Monday, July 21, 2014

Msichana wa ndani aua tajiri yake, amchoma kisu kwenye Titi, afa papo hapo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela.

SAKATA la wafanyakazi wa ndani kunyanyaswa na mabosi wao limeingia katika sura ya kipekee safari hii mabosi wamegeukwa na kuuwawa na wafanyakazi hao.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya mfanyakazi mmoja wa ndani Mkoani Singida, kumwua tajiri yake kwa kumchoma kwa kisu sehemu ya juu ya titi la kulia kwa madai ya kunyanyashwa na tajiri yake.

Kamanda wa polisi Mkoani Singida (SACP) Geofrey Kamwela alisema tukio hilo la aina yake limetokea jana eneo la Sabasaba Kata ya Utemini Manispaa ya Singida saa 10. 00 asubuhi baada ya msichana anayesadikiwa kuwa mtumishi wa ndani kumchoma kisu tajiri wake

Kamanda Kamwela alimtaja marehemu kuwa ni Asha Juma (24)  ambaye ni Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida.

“Baada ya marehemu kuchomwa kisu na msichana wake huyo, alifanikiwa kutoka nje ya nyumba na
kukimbilia kwa majirani kwa ajili ya kuomba msaada, lakini wakati majirani wakiwa katika harakati za kumpeleka hospitali, alianguka chini na kufa papo hapo.”Alisema Kamanda Kamwela

Hata hivyo alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Valetina Kerenge (17) mwenyeji wa Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza , na alikimbia mara baada ua tukio hilo.

Alisema baada ya polisi kuendesha msako kwa kushirikiana na raia wema hatimaye walifanikiwa kumkamata msichana huyo majira ya saa 8:00 mchana huko maeneo ya uwanja wa ndege akiwa katika harakati za kutoroka.

Kamwela alisema mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa madaktari na babada ya zoezi hilo kukamilika utakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Aidha alisema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi zaidi unaendelea ili kujua chanzo cha mauaji hayo ambapo mtuhumiwa atafikshwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment