Friday, April 12, 2013

Serikali mkoa wa Singida yatenga maeneo rasmi kwa ajili ya wawekezaji.

 Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, (anayeangalia kamera) akizungumza kwenye mkutano kati yake, kaimu katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara Dk.Shabani Mwinjaka na mwekezaji wa kiwanda cha ngozi Bw. Takuya  Miyaguchi.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk.Shaban Mwinjaka (wa kwanza kushoto) Mwekezaji wa kiwanda cha ngozi mkoa wa Singida Bw. Takuya Miyaguchi na  Afisa Mipango wa halmashauri ya manispaa ya Singida, Godard Mwakalukwa wakifurahia jambo na mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi (hayupo kwenye picha).
 Kaimu katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara, Dk.Shaban Mwinjak (wa pili kulia) akimwonyesha mwekezaji wa kiwanda cha ngozi Bw. Takuya Miyaguchi (wa kwanza kulia) eneo atakalojenga kiwanda chake cha ngozi katika kijiji Kisaki kitongoji cha Ng’aida manispaa ya Singida. Wa kwanza kushoto ni mshauri wa wizara ya viwanda na biashara na anayefuata ni Afisa Mipango wa manispaa ya Singida, Godard Mwakalukwa.
Mwekezaji wa kiwanda cha ngozi katika manispaa ya Singida Bw.Takuya Miyaguchi (aliyenyoosha mkono juu) akiangalia eneo atakalojenga kiwanda chake katika kijiji cha Kisaki kitongoji cha Ng’aida manispaa ya Singida. Kulia ni mshauri wa wizara ya viwanda na biashara kutoka serikali ya Japan.

Serikali  ya wilaya ya Singida imeiomba wizara ya viwanda na biashara iongeze kasi ya kuhamasisha wawekezaji wengi kuja mkoa wa Singida kwa madai kwamba mkoa una maeneo mengi ya kuwekeza.
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, wakati akizungumza kwenye mkutano wa pamoja kati yake, mwekezaji wa kiwanda cha ngozi na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na biashara Dk. Shaban Mwinjaka.
Amesema kwa upande wa wilaya yake wametenga eneo la
Ngaida katika kata ya Kisaki manispaa ya Singida lenye ukubwa wa hekta 69 kwa ajili ya kujenga viwanda vikubwa na vidogo.
Mlozi amesema eneo hilo lipo kando kando ya barabara kuu ya Dar-es-salaam- Mwanza, kuna maji mengi na muda si mrefu kutapatikana umeme wa kutosha utakaozalishwa kwa njia ya upepo.
“Kwa ujumla sisi hivi sasa tumejiweka vizuri kwa ajili ya kupokea wawekezaji wakiwemo wa viwanda vikubwa.Tunashukuru kwa ujio wa kampuni ya kijapan ya Nitori Holdings ambayo inatarajia kujenga kiwanda cha ngozi katika eneo la Ng’aida”alisema Mlozi huku akitabasamu.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa mbali na kampuni hiyo ya kijapan,yapo makampuni mengine matatu yameonyesha nia ya kuja wilaya ya Singida,kufungua viwanda.

No comments:

Post a Comment