Monday, July 21, 2014

Vijiji vya Mgandu, Manyoni kunufaika na Mnara wa mawasiliano wa TTCL.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa.(Picha na Maktaba).

Shirika la TTCL,linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 503 milioni kugharamia ujenzi wa mnara wa mawasiliano katika kata ya Mgandu jimbo la Manyoni magharibi kabla ya oktoba 31 mwaka huu.

Kwa mujibu wa barua ya Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa yenye kumbukumbu no.WMST/GL/DOM.vol.3/01 ya mei 16 mwaka huu,mnara huo utanufaisha vijiji vya Itagata,Kalagali,Kayui,Makale na Mitundu.

Hayo yamesemwa juzi na mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi,John Paulo Lwanji,wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Makale ulioitishwa kwa ajili ya naibu waziri wa maji,Amos Makala,kupokea kero za maji zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Hatua hiyo ya kujengwa kwa mnara huo,ni juhudi za kipekee za

Serikali yapeleka neema ya maji Manyoni, kutumia Bil moja na nusu.


Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makala, akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kijiji cha Makale na Itagata jimbo la Manyoni magharibi.Makala alikuwa jimbo la Manyoni magharabi  kwenye ziara ya kikazi ya siku moja.Kushoto ni mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, John Paulo Lwanji.

Mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, John Paulo Lwanji akizungumza na wananchi wa kijiji cha Itigi kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makala kuzungumza na wananchi.
Mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Manyoni, Eng.Desidedit Magoma.(wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa naibu waziri wa maji Amos Makala (mwenye kaunda suti) juu ya maendeleo ya ujenzi wa bwawa la kijiji cha Itagata.Anayeangalia kamera ni mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi,John Paulo Lwanji.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Itigi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji,Amos Makala wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.Makala aliwaambia wakazi hao kuwa serikali itatenga zaidi ya shilingi 1.5 kwa ajili ya kazi ya usanifu na ujenzi wa miundo mbinu ya maji katika mjini huo mdogo wa Itigi unaotarajiwa kuwa makao makuu ya wilaya ya Itigi.

Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala (Mb), amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Manyoni  mkoa wa Singida na kutangaza neema ya maji baada ya kusema kuwa serikali imetenga zaidi ya shilingi 1.8 bilioni kupunguza kero ya uhaba wa maji wilayani humo.

Makala ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mbwasa jimbo la Manyoni mashariki na kwenye vijiji vya Makale, Itagata na Itigi jimbo la Manyoni magharibi.

Amesema serikalia inatambua tatizo la maji lililopo wilaya ya Manyoni,kupitia wabunge wake ambao wametumia muda mwingi kuihimiza serikali kuondoa kero hiyo ya maji inayowakabili wapiga kura wao na wananchi kwa ujumla.


“Niwahakikishie tu wananchi wa kata ya Mitundu na jimbo la Manyoni magharibi, kwamba mbunge wenu Lwanji kwa muda mrefu ameibana serikali juu ya tatizo la maji linalowakabili. Kwa hiyo, niwatoe hofu, kwa sababu hivi sasa

Msichana wa ndani aua tajiri yake, amchoma kisu kwenye Titi, afa papo hapo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela.

SAKATA la wafanyakazi wa ndani kunyanyaswa na mabosi wao limeingia katika sura ya kipekee safari hii mabosi wamegeukwa na kuuwawa na wafanyakazi hao.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya mfanyakazi mmoja wa ndani Mkoani Singida, kumwua tajiri yake kwa kumchoma kwa kisu sehemu ya juu ya titi la kulia kwa madai ya kunyanyashwa na tajiri yake.

Kamanda wa polisi Mkoani Singida (SACP) Geofrey Kamwela alisema tukio hilo la aina yake limetokea jana eneo la Sabasaba Kata ya Utemini Manispaa ya Singida saa 10. 00 asubuhi baada ya msichana anayesadikiwa kuwa mtumishi wa ndani kumchoma kisu tajiri wake

Kamanda Kamwela alimtaja marehemu kuwa ni Asha Juma (24)  ambaye ni Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida.

