafla ya sala kuwaombea watu waliopoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya summary aprili 28 mwaka huu.Sala hiyo maalum,imefanyika jana eneo ilikotokea ajali hiyo.
Mke wa marehemu mwenyekiti wa kijiji cha Utaho Paulo Hamisi (41) aliyefariki dunia kwa kugongwa na basi la Summry Aprili 28 mwaka huu.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Utaho tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi,waliohudhuria sala maalum ya kuwaombea ndugu zao 15 waliopoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kamuni ya summry Aprili 28 mwaka huu.

WAUMINI wa madhehebu mbalimbali ya dini wakazi wa kata ya Utaho tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi mkoa wa Singid hivi karibuni wameungana na kufanya sala maalum katika kuwaombea ndugu zao 15 waliofariki dunia baada ya kugongwa na basi la kampuni ya summary.

Sala hiyo maalum imefanyikia kando kando ya barabara kuu itokayo Singida – Dodoma eneo la kambi la kampuni ya SIETCO kijiji cha Utaho  ajali hiyo mbaya ilitokea Aprili 28 mwaka huu saa 2.45 usiku.

Akihubiri kwenye hafla hiyo ya sala,Mchungaji wa kanisa la Free Pentekoste kijiji cha Utaho,Francis Pius amewataka waumini wa dini mbalimbali na wananchi kwa ujumla wazingatie sheria za usalama barabarani kama njia mojawapo ya kupunguza ajali zinazochangia watu kupoteza maisha pamoja na mali zao.

Amesema baada ya kujengwa barabara kwa kiwango cha lami ajali zimeongezeka mara dufu kutokana na baadhi ya watu kutokuwa waangalifu na kwa kiasi kikubwa kutokutii sheria za usalama barabara.

“Tabia ya watu kutokuzingatia sheria za usalama babarani inachangia mwenye baiskeli kumdharau mwenye pikipiki na mwenye pikipiki kumdharau mwenye gari kinachotokea ni kwamba wananyang’anyana barabara na kusababisha ajali zinazopoteza maisha ya watu na mali zao”alifafanua zaidi Mchungaji

Mchungaji huyo amesema makosa ya aina hiyo,hayapaswi kufanywa na binadamu mwenye akili tofauti na mnyama kwa hiyo tunapaswa kuzingatia matumizi sahihi ya barabara ili kupunguza ajali.

 “Tuwe makini wakati wa kuvuka barabara na pia wakati tukivusha mifugo yetu tukifanya dharau barabarani kuwa dereva wa gari,pikipiki na hata baiskeli eti atakuona ili asikugonge tutakosea sana kwa sababu tutakuwa tunasababisha ajali kila kukicha”,amesema Mchungaji Francis.

Akifafanua zaidi,amesema
barabara za kiwango cha lami ni nzuri  na zina faida nyingi pamoja na kuharakisha upatikanaji wa maendeleo,lakini tunapaswa tuzingatie matumizi bora ya barabara ili tusiendelea kupukutika kwa ajali.

Naye Diwani wa kata ya Kituntu (CCM),Naftali Gwae alikanusha uvumi kuwa Rais Jakaya Kikwete alituma rambai rambi zikiambatana na fedha.

“Rais wetu alituma salama za rambi rambi na wala sio fedha kwa hiyo ndugu zangu niwasihi tu kwamba wakati huu mgumu unaoambatana na majonzi mengi yatasemwa lakini tuwe makini na kuyafanyia uchunguzi kwanza”,amesema.

Aidha,uvumi ulioenea kwamba Diwani wa CCM na Mtendaji wamechukua kutoka ofisi ya kijiji nyaraka za benki zinazodaiwa kuonyesha kuwa kijiji hicho kina akaunti yenye zaidi ya shilingi milioni mia moja si za kweli ni uongo mtupu. 


Kwa mujibu wa Diwani Gwae baada ya sala hiyo waathirika wa ajali hiyo kila moja amepewa shilingi 212,500 ikiwa ni rambarambi kwa kupoteza ndugu.Fedha hizo ni kutoka fedha za ubani za shilingi 5 milioni zilizotolewa na mmiliki wa kampuni ya summary na shilingi laki moja zilitolewa Mkuu wa mkoa wa Singida na shilingi 150,000 zilizotolewa na wakazi wa kijiji cha Minyinga.

No comments:

Post a Comment