Thursday, November 6, 2014

Viongozi wa dini, wanasiasa waombwa kusaidia kufanikisha chanjo ya Surua na Rubella.

Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi, akifungua kikao cha uhabarisho wa chanjo mpya ya Surua na Rubella wilayani humo. Dc Mlozi pamoja na mambo mengine, ameagiza viongozi wa madhehebu ya dini na wale wa kisiasa, kushiriki kikamilifu zoezi hilo la kitaifa linalotarajiwa kuanza Okt. 18 hadi 24 mwaka huu. Jumla ya watoto 103,879 wilayani humo, wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Singida, Mwendahasara Maganga.
Mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Singida, Emmanuel  Mawi, akitoa mada yake ya uhabarisho juu ya chanjo mpya ya Surua na Rubella inayotarajiwa kuanza kutolewa kuanzia Okt. 18 hadi 24 mwaka huu nchini kote.

Maafisa Mipango washirikishe makundi maalum upangaji bajeti – DED Ikungi.

Mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi, Mwl. Olivary Kamilly, akitoa taarifa yake kwenye kilele cha mahafali ya 63 yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo kongwe iliyoanzishwa mwaka 1944.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Celestine Yunde, akizungumza kwenye mahafali ya 63 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 63 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko, Celestine Yunde, akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa darasa la saba (mwenye ulemavu wa macho).

SUA kutumia shilingi milioni 65 kushawishi matumizi ya Mtama.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha kilimo Sokoine, Profesa Joseph Phillip Hella, akitoa mada yake ya uongezaji wa uzalishaji wa Mtama katika wilaya tisa zinazokabiliwa na ukame hapa nchini.
Afisa kilimo umwangiliaji na ushirika wilaya ya Singida, Abel Mngale, akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya uhabarisho juu ya kuongeza uzalishaji wa zao la Mtama kwenye wilaya tisa zinazokabiliwa na ukame nchini.Kulia ni mhadhiri wa chuo kikuu kilimo cha Sokoine mjini Morogoro, Profesa Joseph Philip Hella na kushoto ni mhadhiri chuo kikuu kilimo Sokoine, Dk.Mafuru.

Wito watolewa wazazi kuwajengea maadili mema watoto.

Diwani wa kata ya Issuna  wilaya ya Ikungi,Stephano Misai,akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya darasa la saba  shule ya msingi Unyahati iliyopo kijiji cha Muungano .Mgeni rasmi huyo amezitaka shule za msingi na sekondari zenye bahati ya kuwa karibu na huduma ya umeme, kuweka nishati hiyo kwa ajili ya wanafunzi kujifunza kompyuta. Wa kwanza kushoto (aliyekaa) ni Chiku Alli raia wa Norway aliyekusanya fedha kutoka kwa raia wa Norway na kugharamia ujenzi wa shule ya Unyahati. Kulia ni mwenyekiti wa kamati ya shule, Alli.
Diwani mstaafu wa nchini Norway Chiku Alli (mzaliwa wa Singida), akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya shule ya msingi Unyahati wilaya ya Ikungi.Chiku amefadhili ujenzi wa shule hiyo baada ya kuchangisha raia wa nchini Norway na ameahidi ndoto ya kijiji hicho kuwa na shule ya sekondari, atahakikisha inatimia.
Mama mzazi wa Chiku, Mwagili Saidi Gwau, akizungumza kwenye hafla ya mahafali ya kwanza ya shule ya msingi Unyahati kijiji cha Muungano.Mama Mwagili amesema yeye ndiye aliyemshauri mtoto wake kujenga shule ya msingi, ili kuwaondolea adha wanafunzi kutembea umbali wa kilometa nne kwenda na kurudi shuleni Ikungi.

Sunday, October 19, 2014

Taarifa fupi ya mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za serikali mkoani Singida kipindi cha 2005 – 2014.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone.
 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
 Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.

Lissu akerwa na uongozi wa Chadema Singida kwa kumdodesha.

Mwenyekiti CHADEMA jimbo la kanda ya kati, Tundu Lissu, akihutubia wana CHADEMA na baadhi ya wakazi wa manispaa ya Singida kwenye viwanja vya Peoples mjini Singida.Tundu pamoja na mambo mengine, amewahimiza wananchi kuikataa rasimu ya katiba mpya kwa madai kwamba imechakachuliwa.

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Singida,wakimsikiliza mwenyekiti CHADEMA jimbo la kanda ya kati na mbunge wa jimbo la Singida mashariki, Tundu Lissu, wakati akiwahutubia.

IDADI  ndogo ya wanachama na wasio wanachama wa CHADEMA waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya mwenyekiti wa jimbo la kanda ya kati, Tundu Lissu, kuzungumza nao, ilimuudhi mgeni huyo rasmi na kutangaza kwamba viongozi wa CHADEMA Manispaa ya Singida, hawana sifa ya uongozi.

Tundu akionyesha kukerwa mno na mahudhurio hayo, alisema wananchi wa mji wa Singida kwa kipindi cha miaka sita, hawajapata viongozi wanaowastahiki.

“Haya maneno yaliyosemwa na viongozi wa CHADEMA manispaa ya Singida, kwamba wananachi wa mji huu, ni waoga kuhudhuria mikutano ya CHADEMA, ni

Matere wabamiza timu inayokusanya michango ya maabara.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SACP,Geofrey Kamwela.

TIMU ya ukusanyaji michango kwa ajili ya ujenzi wa maabara kata ya Mwangeza wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida,imeshambuliwa na kujeruhiwa vibaya na baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Matere kijiji cha Dominiki.

Timu hiyo iliyokuwa inaongozwa na afisa mtendaji kata ya Mwangeza,Halfa Mrisho,imekubana na dhahama hiyo ikiwa kazini, oktoba mosi mwaka huu majira ya mchana huko katika kitongoji cha Matere kijiji cha Dominiki.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mwandishi wa Singida Blog, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama, James Mkwega, ametaja wengine waliojeruhiwa kuwa ni Mtendaji wa kijiji cha Dominiki, Juma Saidi, Afisa mifugo Joseph Doto, Mratibu elimu kata Saidi Nyika na Askari mgambo, Koyo Maduhu.

Alisema watendaji hao baada ya kujeruhiwa vibaya kwa silaha za jadi, walikimbizwa katika hospitali ya misheni ya Hydomu mkoa wa Manyara ambako wanaendelea na matibabu.

Akifafanua, alisema siku ya tukio watendaji hao wakiwa kazini kukusanya michango ya maabara, walivamiwa na watu ambao kuna kila dalili kwamba