Thursday, October 31, 2013

Shule ya msingi Ikungi yazindua ufundishaji kwa njia ya TEHAMA.

Mkuu wa wilaya ya kungi mkoani Singida, Manju Msambya akizindua mitambo ya kufundishia kwa njia ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika shule ya msingi Ikungi mchanganyiko.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi (mwenye skafu) akipewa maelezo na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko, Olivary Kamili,juu ya mitambo ya kufundishia TEHAMA.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Manju Msambya akiangalia screen inayoonyesha namna somo linavyotolewa kupitia TEHAMA.

Shule ya Msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoani Singida imezindua rasmi ufundishaji wa kisasa kupitia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuwawezesha wanafunzi kutumia vifaa mbalimbali katika mawasiliano na kujiendeleza kielimu.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Olivary Kamili amesema mfumo huo wa ufundishaji pia utawawezesha wanafunzi kwenda na wakati katika kujifunza.

Akifafanua amesema mfumo huo utawajengea mazingira mazuri wanafunzi kuwa na tabia ya udadisi ambayo itapelekea wawe wagunduzi.

“Kupitia somo la TEHAMA wanafunzi watajenga tabia ya kujifunza kupitia udadisi wa mambo mbali mbali hivyo itasaidia kupata vijana ambao watakuwa na uwezo wa kufanya tafiti za uhakika”,amesema Mwalimu Kamili.

 Aidha, amesema kutokana na umuhimu wa somo la TEHAMA ameishauri Serikali ilipe kipaumbele kwa kuhakikisha shule zote zinanufaika na somo hilo.

 “Somo la TEHAMA linarahisisha sana upatikanaji wa elimu bora na yenye mafanikio makubwa.Napendekeza serikali iangalie namna ya kuboresha somo hili ili liweze kuwa na
manufaa pia kwa wanafunzi wenye ulemavu wakiwemo wasioona”alifafanua mwalimu huyo.

Akiijengea nguvu hoja yake hiyo Mwalimu Kamili amesema kwa sasa vifaa vinavyotumika katika somo la TEHAMA ni rafiki tu kwa wanafunzi wasio na ulemavu wa kutokuona.

Kamili amesema vifaa vinavyotumika sasa,sio rafiki kabisa kwa wanafunzi viziwi ambao mawasiliano yao ni ya lugha za isahara na wananfunzi wasioona,wanasikia sauti lakini hawaoni matendo yanayotumika kwenye somo la TEHAMA.


Uzinduzi huo ulifanywa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Manju Msambya ambaye alihimiza matumizi ya TEHAMA katika shule zote za wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment