Sunday, March 16, 2014

Wanawake washauriwa kuanzisha ufugaji wa Kuku wa kienyeji.

Mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida.Fatma Hassan Toufiq, akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya siku tatu inayohudhuriwa na viongozi wa UWT wilaya ya Manyoni.Pamoja na mambo mengine, mada ya ujasiriamali itatolewa.Wa kwanza kushoto ni katibu wa UWT wilaya ya Manyoni, Defroza Lucas na kulia ni mwenyekiti wa UWT, Mwanaidi Issa.

Baadhi ya viongozi wa UWT wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida,wakaifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM wilaya ya Manyoni.Mada zinazotolewa kwenye semina hiyo ni pamoja na Ujasiriamali,Ukimwi na uendeshaji wa jumuiya hiyo ya CCM.

MKUU wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida, Fatma Hassan Toufiq amewaagiza wanawake wilayani humo, kuanzisha ufugaji wa kibiashara wa kuku wa kienyeji, ili waweze kuharakisha kujikomboa kiuchumi.

 Mkuu huyo wa wilaya, ametoa changamoto hiyo hivi karibuni wakati akifungua semina ya siku tatu inayohudhuriwa na vingozi wa jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Manyoni.

Amesema kuwa uzoefu unaonyesha wazi kwamba wanawake wengi hawana mali inayokubalika na taasiis za kifedha yakiwemo mabenki, kuweka dhamana ili waweze kupata mkopo.

Toufiq amesema kutokana na ukweli huo, njia rahisi kwa wanawake kujikomboa kiuchumi, ni kuanzisha ufugaji wa kibiashara wa kuku wa kienyeji pamoja na kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa.

“Kuku wa kienyeji wa mkoa wa Singia wakiwemo na wa wilaya ya Manyoni, wanapendwa sana hapa nchini. Soko lake ni kubwa kila mahali ikiwemo miji mikubwa kama Dar es salaam na Arusha.  Tukianzisha ufugaji bora wa kuku wa kienyeji, nina hakika familia husika zitaondokana na umaskini na hivyo kuishi maisha bora.wilaya”,alifafanua Dc huyo.

Aidha, mkuu huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wanawake kuwa gonjwa hatari la

Wanawake wahimizwa kuwakumbuka wenzao walioko magerezani.

 Mtoto Njiti akiwa amebebwa na mama yake.
WANAWAKE Mkoani Singida wamehimizwa kujenga tabia ya kuwakumbuka wanawake wenzao waliofungwa na walioko mahabusu gerezani ili waendelee kuaminiwa kuwa bado ni sehemu muhimu ya wanawake mkoani humu.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake kanisa la Free Pentekoste church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida mjini, Lessi Jaredi muda mfupi baada ya kutoa msaada wa vitu mbali mbali kwa wanawake wanatumikia adhabu jela na wale walioko mahabusu katika gereza la wilaya ya Singida.Msaada huo ulikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wananwake duniani.

Amesema wanawake waliopo magerezani, hawajapoteza utu wao na wala sio kwamba hawana msaada tena katika kuchangia maendeleo ya mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya watoto waliozaliwa kabla ya kufikia umri wa kuzaliwa (Njiti) ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida.

“Wanawake hawa ni wenzetu, ndugu zetu na watoto wetu, wapo gerezani kwa lengo la kusaidiwa kurekebisha baadhi ya mienendo na tabia zao tu.  Kwa hali hiyo, tunapaswa kuwapenda,kuwathamin na kuwajali, ili kuondoa uwezekano wao wasianze kuhisi kwamba, wametengwa au sio sehemu muhimu ya jamii”,alifafanua Mwenyekiti huyo.

Akisisitiza zaidi, Lessi amesema wanawake hao waliopo gerezani wakitembelewa na hasa na wanaweke wenzao na kukpewa misaada, kitendo hicho kitawatia moyo na kamwe hawatakata tamaa katika maisha yao.

“Nitumie fursa hii kuwahimiza wanawake wa jimbo la Singid mjini na wa mkoa wetu wa Singida kwa ujumla, tujenge utamaduni wa kuadhmisha siku ya wanawake duniani, kwa kuwatembelea wanawake wenzetu walioko magerezani, haspitali na wenye matatizo mbali mbali, ili makundi hayo yaweze kutembua kwamba tunayajali na kuyathamini”,amesema.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo pia amewahimiza wanawake kuwatembelea wanawake walioko katika hospitali mbali mbali baada ya kujifungua watoto na hasa wale ambao watoto wao hawakufikisha umri wa kuzaliwa (njiti).