“Baada ya marehemu kuchomwa kisu na msichana wake huyo, alifanikiwa kutoka nje ya nyumba na
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela.

WAANDISHI wa habari mkoa wa Singida, wamehimizwa kutumia kalamu zao kuwaelimisha wanawake juu ya haki zao mbalimbali ili kupunguza vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa dhidi yao.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na kiongozi wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Singida Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Eileen Mbwatila wakati akizungumza na waandishi wa habari wanaotathmini utekelezaji wa mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na jinsia (TMEP).
Mradi huo unatekelezwa kwa pamoja na mashirika ya HAPA na YMC ya mjini hapa.

Alisema uzoefu unaonyesha wazi kwamba wanawake wengi mkoani hapa, wanaendelea kukandamizwa kwa kuachiwa kazi zote za nyumbani na wanaume,wananyanyaswa na wanapigwa vibaya kutokana na kutokujua haki zao.

Mbwatila alisema vitendo vingi viovu wanavyofanyiwa wanawake hasa na wanaume wakiwemo waume wao,vimekuwa vikifikishwa kwa ndugu ambao kazi yao ni kutoa

NSSF, Singida yatumia Bilioni 1.52 kukopesha vikundi sita vya wajasiriamali.


Meneja wa shirika na hifadhi ya jamii NSSF, Magreth Mwaipeta akizungumza na wanachama wa kikundi cha Aminika gold Mine Ltd cha Sambaru Wilaya ya Ikungi, Singida.

Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Aminika Francis Mbasha akizungumza kwenye mkutano baina ya wanakikundi na NSSF.  

Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida Magreth akizungumza na wajumbe wa bodi pamoja na wanachama wa kikundi cha Aminika cha Sambaru Wilayani Ikungi.

Wanachama wa chama cha Aminika Gold Mine wakiwa kwenye ukumbi wa ofisi ya madini wakati wa semina ya uhabarisho.

Makamu Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Aminika akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi nje ya ukumbi wa madini Singida mjini.
Wanachama wa chama cha Aminika Gold Mine wakimsikiliza meneja wa NSSF Mkoa wa Singida.

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umetumia zaidi ya shilingi bilioni 1.52 kwa ajili ya kuvikopesha vyama  sita vya ushirika Mkoani Singida.

Hayo yamebainishwa jana mjini hapa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Magreth Mwaipeta wakati akizungumza kwenye semina ya uhabarisho baina ya shirika la kikundi cha wachimbaji wa madini ya dhahabu cha Aminika Gold Mine cha kijiji cha Sambaru Wilayani Ikungi.

Mwaipeta alisema mikopo hiyo imetolewa kwa riba nafuu kwa vikundi hivyo ili waweze kujikwamua kutokana na umaskini iongoni mwao.

Aidha alivitaja vikundi hivyo vilivyopewa mkopo na kiasi cha fedha kwenye mabano kuwa ni kuwa ni Veta Singida (milioni 500), Mtinko (milioni 164), Amani Manyoni (milioni 223), Kumekucha Itigi (milioni 50) ,Tumaini (89) milioni na Ndago cha Wilayani Iramba( milioni 500).

Alisema vikundi hivyo vimepata mikopo hiyo baada ya

Utoaji elimu ya afya ya uzazi na ujinsia wafanikiwa.

