Saturday, June 20, 2015

Ajali yaua sita na kujeruhi wengine 40 Singida.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu za kugombea urais.
Dereva wa lori kubwa RAC 317 N raia wa Uganda,Waguuma Mohammed, akizungumzia ajali ya lori lake kugongwa kwa nyuma na basi T.174 CAV mali ya Enock Mwita wa jijini Mwanza.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya ajali mbili tofauti ikiwemo ya basi ambazo zimeuawa abiria sita na kujeruhi abiria wengine 44.

Baadhi ya abiria waliojeruhiwa kwenye ajali ya basi T.174 CAV Nice Line Coach mali ya Enock Mwita kugonga lori na kuuwa abiria watano na kujeruhi abiria 39 saa mbili usiku, wakiwa wamelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida wakiendelea na matibabu.

Abiria Mwita Marwa aliyekuwa akisafiri na mke na watoto wao watatu wakitokea Dar-es-salaam kwenda kwao mkoani Mara kwa basi T.174 CAV la Nice line coach akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida baada ya basi hilo kugonga lori na kusababisha vifo vya abiria watano na kujeruhi 39.

WATU sita wamefariki dunia na wengine 40 kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao na wengine kukatwa miguu na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa mjini hapa, katika ajali mbili tofauti zilizotokea Mkoani Singida.

Miili ya abiria hao waliojeruhiwa wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa iliyopo mjini hapa, huku wengine sita kati yao wamepewa rufaa kwenda katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na wengine Hospitali ya KCMC, mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, SACP, Thobiasi Sedoyeka alisema ajali ya kwanza iliyohusisha basi la kampuni ya Nice Line Coach lenye namba za usajili T.174 CAV ya jijini Mwanza,ilitokea juni,11,saa mbili usiku katika eneo la Kijiji cha Manga,kilomita 11 kutoka mjini Singida, barabara kuu ya Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari, abiria wa basi hilo aliyekuwa akisafiri pamoja na mke wake, Ron Nairo alisema wao walikuwa wameketi kiti cha nyuma ya dereva na kwamba walipoondoka kituo cha mizani cha mjini Singida, ndipo dereva huyo alipoanza kukimbiza kwa mwendo kasi na kudai kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa hawezi kuona mbali nyakati za usiku.

“Tulipofika eneo la tukio kulikuwa na gari la kubebea maji lililokuwa limesimama katikati ya barabara baada ya kuharibika,dereva wetu alilishitukia kwa karibu na alipotaka kulikwepa ndipo tairi za nyuma ziligonga tofali la saruji   ukingo wa barabara na tairi hizo zilipasuka, kitendo hicho kilichosababisha dereva ashindwe kulimudu basi hilo”, alifafanua abiria huyo.

Aidha Nairo alisema basi hilo liliweza kugonga lori kubwa la mizigo lenye namba za usajili RAT.317N/RL.0754 m/benzi kwa nyuma na kuanzia mlango wa kuingilia na sehemu hiyo yote hadi nyuma ilikwanguliwa na hivyo kusababisha baadhi ya abiria kukatwa na kutoka sehemu mbili na wengine kukatwa miguu.

Hata hivyo alisema abiria huyo kuwa dereva aliyekuwa akiendesha basi hilo na mwenzake wa akiba mara baada ya kutokea kwa ajili hiyo walifanikiwa kutoroka pamoja na wafanyakazi wengine.

Kwa upande wake abiria Mwita Marwa alisema yeye,mke pamoja na watoto wao watatu walikuwa wakielekea kwao Mkoani Mara kwa shughuli za kimila, lakini ajali hiyo imesababisha akatike mguu wa kushoto na kuumia vibaya kichwani.

“Hadi sasa saa nne asubuhi na ajali imetokea jana jioni,sijui mke wangu yupo wapi wala watoto wangu wapendwa”,alisema Mwita kwa masikitiko.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Singida,Dk.Danaiel Tarimo amekiri kupokea miili ya watu watatu waliofia eneo la tukio na kwamba wawili kati yao wamefariki dunia wakati wakipatiwa matibabu.

Alisema katika ajali ya basi walipokea majeuri 39 na kati yao wanne wamekatwa miguu kutokana kusagwa vibaya na  wanaendelea vizuri na matibabu.

Aidha daktari huyo alisema kuwa miili ya abiria wawili imeishatambuliwa kuwa ni ya Shila Masanja na mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Yohana,na kuongeza kwamba miili mingine bado haijatambuliwa na ipo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa.

“Kuna ajali nyingine ambayo imetokea juzi asubuhi katika eneo la kijiji cha Kindai Manispaa ya Singida iliyohusisha gari aina ya Noah lenye namba za usajili T.998 CWG  lililoacha barabara na kupinduka na kusababisha kifo cha Febronia Kwayu (31) anayedaiwa alikuwa na ujauzito.

Alisema Noah hiyo iliyokuwa ikitokea Dar-es-salaam kwenda Kahama, Mkoani Shinyanga lilikuwa likiendeshwa na Paulo Bundala na kwamba lilipofika eneo la tukio lenye kona kali,dereva alishindwa kulimudu kutokana na kuwa kwenye mwendo kasi.

“Abiria waliojeruhiwa kwenye ajali ya Noah ni pamoja na Bundala Magembe (31),Witnes Marick (27),mwanafunzi Timotheo Simon (12),Agnes Longino (16) mwanafunzi wa sekondari na Helena Longino (24) wote wakazi wa Dar-es-salaam na wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa”,alisisitiza


Kwa mujibu wa kamanda Sedoyeka alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa madereva wote kuendesha vyombo vya usafiri kwa uangalifu huku wakizingatia sheria, kanuni, taratibu na matumizi sahihi ya barabara.

No comments:

Post a Comment