Wednesday, October 7, 2015

DORIS MOLLEL FOUNDATION: Yakabidhi vitabu 200 kwa Shule ya Msingi Midamigha Ilongero SINGIDA.

Mwalimu wa taaluma wa shule Msingi Midamigha Ilongero, Singida akipokea vitabu hivyo kutoka taasisi ya Dmf wakati wa kukabidhi vitabu hivyo.
[SINGIDA] Taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ‘DORIS MOLLEL FOUNDATION’(Dmf)  mwishoni mwa wiki imekabidhi vitabu 200 kwa ajili ya kujifunzia  katika shule ya msingi Midamigha ilongero, singida.

Vitabu hivyo vitakuwa chachu na changamoto kwa wanafunzi wa shule hiyo ambapo watapata furasa za kujifunza mambo mbalimbali katika elimu yao.

Dmf imetoa vitabu hivyo ni kutokana na ufadhili wa taasisi ya Kituruki iitwayo Rhema Trust.

Taasisi ya Dmf  imekuwa mstari wa mbele katika harakati za kutetea watoto hasa watoto njiti wasipoteze maisha kutokana na kukosa vifaa vya kufanya watoto hao waweze kuishi na kufikia malengo kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa na wakiwa njiti.

No comments:

Post a Comment