Saturday, March 15, 2014

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza afa maji.

Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Ipembe mjini Singida Rashid Said (16) (kushoto) na wa kijana ambaye hajafahamika jina aliyekuwa anajaribu kumwokoa mwanafunzi.Vijana hao wawili waliofariki dunia Machi 08 mwaka huu saa nane mchana ,mwanafunzi huyo amefariki dunia baada ya Mtumbwi waliokuwa wameupanda kupigwa na upepo na wao kutumbukia ndani ya maji.
Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Ipembe Rashid Said, ukiingizwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida.

MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Ipembe mjini hapa,Rashid Saidi (16) amefariki dunia baada ya mtumbwi aliokuwa umeupanda ziwani, yeye na baadhi ya wanafunzi wenzake kupigwa na upepo mkali na kusababisha mtumbwi kupinduka na wao kutumbukia kwenye maji.

Kijana mmoja ambaye sio mwanafunzi na jina lake bado halijapatikana,alijitolea kumwokoa mwanafunzi huyo,lakini naye kwa bahati mbaya alifariki dunia baada ya kunywa maji mengi na kuzama ziwani.

Inadaiwa kuwa wanafunzi hao baada ya kumaliza kipindi cha’tuition’ shuleni kwao,kama kawaida yao walienda ‘pikiniki’ katika ziwa la Kindai na kuanza kuogelea pembeni mwa ziwa hilo.

Askari kutoka kikosi cha zima moto mjini hapa,Bahati Hemed,amesema kwa mujibu wa taarifa alizopewa na mashuhuda wa tukio hilo,ni kwamba baada ya wanafunzi hao kumwagwa ndani ya maji,baadhi ya wanafunzi

Mahakama yavunjwa rasmi ndoa ya mfanyabiashara.

Jengo la mahakama ya mwanzo Utemini jimbo la Singida mjini.

MAHAKAMA ya mwanzo Utemini Mjini mjini hapa,  imeamuru kuvunjwa rasmi kwa ndoa na kutoa talaka dhidi ya mfanyabiashara Baltazar Mushi, maarufu kwa jina la Sammayuni (34) na mkewe Lucy Msuya (32), ili kuepusha udhalilishaji dhidi ya Mwanamke huyo.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Ferdnand Njau, ambaye pia mahakama hiyo iligawanya mali sawa, ili wanadoa hao kila mmoja anufaike na jasho lake katika ndoa hiyo iliyodumu kwa miaka sita na kujaliwa kupata watoto wawili.

Aidha makahama hiyo ilimwamuru mwanaume kuhakikisha kila mwezi anawasilisha mahakamani hapo Sh.100,000 kwa mtalaka wake, kwa ajili ya matunzo ya watoto wao wadogo wawili.

Pamoja na utetezi wa mfanyabiashara huyo kuwa anadaiwa deni kubwa linalofikia zaidi ya Sh. Milioni

Wednesday, March 12, 2014

Jela miaka 10 kwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wakati wa kutoa mimba.

Aliyekuwa tabibu msaidizi wa Dispensari ya Tumaini mjini Singida, (wa mbele) Godlisten Raymond (37) na mfanyabiashara wa mbuzi na biashara ya kusaga nafaka (wa tatu mbele) Adamu Shaban Hole (46) mkazi wa kijiji cha Kitandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi,wakisindikizwa na askari polisi kwenda gerezani kuanza kutumikia adhabu ya kila mmoja kifungo cha miaka 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumtoa mimba mwanafunzi na kusababisha kifo chake.
Mfanyabiashara wa Mbuzi na kusaga nafaka katika kijiji cha Kintandaa Adamu Shaban Hole (46) (mbele mwenye kofia baraghashia) na aliyekuwa tabibu msaidizi katika dispensari ya Tumaini mjini Singida, Godlisten Raymond (37) aliyefunika uso,wakisindikizwa gerezani kwenda kuanza kutumikia kifungo cha miaka 10 baada ya kutiwa hatiani na mahakama kuu kanda ya kati kwa kosa la kumpa mimba mwanafunzi na kuitoa na kusababisha kifo chake.Mwanafunzi huyo Hamida Athumani (16) alifariki dunia siku chache kabla ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.

