Sunday, June 1, 2014

Kinana amaliza ziara yake Mkoani Singida kwa kuzuru Singida Vijijini.

Mbunge wa Singida Mashariki Lazaro Nyalandu akimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo wa Chama,  katika kata ya Msisi, Singida Vijijini, jana Mei 26, 2014.
Wanachama wa Jumuia ya Wazazi Kata ya Msisi wakimvalisha mgolole Kianana kabla ya kufungua tawi la Wazazi la Kata hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua tawi la Jumuia ya Wazazi Kata ya Msisi, wilaya ya Singiga Vijijini.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki kuvuna mtama katika shamba la mfano la zao hilo katika kata ya Mtinko, Singida Vijijini, Jana. Aliyevaa suti ni Waziri wa maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Mashariki, Lazaro Nyalandu.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwasha mashine ya kupukuchua mtama, wakati yeye na Kinana waliposhiriki uvunaji na upuchuaji mtama kwenye shamba darasa la zao hilo katika kata ya Mtinko, Singida Vijijini.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akishiriki kupukuchua mtama kwenye mashine maalum, katika Kata  hiyo.
Kinana na Nyalandu wakiweka dirisha kwenye jengo la mradi wa ushirika wa kusindika mafuta ya alizeti kata ya Mtinko.
Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msisi katika mapokezi yake kuingia Singida Vijijini.
Wananchi wakiwa nje ya Zahanati ya Mkange, Singida Vijijini, wakati Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alipokagua zahanati hiyo mpya jana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alimpatia chanjo ya matone, mtoto Erick Gabriel mwenye umri wa miezi miwili, aliyepatakwa na mama yake, Maria Jacob, Kiongozi huyo mkuu wa CCM, alipokagua huduma za  zahanati ya Mkenge, Singida Vijijini jana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiondoka na msafara wake  baada ya kukagua jengo la bweni la wanafunzi Maghojoa, Singida Vijijini.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiwa na Nyalandu wakati alipozungumza na wananchi baada ya kukagua ujenzi wa Ukumbi wa Ofisi ya CCM, Kata ya Maghojoa, Singida Vijijini.
Nyalandu akisalimiana na wananchi wakati alipowasili na Kinana katika kata ya Mtinko, Singida Vijijini.
Kinana akihutubia wananchi Kata ya Mtinko, Singida Vijijini.

No comments:

Post a Comment