Mkulima John Leonard Njiku
akiwa amelazwa katika wodi namba tatu katika hospitali ya mkoa mjini
Singida baada ya kuvamiwa akiwa shambani na wenzake wawili. Njiku
amedai kuwa uvamizi huo unachangiwa na ugomvi wa kugombe shamba kati
yake na Dk. Damas Simbu aishiye Dar-es-salaam.
Wakulima
watatu wakazi wa kijiji cha Ughaugha (b) manispaa ya Singida,
wamenusurika kuuawa baada ya kuvamiwa na watu wanaokadiriwa kuwa 12
wakiwa shambani na kushambuliwa kwa majembe kwa kile kilichodaiwa kuwa
ni ugomvi wa kugombea shamba.
Wakulima
hao waliovamiwa
Februari nane mwaka huu saa tatu asubuhi wakiwa
shambani ni John Leonard Njiku (41) na mdogo wake Mateo (37), wakati
mkulima mwingine ni Eliasi George (37) na wote hao wamelazwa wodi namba
tatu katika hospitali ya mkoa mjini Singida na hali zao zinaendelea
vizuri.
Uvamizi
huo unadaiwa kuwa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ugomvi wa kugombea
shamba kati ya John na Dk.Damas Simbu, anayefanyia kazi jijini
Dar-es-salaam.
Akizungumza
kwa taabu kubwa akiwa kitandani ,John amesema kuwa siku ya tukio
wakiwa shambani kwake, ghafla walivamiwa na kundi la watu lililokuwa
limebeba hengo na mawe mikono yao yote miwili.
Amesema
yeye inaonekena kuwa alikuwa mlengwa kwani watu hao walimuanza kumkata
kwa hengo kwenye paji lake la uso na kusababisha aanguke chini na
kupoteza fahamu.
Amesema
kuwa watu hao vile vile walimpiga kwa jiwe mdomoni na kusababisha meno
matatu kulegea na kudai kutokana na kulegea sana,huenda yakatolewa.
“Mdogo
wangu Mateo yeye amepigwa na jiwe lenye ncha kali kichwani na ameumizwa
vibaya kwa jembe kwenye mbavu za kulia, wakati jirani na rafiki yetu
George yeye amejeruhiwa vibaya kichwani na sehemu za mbavu zake kwa
kukatwa na jembe na pia kupigwa kwa mawe”,amesema mkulima huyo.
Akifafanua zaidi, John amesema uvamizi huo umechangiwa na ugomvi wa muda mrefu wa kugombea shamaba yeye na Dk.Simbu.
Alisema
yeye na Dk.Simbu wamewahi kifikishana mbele ya baraza la ardhi la
wilaya na pia kwenye mahakama ya wilaya ya Singida na kote huko
alimgaragaza vibaya daktari huyo.
John
amesema kuwa pamoja na vyombo vyote hivyo vya sheria kumpa ushindi
Dk.Simbu hakuweza kuridhika na hivi sasa faili lipo mahakama kuu Dodoma.
No comments:
Post a Comment