Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu na mkewe Bi.Faraja Nyalandu wakiingia uwanja wa Namfua Mjini Singida kabla ya kuhutubia wananchi kwa kutangaza nia ya kugombea Urais.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya wa Singida, Barnabas Hanje kabla kutangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania kwenye mkutano uliofanyika uwanja wa Namfua Mjini Singida.
Bi. Faraja Nyalandu akiongea na wananchi kabla ya hotuba ya mumewe Mhe. Lazaro Nyalandu ya kutangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania.
Kijiko mali ya manispaa ya Singida kilichonunuliwa kwa shilingi 110 milioni,kikipakia taka ngumu kutoka kwenye dampo la soko la vitunguu mjini hapa jana.
Malori mawili mapya mali ya manispaa ya Singida yaliyotolewa na serikali kuu kwa ajili ya kuzoa taka ngumu. Thamani ya malori hayo ni zaidi ya shilingi milioni 140. Na chini picha ya kijiko hicho .
Serikali kuu imeipatia msaada halmashauri ya manispaa ya Singida, kijiko na malori mawili makubwa vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 250 milioni,kwa ajili ya uzoaji wa taka ngumu.
Hayo yamesemwa juzi na mkurugenzi wa manispaa ya Singida, Joseph Mchina, wakati akizingumza na waandishi wa habari juu msaada huo ambao utasaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha hali ya usafi katika mji wa Singida,na pia zitapunguza gharama kubwa ya uzoaji taka ngumu.
Alisema malori hayo mawili ya tani 20 kila moja, thamani yake ni shilingi 70 milioni kila moja na kijiko ni shilingi 110 milioni.
“Kwa mwezi tulikuwa tunatumia zaidi ya shilingi
Baadhi ya maghuba yaliyopo katika Manispaa ya Singida yakiwa yamefurika taka ngumu kwa muda mrefu sasa kama ambavyo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bwana Joseph Mchina alivyokiri katika maelezo yake kushindwa kuzoa kutokana na magari ya kuzolea taka kuchelewa kufika.
WAKAZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida wameulalakia uongozi wa Manispaa hiyo kwa kushindwa kuzoa taka kwenye maghuba ya kukusanyia taka ngumu zinazokusanywa na wananchi wa mji wa Singida,licha ya wananchi hao kutozwa ushuru wa shilingi elfu tano kwa kila mwezi kwa ajili ya uzoaji wa taka hizo ngumu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao,Abdallah Daudi Kibiriti,Mwandoghwe Gwao na Avi Mohamedi walifafanua kuwa uongozi wa Manispaa hiyo,akiwemo mkurugenzi kwa kushirikiana na madiwani waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia maendeleo kwenye maeneo yao,lakini maslahi zaidi yamewekwa katika kulipana posho za vikao na safari za mara kwa mara za mkurugenzi huyo.
Walifafanua wananchi hao kwamba kutokana na kuwepo kwa hali hiyo,ni wakati wowote ule
Mwanyekiti wa Umoja wa Wanawake watumishi kanisa la Pentekoste (UWW) mjini Singida, Lessi Jared (kushoto) akimkabidhi vifaa tiba Kaimu mganga mfawidhi hospital ya mkoa ya mjini Singida, Dk.Daniel Tarimo.Vifaa tiba hivyo vingi vikiwa kwa matumizi ya chumba cha upasuaji imedaiwa kuwa gharama yake ni mamilioni ya shilingi, vimetolewa na shirika lisilo la kiserikali la waumini wanawake kanisa Pentekoste nchini Denmark-Heart to Heart.
Mganga Kaimu mganga mfawidhi hospitali ya mkoa mjini Singida, Dk.Daniel Tarimo (wa tano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa Umoja wa Wanawake watumishi FPCT Singida mjini na baadhi wa viongozi wa kanisa hilo, muda mfupi baada ya kukabidhi vifaa tiba.
Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Bi Martha Mlata (wa pili kutoka kulia) akimkabidhi pikipiki Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mkalama, Bi Elipendo Machafuko (aliyepanda pikipiki) atakayotumia kuwatembelea wanachama wa jumuiya hiyo. Wengine walioshuhudiwa hafla ya makabidhiano hayo ni pamoja na Katibu wa CCM wilaya ya Mkalama,Bw.Amosi Shimba(wa kwanza kulia),Bi Hadija Kisuda-mwenyekiti wa UWT wilaya ya Singida vijijini(wa tatu kutoka kulia) na katibu wa UWT Mkoa wa Singida,Bi Anjela Robert(wa kwanza kutoka kushoto).
Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Bi Martha Mlata (wa kwanza kulia) akiwakabidhi makatibu wa matawi ya jumuiya ya UWT baiskeli moja kwa kila kata.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida,James John Mkwenga,akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika kijiji cha Nduguti.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Asma Seif na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mkalama,Cusbert Mwinuka.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Edward Ole Lenga, akizungumza mbele ya kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama. Ele Lenga alitumia nafasi hiyo kuagiza madiwani na viongozi kuongeza juhudi kuhamasisha wananchi kuisoma na kuielewa vizuri Katiba iliyopendekezwa.
Mwenyekiti wa Benki ya Posta nchini, Lettice Rutashobya (kulia) akimkabuidhi kadi ya benki Mwenyekiti wa mtaa wa Majengo mjini Singida, Stamili Shomari baada ya kupewa offer na benki hiyo kufungua akaunti.
Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Posta nchini, Sabasaba Moshingi,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la benki ya Posta mjini Singida.