Kaimu Katibu Mkuu wa kikundi cha Aminika Antony Muhenyi akisoma agenda ya mkutano huo maalumu kwa wanachama wa Aminika.
Wananchi wa kijiji cha sambaru wakimsikiliza meneja wa Shanta.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Sambaru akigongesha na Meneja wa Shanta.
KAMPUNI ya uchimbaji wa Madini ya dhahabu ya Shanta mining Limited iliyopo katika kijiji cha Sambaru Kata ya Mang’onyi Wilayani Ikungi, imekabidhi hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4.23 kwa kikundi cha Aminika .
Msaada huo umekabidhiwa kwa bodi ya Wakurugenzi wa kikundi hicho cha Aminika jana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Shanta, Zone Swanepoel katika kijiji cha Sambaru yaliko makao makuu ya Aminika.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya hundi hiyo Meneja huyo aliwataka wanachama na wanakikindi cha Aminika kuzitumia fedha hizo katika matumizi yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
“Ni matarajia yangu fedha hizo zitakuwa ni mwanzo mzuri wa kuanza kazi yenu ya uchimbaji wa dhahabu, na sitegemei kusikia malumbano ya kugawana hizi fedha, bosi wangu ametoa kwa moyo wake baada ya kuona umoja wenu.” Alisema Swanepoel.
Swanepoel alisema kuwa Kampuni itaendelea kutoa ushirikiano baina ya jamii inayozunguka mgodi wao, ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa vijana ndani ya mgodi huo pindi utakapoanza kazi ya uzalishaji.
Aidha alisema wakati wa kukabidhi leseni tatu kwa kikundi cha Aminika Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Shanta aliahidi kutoa dola USD 25,000 za kimarekani mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini Steven Masele mapema Mwezi Mei mwaka huu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Aminika Gold Mine Cooperative Society Limited, Francis Mbasa alishukuru Kampuni ya Shanta kwa kuweza kutimiza ahadi yake kwa wakati muafaka.
Aidha Mbasa alisema kikundi chake kitaendelea kutoa ushirikiano kwa Kampuni hiyo katika kuhakikisha kuwa mahusiano baina ya kampuni na jamii inayowazumguka yanakuwa mazuri wakati wote.
No comments:
Post a Comment