Sunday, June 1, 2014

Watanzania washauri kupata elimu ya kuendesha biashara.

Mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB tawi la Singida,Kyoma (katikati) akifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa kwenye semina yao ya siku moja.Wa kwanza kulia ni katibu wa klabu hiyo,Welu Ntandu na kushoto ni makamu mwenyekiti,Elizabeth Masawe.
Meneja Mahusiano na Biashara wa makao makuu NMB jijini Dar-es-salaam, Dickson Mpangarawe (wa kwanza kushoto),akifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina ya siku moja iliyohudhuriwa na wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wa tawi la NMB Singida.Wa pili kushoto,ni Meneja wa tawi la benki ya NMB Singida, Christine Mwangomo.
Mwezeshaji Isack Mnyagi, akitoa mada yake ya ujasiriamali kwa wanachama wa klabu ya wafanyabiashara wa tawi la NMB Singida mjini kwenye semina ya siku moja iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque Vitae.
Afisa elimu kwa wafanyabiashara TRA mkoa wa Singida,Zakaria Bwagilo,akitoa mada yake ya umuhimu wa kulipa kodi kwenye semina iliyohudhuriwa na wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wa tawi la MNB Singida mjini.

WATANZANIA wanaotarajia kuanzisha shughuli za biashara za aina mbalimbali wameshauri kujenga utamaduni wa kupata elimu na mafunzo ya uendeshaji wa biashara kwanza kabla ya kuanzisha biashara husika.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Integrity Foundation la jijini Dar-es-salaam,Isack Mnyagi wakati akitoa mada ya ujasiriamali  kwa wanachama wa klabu ya wafanyabiashara wa benki ya NMB tawi la Singida.

Amesema uzoefu unaonyesha wafanyabiashara wengi ambao huanzisha biashara bila kuwa na elimu ya kutosha ya biashara,hufilisika kwa kipindi kifupi.

Akifafanua zaidi,amesema “Watu wengi huanzisha biashara kwa kuiga au kutokana na kiburi chao kwamba wanajua kila kitu.Biashara za sasa sio sawa na zile za zamani ambazo zilikuwa na faida ya shilingi kwa shilingi.Biashara za sasa zina ushindani mkubwa kwa hali hiyo, zinahitaji mtu anayetaka kufanya biashara,ahakikishe ana elimu ya kutosha juu ya kuendesha biashara”.

Katika hatua nyingine,Mnyagi amewataka kupiga vita vitendo vya familia kutumia bidhaa za duka bila kulipa kwa madai kwamba vitendo hivyo vinachangia kwa kiasi kikubwa kufilisi duka.

“Pia msipende kununua bidhaa za
wizi,bidhaa za wizi zinaweza kuwa na bei ya chini mno,lakini ukikamatwa nazo zitasababisha ufilisiwe au ufungwe jela”,amesema Meneja huyo.


Wakati huo huo,Mnyagi amewahimiza kujenga mahusiano mazuri baina yao ili waweze kupata fursa ya kubadilishana uzoefu wa kuendesha biashara na kukopeshana fedha kwa ajili ya kupanua biashara zao.

No comments:

Post a Comment