Baadhi ya madereva wa boda boda mkoa wa Singida, wakiwa kwenye maandamano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya boda boda kitaifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Peoples klabu mjini hapa.Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Dk.Harrison Mwakyembe,ameagiza SUMATRA kuandaa mikakati itakayosaidia kuanzishwa kwa benki ya boda boda nchini,itakayosaidia wafanyabiashara hao kupata mikopo kwa ajili ya kuboresha uchumi wao.
Waziri wa uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe, akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya boda boda kitaifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Peoples klabu mjini Singida.Ameagiza SUMATRA kuandaa mikakati itakayosaidia kuanzishwa kwa benki ya boda boda nchini,itakayosaidia wafanyabiashara hao kupata mikopo kwa ajili ya kuboresha uchumi wao.
Meneja wa shirika lisilo la kiserikali la Anti Poverty and Envirinment Care, Respicius Timanywa, akitoa taarifa yake ya utoaji wa mafunzo kwa waendesha pikipiki kwa lengo la kupunguza maafa na kuandaa ajira,kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya boda boda kitaifa yaliyofanyikia mjini Singida.
Waziri wa uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi wa shirika la APEC,linalotoa mafunzo ya uendeshaji bora na unaozingatia sheria za usalama barabarani kwa waendesha pikipiki.Wa kwanza kushoto ni kamanda wa polisi mkoa wa Singida, ACP.Thobias Sedoyeka anayefuatia ni mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone.Wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi na mwenye shuka ya rangi ya zambarau,ni meneja wa shirika la APEC,Respicius Timanywa.
WAZIRI wa uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe, ameiagiza SUMATRA ishirikishe wadau mbalimbali kuandaa mikakati itakayowezesha kuanzisha benki ya umoja wa wafanyabiashara ya boda boda nchini,na kuiwasilisha serikalini mapema iwezekanavyo.
Dk.Mwakyembe ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya boda boda nchini yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Peoples klabu mjini Singida.
Alisema biashara ya boda boda nchini imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kurahihisha usafirishaji maeneo ya vijijini na kwenye majiji yenye misongamano ya karibu kila kitu.
Dk.Mwakyembe alisema kutokana na ukweli huo,upo umuhimu mkubwa kuanzisha benki itakayosaidia kutoa mikopo kwa madereva wa boda boda,ili waweze kuboresha uchumi wao.
“SUMATRA kaeni na viongozi wa Umoja wa madereva wa boda boda na wadau mbalimbali itakayosaidia kuanzisha kwa benki ya taifa ya umoja wa wafanyabiashara wa boda boda”,alisema waziri huyo.
Katika hatua nyingine,Dk.Mwakyembe alisema zaidi ya shilingi trilioni tatu hutumika kila mwaka kwa ajili ya kugharamia hasara zinazosababishwa na ajali za pikipiki nchini.
Alisema kwa kipindi cha mwaka jana,jumla ya ajali 6,831 za pikipiki zilitokea hapa nchini na kusababisha vifo vya watu 1,098 na majeruhi 6,578.
Wakati huo huo,Dk.Mwakyembe,amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la Anti Poverty And Environment Care (APEC), kwa kutoa mafunzo kwa waendesha pikipiki kwa lengo la kupunguza maafa na kuandaa ajira.
No comments:
Post a Comment