Basi la ABC T.433 CVL linaloendeshwa na dereva mbunifu,Gabriel Joseph.
Dereva wa basi la kampuni ya ABC,Gabriel Joseph ifanyayo safari zake kati ya Singida-Dar-es-salaam apongezwa kwa nidhamu yake ya kuwajali wateja wake kwa kuwaita ni sehemu ya familia ya kampuni ya ABC. Pichani ni Dereva Gabriel,a kitoa matangazo mbalimbali wakati wa safari ikiwemo kuwahimza wanafamilia kuhakikisha wamefunga mikanda ya usalama.
DEREVA wa kampuni ya mabasi ya ABC yafanyayo safari zake kati ya Singida na Dar-es-salaam, Gabriel Joseph, amepongezwa kwa hatua yake ya kupandisha hadhi ya wateja wake kwa kuwabatiza jina la wanafamilia wa ABC, badala ya jina la abiria lililozoeleka kwenye vyombo mbalimbali vya usafiri.
Gabriel pamoja na kupandisha hadhi ya abiria wake na kuwaita wanafamilia ya ABC, pia amebuni mbinu mpya ya kuwavutia wanafamilia wa ABC,kwa kuwapa taarifa za mara kwa mara pindi wanapomaliza wilaya na mkoa husika na kuwaarifu wanaingia wilaya nyingine na kutaja mkoa na kilometa za kutembea katika wilaya hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafamilia hao waliokuwa wakisafiri na basi T.433 CVL lililokuwa likiendeshwa na Gabriel,wamedai kwamba kuitwa
wanafamilia wa ABC, kumechangia waipende zaidi kampuni hiyo kwa imani kwamba wamethaminiwa mno na kuheshimiwa.
wanafamilia wa ABC, kumechangia waipende zaidi kampuni hiyo kwa imani kwamba wamethaminiwa mno na kuheshimiwa.
“Huyu dereva kijana Gabriel, amebuni mambo mazuri mno. Kwanza pale Singida mjini basi lilichelewa kuondoka kwa muda wa dakika tatu tu, alipoingia na kushika usukani kabla ya kuondoka alituomba radhi kwa kutupotezea muda wetu wa dakika tatu. Huo kwanza ni ustarabu uliopea watu wengi dakika tatu wangeziona ni kitu kidogo.
Binafsi nawaomba madereva wengine waige mfano wa Gabriel”, alisema mmoja wa wasafiri wa siku hiyo Godfrey Lida.
Godfrey alisema dereva Gabriel ameenda mbali zaidi kwa kitendo chake cha kuwafahamisha wanafamilia wa ABC maeneo mbalimbali muhimu, yakiwemo ya eno la kijiji cha Sukamahema wilaya ya Manyoni palipowekwa alama na wajerumani ya kuonyesha kuwa mahali hapo ndio katikati ya nchi.
“Maeneo mengine ambayo baadhi ya wasafiri tulikuwa hatuyajui, ni bonde la ufa, mlima saranda, majengo ya Bunge la Jamhuri na eneo ambalo Waziri Mkuu Edward Sokoine alipata ajali na kupoteza maisha”, alifafanunua zaidi msafiri huyo.
Godfrey alisema kwa ujumla dereva Gabriel kutokana na ubunifu wake huo,wanafamilia wa ABC wanaotumia basi lake wanajisikia kuwa ni watalii wa ndani kwa kitendo cha kuwatambulisha mambo/maeneo muhimu ambayo wengi hawayafahamu.
Naye Mzee Mjengi Gwao,licha ya kuipongeza kampuni ya mabasi ya ABC, kwa madai kwamba madereva wake wengi wana waledi wa hali ya juu katika kutii sheria za usalama wa barabarani,pia watumishi hao ni waaminifu na wanaheshimu mno wateja wao.
Kwa mujibu wa dereva Gabriel,wanafamilia wengi wa ABC mara nyingi wakifika safari yao,huwa kwanza wanamuaga na kumuuliza ni lini anarudi Singida au Dar-es-salaam,ili waweze kuwemo kwenye safari siku husika.
No comments:
Post a Comment