Mratiibu msaidizi wa polisi mkoa wa Singida,Irene Mbwatila,(anayeangalia kamera),akizungumza na timu ya pamoja ya maafisa wa shirika la HAPA,YMC na RFSU, inayofanya utafiti juu ya mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia.
Baadhi ya wanaume wakiwa na wake zao wakazi wa kijiji cha Ntuntu wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, wakiwa kwenye foleni katika kliniki ya kijijini hapo,wakisubiri kuingia kumwona muuguzi. Elimu iliyotolewa kwa pamoja na mashirika ya HAPA na YMC,ya umuhimu wa ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na unjisia, katika kipindi cha miaka mitatu, imechangia wanaume pamoja na mambo mengine, kusindikiza wake zao kliniki kutoka asilimia 0 hadi 80 ya sasa.
Muuguzi wa zahanati ya kijiji cha Ntuntu wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Mary Lema, akitoa dawa kwa mama mjamzito Lucia Hongoa, huku mume wake Edward akiwa anashuhudia. Kijiji cha Ntuntu ni moja ya vijiji ambavyo elimu ya ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia,inatolewa.
Muuguzi wa zahanati ya kijiji cha Ntuntu wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Mary Lema akitoa taarifa yake juu ya utekelezaji wa mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

 ELIMU ya ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia inayotolewa kwa pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ya HAPA na YMC imezaa matunda baada ya wanaume kubadilika, na kuanza kusindikiza wake zao klinki na kusaidia kazi zote za nyumbani,imeelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, muuguzi wa kliniki ya zahanati ya kijiji cha Ntuntu wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Mary Lema, amesema kuwa miaka mitatu iliyopita,hakukuwa na mwanaume anayesindikiza mke wake klinki.

Alisema elimu hiyo imewahamasisha na kuwaelimisha wanaume ambao kwa sasa

Manyoni yalipa fidia zaidi ya shilingi 158 milioni kupisha zoezi la huduma ya umeme vijijini.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Manyoni Mseya, akitoa taafira yake ya ulipaji fidia kwa baadhi ya wakazi wa kijiji cha Maweni, Mwanzi na Lusillile ili wapishe mradi wa njia ya umeme 400 KV.

HALMASHAURI ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida, imetumia zaidi ya shilingi 158 milioni kulipa fidia kwa baadhi ya wakazi wa vijiji vitatu,ili kupisha zoezi la utoaji wa huduma ya umeme vijijini.

Fidia hiyo imetolewa mapema mwaka huu kwa wakazi wa vijiji vya Maweni,Mwanzi na Lusilile.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Supeet Roine Mseya wakati akitoa taarifa yake kwa naibu wa nishati na madini Charles Kitwanga (Mb),aliyekuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja wilayani humo.

Amesema fidia hiyo imelipwa kwa

Thursday, July 17, 2014

Wanaume washiriki afya ya uzazi, jinsia kwa kusindikiza wake zao kliniki.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Singida, Joseph Sabore (anayeangalia kamera) akizungumza na maafisa wa shirika lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Association (HAPA), YMC na WaterAid Tanzania, ambao wako katika halmashauri hiyo kufanya tathimini ya mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia. Mradi huo unaotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi 1.6 bilioni, unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu na unatarajiwa kufikia ukingoni Desemba mwaka huu.


MRADI wa ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia (TMEP) unaotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Singida,umeanza kuzaa matunda yanayotarajiwa baada ya asilimia 89 ya wanaume kubadilika na kuanza kusindikiza wake zao kliniki na vituo vya afya.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Muuguzi Mkuu wa Halmashauri hiyo,Bertha Herman wakati akitoa taarifa yake ya ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na ujinsia, kwa maafisa wa shirika lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Association (HAPA),YMC na WaterAid Tanzania,ambao wanafanya tathimini ya mradi huo wa miaka mitatu unaotarajiwa kumalizika desemba mwaka huu.

Amesema katika miaka ya nyuma ambayo ilikuwa imetawaliwa na mfumo kandamizi (mfumo dume),ilikuwa mwiko kwa mwanaume kumsindikiza mke wake kliniki au kumsaidia kazi za nyumbani ikiwemo ya kufua nguo za watoto,kuandaa chakula na kusafisha mazingira ya kaya yao.

