Wednesday, November 28, 2012

SHARO MILLIONEA ALIIBIWA HADI NGUO ALIZOKUA KAVAA

 Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu,wanaseme ndugu yao Sharo millionea walimkuta na nguo za ndani tuu,yaani
boxer na vest na kwamba vitu vyote alivyokua navyo kama simu,wallet,pesa alizokua akimpelekea mama yake,mizigo yake n.k vyote viliibiwa na hakuna kitu walichomkuta nacho zaidi ya boxer na vest alizokua amevaa.

Tabia ya kuwaibia wahanga wa ajali hasa za magari imekua ikiongezeka siku hadi siku nchini Tanzania,badala ya kuwasaidia wahanga wa ajili asilimia kubwa ya watu hua wanawaibia kwanza kisha ndo wawape msaada.
Hii sio tabia nzuri hata kidogo na yeyete unaejua umechukua vitu vya Sharo Millionea ni bora uvirudishe kwa ndugu zake.

Sharo Millionea anategemewa kuzikwa leo Jumanne majira ya saa saba mchana kijijini kwao.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa,jina lake lihimidiwe,
Amen.

1 comment:

  1. AnonymousMay 04, 2013

    This is the perfect blog for anybody who would like to understand this topic.
    You know a whole lot its almost hard to argue with you (not
    that I really would want to…HaHa). You definitely put a brand new spin
    on a subject that's been discussed for years. Wonderful stuff, just great!

    Here is my site ハミルトン 時計

    ReplyDelete