Tuesday, September 16, 2014

Mil 500 kutumika zoezi la Chanjo ya Surua na Rubella Mkoa wa Singida.7

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone.

MKOA wa Singida, unatarajia kutumia zaidi ya shilingi 500 milioni kwa ajili ya kugharamia zoezi la kampenin ya taifa ya chanjo mpya ya surua na rubella, kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 15.

Zoezi hilo la nchi nzima,linatarajiwa kuanza mwezi huu wa septemba kuanzia tarehe
24 hadi 30.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, ametoa wito kwa wananchi kutekeleza wajibu wao kuhakikisha wato wenye sifa ya kupata chanjo hizo wanaipata.

Alisema serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii, inatarajia kutoa chanjo hiyo mpya yenye nguvu na uwezo wa kuzuia magonjwa mawili kwa pamoja ambayo ni surua na ugonjwa wa rubella.

Dk.Kone alisema magonjwa hayo mawili kwa kiwango kikubwa ndiyo yanayochangia vifo na ulemavu kwa watoto chini ya miaka 15.

Aidha, alisema ugonjwa wa rubella zake zinafanana sana na ugonjwa wa surua.

“Nawaagiza viongozi wa siasa, madhehebu ya dini, watendaji na watu wote mashuhuri na maarufu,kuitikia wito huu na kujitoa kwa ajili ya watot6o wetu kwa kudhibiti kila aina ya changamoto ili kufanikisha chanjo hii mpya”, alisema mkuu huyo wa mkoa.

No comments:

Post a Comment