Mkaguzi wa dawa wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati, Dkt.Engelbert Mbekenga,
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya msako
unaoendelea wa kukamata bidhaa zilizokwisha muda wake wa kutumika na
zile zilizopigwa marufuku kutumiwa. Hivi karibuni mamlaka hiyo
iliteketeza bidhaa zilizoisha muda wake na zile zenye sumu za thamani ya
zaidi ya silingi milioni 7.1 zilizokamatwa wilaya ya Iramba na Singida
vijijini.
Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati, imeteketeza bidhaa mbalimbali
ikiwemo vipodozi vyenye viambato vya sumu, zenye thamani ya zaidi ya Sh.
milioni 7.1.
Bidhaa zingine zilizoteketezwa ni pamoja na vyakula na vinywaji vilivyokwisha muda wake wa kutumika na zile zenye ubora hafifu.
Hayo
yamesemwa na Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Kati Dkt. Englibert Mbekenga,
muda mfupi baada ya
kuteketeza bidhaa hizo katika mji wa Old Kiomboi, wilaya ya Iramba mkoa wa Singida.
Amesema
bidhaa hizo wamezikamata wakati wa ukaguzi ulioanzia wilaya ya Singida
vijijini Machi 4 hadi 10 na katika wilaya ya Iramba, ulioanza Machi 11
na kumalizika 16 mwaka huu.
Amesema
lengo la ukaguzi huo ni kuangalia hali ya majengo, usafi, hali ya
usajili na vibali kutoka mamlaka ya chakula na dawa, pamoja na hali ya
ubora wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.
Kuhusu bidhaa hizo, Dkt. Mbekenga amesema kuwa vipodozi vyenye viambato vya sumu vyenye uzito wa tani 0.16 vimekamatwa kwenye msako huo endelevu, na thamani yake ni zaidi ya Sh.3.2 milioni.
Amesema
pia tani 0.15 za vyakula ambavyo muda wake wa kutumika umeisha,
vimekamatwa na kuviteketeza na thamani yake ni zaidi Sh. laki sita na
vile vile vinywaji vyenye uzito wa lita 701 vimeteketezwa.
Katika
hatua nyingine, Dkt. Mbekenga ametumia fursa hiyo kuwatahadharisha
wananchi kuwa makini wakati wanafanya manunuzi ya bidhaaa mbali mbali.
Amesisitiza
kuwa mwananchi asipokuwa makini, kuna uwezekano mkubwa akanunua sumu
ambayo itaenda kumuuawa taratibu, kwa hiyo ni lazima kuwe na umakini,
soma maelezo ya bidhaa, angalia muda wake wa kutumika na ubora wake.
Mkaguzi
huyo pia amewaonya wafanyabiashara wanaowakimbia wakaguzi wa TFDA, kuwa
arobaini yao ipo karibu, na kuwa dawa pekee ya wafanyabiashara ni kuwa
rafiki wazuri wa TFDA, ni kuwa waadilifuna wanaoheshimu maisha ya watu.
No comments:
Post a Comment