Kamanda wa jeshi la polisi
mkoa wa Singida (wa kwanza kushoto mwenye fimbo) akiangalia daraja
lililobomoka la Munung’una lililopo barabara kuu ya Singida – Mwanza
eneo la kijiji cha Msisi wilaya ya Singida.
Mhandisi wa TANROADS mkoa wa Singida,Yustaki Kangole akiwaelekeza jambo wahandisi wa kampuni ya CHICO iliyojenga daraja lililobomokajuzi la kijiji cha Msisi wilaya ya Singida.Daraja hilo lililopo kwenye barabara kuu ya Singida – Mwanza,limebomoka baada ya kuzidiwa na maji ya mvua kubwa iliyonyesha siku moja kabla ya mwaka mpya.
Baadhi wa wasafiri waliokwama baada ya daraja la Munung’una lililopo katika barabara kuu ya Singida – Mwanza eneo la kijiji cha Msisi wilayani Singida, kubomoka juzi kufuatia mvua kubwa zilizonyesha mkoani Singida.
Mhandisi wa TANROADS mkoa wa Singida,Yustaki Kangole akiwaelekeza jambo wahandisi wa kampuni ya CHICO iliyojenga daraja lililobomokajuzi la kijiji cha Msisi wilaya ya Singida.Daraja hilo lililopo kwenye barabara kuu ya Singida – Mwanza,limebomoka baada ya kuzidiwa na maji ya mvua kubwa iliyonyesha siku moja kabla ya mwaka mpya.
Baadhi wa wasafiri waliokwama baada ya daraja la Munung’una lililopo katika barabara kuu ya Singida – Mwanza eneo la kijiji cha Msisi wilayani Singida, kubomoka juzi kufuatia mvua kubwa zilizonyesha mkoani Singida.
Mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Singida,zimeendelea kuleta maadhara
makubwa ikiwemo kuvunja daraja na barabara kuu ya Singida – Mwanza na
kuua raia moja wa nchini China.
Juzi
mvua hizo zilisababisha familia ya watu wanne
ya wilaya ya Mkalama mkoa
wa Singida, kupoteza maisha baada ya kuangukiwa na nyumba ya tembe.
Mvua
hizo kubwa zilizonyesha kuanzia mwaka mpya (1/1/2013) saa nane mchana
hadi saa 12.30 jioni zilisababisha daraja la Munung’una lililopo katika
kijiji cha Msisi wilayani Singida, barabara kuu itokayo Singida
kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani za Kongo, Burudi, Rwanda
na Uganda, kubomoka na kusabaisha shimo kubwa.
Kubomoka
kwa daraja hilo kumechangia foleni kubwa ya magari yanayokadiriwa kuwa
ni zaidi ya mia tatu. Pia mawasiliano kati ya mikoa mbalimbali ikiwemo
ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani yamekatika.
Mmoja
wa madereva walioathirika na kubomoka kwa daraja hilo, George Medadi,
aliyekuwa akitokea Mwanza akirudi jijini Dar-es-salaam, alisema kubomoka
kwa daraja hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kujengwa chini ya
kiwango.
“Wenyeji
wa hapa wametueleza kuwa kalvati zilizotumika ni zile za zilizowekwa
wakati Nalaila Kiula alipokuwa Waziri wa Ujenzi. Kampuni ya CHICO
iliyojenga barabara hii kwa kiwango cha lami waliyatumia makalivati hayo
hayo na walichofanya ni kulundika udogo juu tu,” Medadi alisema.
Naye
dereva Iddi Mussa alisema kuwa barabara nyingi zinazojengwa na kampuni
za kichina zimekuwa hazisimamiwi ipasavyo kitendo kinachochangia
kuharibika haraka na kuisababishia serikali kuingia hasara kubwa.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi alisema kwa
kuanzia wameimarisha ulinzi katika eneo hilo pamoja na kufungua kituo
kidogo cha kutolea huduma ya afya na kudhibiti uwezekano wa kutokea kwa
magonjwa ya mlipuko.
“Pia
tumefungua barabara ya Singida-Ndago –Misigiri kwa ajili ya kutumiwa na
mabasi ya abiria na yale yenye uzito chini ya tani kumi. Vile vile
tunaangalia uwezekano wa kuangalia ni namna gani watu waliokwama
wanapata chakula,” alisema.
Meneja
wa TANROADS Mkoa wa Singida, Mhandisi Yustaki Kangole, ambaye alifika
na wahandisi wa kampuni ya CHICO, alisema kuwa wamekubaliana na CHICO
kwamba wafukie shimo hilo kwa vifusi vya mawe makubwa ili barabara hiyo
ianze kutumika mapema iwezekanavyo.
“Kwa
sasa tunafanya kazi hii ya muda na baada ya eneo hili kukauka ndio
ukarabati mkubwa utafanywa ili kuimarisha barabara hii muhimu kwa uchumi
wa taifa,” alisema Mhandisi Kangole.
Wakati
huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Edward Ole Lenga amesema kuwa raia
moja wa China amefariki dunia baada ya gari lake kusombwa na maji ya mto
jirani na kijiji cha Gumanga.
Alisema
Mchina huyo ambaye jina lake bado halijatambuliwa hadi sasa, alisombwa
na maji ya mto juzi majira ya jioni wakati akikatisha mto wa kijiji cha
Gumanga wilaya ya Mkalama. Ndani ya gari hilo alikuwa na mtoto wake
ambaye alinusurika kufa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa zaidi atatoa baadae.
No comments:
Post a Comment