Friday, January 2, 2015

Singida watumia Bil 1.5/- kutengeneza madaraja.

Kaimu meneja TANROADS mkoa wa Singida, Eng.Leonard Kapongo, akitoa ufafanuzi juu ya matengenezo ya barabara za ngazi ya mkoa, kwenye kikao cha 37 cha bodi ya barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Social Training Centre mjini Singida.

WAKALA wa barabara (TANROADS) mkoani Singida, umetumia zaidi ya shilingi 1.5 biloni kugharamia matengenezo makubwa na madogo ya madaraja ya barabara kuu na za mkoa kwa kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu.

Hayo yamesemwa na kaimu  meneja TANROADS mkoa wa Singida,Eng.Leonard Kapongo, wakati akizungumza na mwandishi wa SingidaYetuBlog  juu ya utekelezaji wa kazi za barabara kwa kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu.

Alisema madaraja makubwa ya Mnung’una na Malendi yaliyopo barabara kuu,yalifanyiwa matengenezo makubwa yaliyogharimu zaidi ya shilingi 343.2 milioni.

Aidha,kaimu meneja huyo,alisema jumla ya madaraja
23 yalifanyiwa matengenezo ya kinga katika barabara kuu za lami kwa gharama ya zaidi ya shilingi 89 milioni.

Kuhusu barabara za mkoa ,Eng.Kapongo alisema kuwa madaraja makubwa 10,yamefanyiwa matengenezo makubwa katika barabara tisa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni moja.

“Barabara hizo za mkoa ni ya Kidarafa-Nkungi ambayo madaraja yake mawili yalihusika.Zingine za daraja moja moja,ni ya Kizaga-Mgungira,Ulemo-Sibiti, Iguguno Shamba-Gumanga, Ilongero-Nduguti, Soweto-Kiombi-Chemchem, Iyumbu-Magareza (Singida mjni), Kinyamshindo-Kititimo na Njuki-Ilongero-Ngamu”alifafanua kaimu meneja huyo.

Eng.Kapongo alisema pia jumla ya madaraja madogo 14 katika barabara za mkoaa,yalipata matengenezo madogo madogo kwa gharama ya zaidi ya shilingi 53 milioni.


TANROADS mkoa wa Singida, inahudumia jumla ya kilometa 1,689.5 za barabara kuu na barabara za mkoa.Kati ya hizo,kilometa 456.13 ni za lamisawa na aslimia 27 ya barabara zote.Sehemu iliyobaki yenye kilometa 1,236.52 sawa na asilimia 73.2,ni barabara za changarawe.

No comments:

Post a Comment