Amesema mfumo huo kwa kiasi kikubwa ulipunguza mawasiliano baina ya mke na mume na ulijenga utamaduni wa kuwa mwanaume ana haki ya kumpa kipigo kikali mke pindi anapoona inafaa.

“Baada ya kuanzishwa kwa mradi huu miaka mitatu iliyopita,mambo yanaendelea kubadilika kwa kasi kubwa.Kwa sasa si rahisi kusikia mwanaume

HAPA Singida kutumia mil 485 kuboresha afya vijiji 62.

Meneja wa shirika la HAPA la mkoa wa Singida, David Mkanje akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 7.4 milioni kwa kijiji cha Mlandala kata Urughu wilaya ya Iramba.Vifaa hivyo vimetolewa msaada na shirika la HAPA. Kulia ni mwenyekiti wa kijiji cha Mlandala,Mahona Mahela na kushoto ni kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Iramba, Dk.Antony Mburu.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mlandala kata Urughu wlaya ya Iramba,Mahona Mahela, akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba vya zanahati ya kijiji hicho vilivyotolewa msaada na shirika la HAPA la mjini Singida. Kulia ni meneja wa shirika la HAPA, David Mkanje.
Kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Iramba, Dk.Antony Mburu, akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 7.4 milioni vilivyotolewa msaada na shirika la HAPA.
Meneja wa shirika la HAPA, David Mkanje (kushoto) akimkabidhi kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Iramba, Dk.Antony Mburu,mizani ya kupimia watoto wachanga,ambayo ni sehemu ya msaada tiba wenye thamani ya zaidi ya shilingi 7.4 milioni uliotolewa na HAPA.
Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya makabidhiano wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 7.4 milioni vilivyotolewa msaada kwa kijiji cha Mlandala kata Urughu wilaya ya Iramba.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Association (HAPA) la mkoa wa Singida,linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 485 milioni kugharamia utekelezaji wa mradi wa ‘Pamoja Tunaweza’ katika vijiji 62 vilivyopo kwenye kata 13, za wilaya ya Iramba na wilaya ya Mkalama.

Mradi huo wa miaka mitano ambao unatarajiwa kumalizika mwakani,lengo lake ni kuinua hali za afya za uzazi kwa akina mama na watoto.

Meneja wa shirika la HAPA, David Mkanje, alisema hayo wakati akizungumza kwenye hafla iliyofana ya makabidhiano ya vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 7.4 milioni vilivyotolewa na shirika hilo la HAPA,kwa kijiji cha Mlandala kata ya Urughu wilaya ya Iramba.

Alisema fedha hizo zilizotolewa na shirika la nchini Uholanzi la SIMAVI, zinatumika katika

Waziri wa Maliasili na Utaliii, Nyalandu aipiga jeki ofisi ya Qadhi mkoa wa Singida.

Waziri wa Maliasili na Utaliii, Nyalandu aipiga jeki ofisi ya Qadhi mkoa wa Singida.
Msaidizi wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Helen Mtalemwa akimkabidhimsaada wa shilingi 10 milioni  Katibu wa mahakama ya Qadhi mkoa wa Singida, Alhaj Burhan Mlau kwa ajili ya kupunguza makali ya uendeshaji wa mahakama hiyo mjini Singida.

Kampeni ya ushawishi CHF yaanza Mkoani Singida.

Timu ya wataalamu kutoka NHIF mkoa wa Singida na ofisi ya DMO wilayani Singida, wakiendesha zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi wa kata ya Msange wilayani Singida.
Afisa matekelezo na uratibu NHIF mkoa wa Singida, Isaya Shekifu (mwenye shati jeupe) akiendesha zoezi la upomaji wakazi wa kijiji cha Msange wilaya ya Singida vijijini.
Meneja wa NHIF mkoa wa Singida,Agnes Chaki, akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwa wananchi wa kata ya Ikhanonda .Kulia ni diwani wa kata ya Ikhanoda, Higa Mnyawi.

