Tuesday, November 11, 2014

Rais aagiza kufunguliwa kwa mgodi wa dhahabu wa Mattany Ikungi.

Rais wa Shirikisho la wachimba madini Tanzania, John Bina, akizungumza na wachimbaji madini wa machimbo ya dhahabu kijiji cha Mhintiri tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi .Rais Bina pamoja na mambo mengine, aliagiza kufunguliwa kwa mgodi wa dhahabu unaomilikiwa na Mattany Khalifa uliofungwa baada ya kuvamiwa na wachimbaji wadogo.
Mmiliki wa Mattany Gold mine, Mattany Khalifa, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa maalum kwa ajili ya kufunguliwa kwa mgodi wake uliofungwa baada ya kuvamiwa na wachimbaji wadogo.Mwenye kofia ya pama ni Rais wa shirikisho la wachimbaji madini Tanzania, John Bina.

Milioni 16/- zatolewa na CIP Trust ujenzi wa madarasa.


Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi, (mwenye mgorore wa bluu) akishiriki kutoa burudani na kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Kinyamwenda kwenye sherehe ya kukabidhi vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu wa shule ya kijiji hicho.

Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,akiwa amevikwa nguo na kukabidhiwa zana za ushujaa na wananchi wa kijiji cha Kinyamwenda,kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mchapa kazi wa kupigiwa mfano katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Watoto zaidi ya 66,442 mkoani Singida kupatiwa chanjo mpya ya Malaria na Rubella.

Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi, akizindua zoezi la chanjo mpya ya Malaria na Rubella kwa manispaa ya Singida.Uzinduzi huo umefanyika kwenye kituo cha afya cha Sokoine mjini Singida. Pamoja na chanjo ya Malaria na Rubella, pia dawa za minyoo na mabusha zilitolewa.
Meya wa manispaa ya Singida Sheikh Salum Mahami, akizungumza kwenye zoezi la uzinduzi wa chanjo ya Malaria na Rubella  kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo cha afya Sokoine mjini Singida.Wa pili kulia (waliokaa) ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi na anayefuata ni kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Singida.

TUNAJALI wawajali wanawake na vifaa tiba vya mil 155/-

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la TUNAJALI, Dk.Gottlieb Mpangile (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya kuzindua mpango wa kutokomeza vifo vya wajawazito na watoto wachanga mkoani Singida, Pia hafla hiyo ilitumika kutoa msaada wa vifaa tiba vikiwemo vitanda vya kujifungulia vyote kwa pamoja  vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 155 milioni.Wa pili kushoto (waliokaa) ni mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone na wa kwanza ni katibu tawala mkoani Singida, Liana Hassan.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye hafla ya kuzindua mradi wa kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kukabidhiwa vifaa tiba na shirika la TUNAJALI. Wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan na Kulia ni Mkurugenzi wa shirika la TUNAJALI, Dk. Gottlieb Mpangile.

Wanafunzi waaswa kutokufaulu kidato cha nne, sio kufeli maisha.

Rais wa shirikisho la wachimba madini Tanzania na mgeni rasmi wa mahafali ya sita ya shule ya sekondari kata Mandewa,John Bina,akizungumza kwenye mahafali hayo. Kulia ni mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari ya Mandewa.Bahati Shagama na kushoto ni mkuu wa  wa shule hiyo, Margreth Missanga.
Mkuu wa shule ya sekondari kata ya Mandewa manispaa ya Singida, Margreth Missanga, akitoa taarifa yake kwenye mahafali ya sita ya wahitimu wa kidato cha nne yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo. Kulia ni rais wa shirikisho la wachimba madini Tanzania (mgeni rasmi) John Bina, na Kushoto mwalimu wa shule hiyo.
Rais wa shirikisho la wachimba madini Tanzania, John Bina akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari kata ya Mandewa mjini Singida,wakati wa mahafali ya sita.

Thursday, November 6, 2014

Kikongwe apigwa risasi na polisi na kufariki dunia.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela.

KIKONGWE mmoja mkazi wa kitongoji cha Ilolo kata ya Iglansoni tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi, Joyce Maragabu (65),amefariki dunia baada ya kupigwa kwa risasi na askari polisi waliokuwa wakijihami dhidi ya kundi kubwa la wananchi waliokuwa wakitaka kuwavamia,ili wasiweze kumkamata mhalifu.

Askari hao walikuwa wakitaka kumkamata Nkida Gwisu, aliyekuwa akituhumiwa kumshambulia mtu mwingine.

Kikongwe huyo alipigwa risasi kichwani wakati akiwa anaendelea

RC Singida akataza warsha kuendeshwa kwa kiingereza.

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye ufunguaji wa warsha ya wadau kujadili rasimu ya mwisho ya taarifa ya mpango wa usimamizi na uendelezaji wa pamoja wa rasilimali za maji wa bodi ya maji ya bonde la kati, liyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aquar Vitae hotel mjini Singida.
Baadhi ya wadau waliohudhuria warsha ya wadau kujadili rasimu ya mwisho ya taarifa ya mpango wa usimamizi na uendelezaji wa pamoja wa rasilimali za maji wa bodi ya maji ya bonde la kati,iliyofanyika mjini Singida.