MFUKO  wa taifa  wa bima ya afya (NHIF)Mkoa wa Singida, umeanzisha kampeni ya utoaji elimu juu ya umuhimu wa kujiunga  na mfuko huo, na ule wa afya ya jamii (CHF),ili wananchi waweze kujijengea mazingira  ya kupata matibabu hata wakati hana fedha.

Katika kampeni hiyo wananchi watapata nafasi ya kupima afya.

Meneja wa NHIF mkoa wa Singida,Agness Chaki, akizungumza na waandishi wa habari alisema shughuli za upimaji wa afya ya msingi kwa wananchi wote zinafanyika kwa lengo la kuwafanya wananchi kuwa na hamasa ya kujua.


“Upo umuhimu mkubwa kujua hali ya afya yako mapema, badala ya

SEMA Singida wapongezwa kwa kuelimisha tabia nchi.

Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vifaa vya kuongeza uwajibikaji katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi wilayani humo.Kulia ni meneja wa shirika la SEMA, Ivo Manyaku.Kushoto ni mwenyekiti wa kijiji cha Kinyagigi.
Meneja wa shirika lisilo la kiserikali la SEMA,Ivo Manyanku, akitoa taarifa yake kwenye hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vifaa vya kuongeza uwajibikaji katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi wilaya ya Singida.Vifaa hivyo ni pamoja na vipeperushi,vikaragozi na mabango yenye gharama ya zaidi ya shilingi 22 milioni. Kushoto aliyekaa ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kunyagigi wilaya ya Singida,waliohudhuria uzinguzi wa ugawaji wa vifaa vya kuongeza uwajibikaji katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Baadhi ya wanakikundi cha uhamasishaji cha Youth Culture Group cha mjini Singida, wakitoa burudani kwenye ufunguzi wa ugawaji wa vifaa vya kuongeza uwajibikaji katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika kwenye kijiji cha Kinyagigi.
Kikaragosi kimojawapo ambavyo

Watu wanne wafariki dunia katika matukio tofauti Mkoani Singida.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela.

WATU Wanne mkoani Singida wamefariki dunia katika matukio tofauti,likiwemo la wanandoa wawili kuuawa na kisha nyumba yao kuchomwa moto na wao kuteketea pamoja na mali zao.

Wanandoa hao ni Ramadhani Lyanga (80) na mke wake Aziza Ally (60) wakazi wa kitongoji cha Kizega kijiji cha New Kiomboi tarafa ya Kisiriri wilaya ya Iramba.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo la kusikitisha,limetokea Juni 10 mwaka huu saa 7.15 usiku huko katika kitongoji cha Kizega.

Amesema mtu huyo alivunja mlango wa nyumba ya vikongwe hao kwa kutumia kitu kizito kinachodhaniwa kuwa ni jiwe aina ya Fatuma na alipoingia ndani moja kwa moja alienda chumba walichokuwa wamelala wajukuu wao watatu wa vikongwe hao na kuwatisha.

“Baada ya kuwatisha wajukuu hao mtu huyo alihamia chumba walikolala wanandoa hao na kuanza kuwacharaza fimbo hadi walipofariki dunia.Baada ya kufariki dunia,alimwaga petrol chumba kizima cha wazee hao na kisha kuwasha moto kwa kutumia njiti ya kiberiti”,amesema Kamwela.

Kamanda huyo,amesema wajukuu wa wazee huyo

PICHA 10 ZA YALIYOJIRI KWENYE SHINDANO LA MISS SINGIDA 2014

Huyu ndiye Miss Singida 2014 Doris Mole (23) akiwa na mshindi wa pili Blath Chambo na mshindi wa tatu Lulu Abdul.
Mgeni rasmi mama balozi Seif Idd akimkabidhi fedha kiasi cha shilingi laki tano Miss Singida.
 Warembo waliofanikiwa kuingia tano bora ya Miss Singida 2014.