MAHAKAMA Kuu kanda ya kati iliyomaliza vikao vyake hivi karibuni mjini Singida,imewahukumu aliyekuwa tabibu msaidizi wa dispensari ya Tumaini Godlisten Raymond (37) adhabu ya kutumikia jela miaka 10 baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kutoa mimba kwa njia isiyo sahihi kwa  mwanafunzi na kusababisha kifo chake.

Mshitakiwa Godlisten anadaiwa kumtoa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi Kintandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi, Hamida Athumani (16) septemba saba mwaka 2006 na alifariki dunia septemba 17 mwaka huo huo wa 2006, siku chache kabla ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.

Pia katika kesi hiyo,mfanyabiashara wa mbuzi na kusaga nafaka mkazi wa kijiji cha Kitandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi,Adamu Shabani Hole (46),naye amepewa adhabu ya kutumikia jela miaka 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi Hamida Athumani (16) na kisha kushiriki kutoa mimba hiyo na kusababishia kifo mwanafunzi huyo.

Ilidaiwa mahakamanai hapo kuwa mshitakiwa wa pili ambaye ni mfanyabiashara ya mbuzi,Adamu,katika kipindi hicho hicho,aliweza kumpa mwanafunzi mwingine Rukia Juma aliyekuwa akisoma darasa moja na Hamida (marehemu).

Rukia baada ya kutolewa mimba na washitakiwa,aliweza kulazwa katika hospitali ya mkoa mjini hapa,na aliweza kunusurika kufariki dunia baada ya kupatiwa matibabu.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo,mwendesha mashitaka wakili wa serikali mkuu mfawidhi kanda ya Singida,Neema Mwanda,aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali ya kifungo cha

Halmashauri ya Singida kutumia zaidi ya shilingi 350 milioni kujenga machinjio.

Mkurugenzi wa manispaa ya Singida, Joseph Mchina akitoa taarifa yake ya utekelezaji mbele ya kikao maalum cha baraza la madiwani. Wa pili kulia ni Mustahiki meya wa manispaa ya Singida na Sheikh wa mkoa wa Singida,Salum Mahami.Wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida, Hamisi Nguli na anayefuatia ni makamu meya manispaa ya Singida, Hassan Shabani Mkata.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida inatarajia kutumia zaidi ya shilingi 350 milioni, kwa kujenga machinjio ya kisasa katika eneo la Ng’aida kijiji cha Kisaki.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Joseph Mchina wakati akitoa taarifa yake ya ujenzi huo mbele ya kikao cha baraza la madiwani.

Amesema eneo hilo lililoridhiwa kwa ujenzi huo na serikali ya kijiji cha Kisaki,lina ukubwa wa ekari 6.72,na jumla ya zaidi ya shilingi 11.2 milioni, zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi watakaohamishwa kupisha ujenzi huo.

Akifafanua,Mchina amesema manispaa imeibua maradi huo ikiwa ni kutekeleza mkakati wa kuboresha mazao yatokanayo na mifugo hususani nyama na ngozi.

Aidha,, Mkurugenzi huyo amesema kuwa machinjio ya awali ambayo yalianza kujengwa eneo la Manguanjuki na ujenzi huo ukagharimu shilingi

Serikali yapongezwa kwa kupeleka umeme wilaya ya Mkalama.

Mkuu wa wilaya mpya ya Mkalama mkoani Singida,Edward Ole Lenga,akihimiza shughuli za maendeleo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Gumanga kata ya Nduguti.
MKUU wa wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Edward Ole Lenga ameipongeza serikali kwa juhudi zake ya kutekeleza kwa wakati ahadi yake ya kuipatia umeme wilaya hiyo.
Lenga amesema ujio huo wa umeme wilayani humo, pamoja na mambo mengine, utaharakisha mno, upatikanaji wa maendeleo endelevu.
“Wakati wilaya zingine zilizoanzishwa siku nyingi zimepiga hatua kubwa kimaendeleo,wakati pengine wao kwa sasa zinatembea,sisi wachanga tunatakiwa kukimbia ili tumeze kuzifikia na ikiwezekana tuzipite.Kwa hiyo ujio wa umeme utatusaidia sana katika kufikia hayo malengo”,amesema.
Mkuu huyo wa wilaya, amesema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake, juu ya ahadi ya serikali ya kuipatia wilaya hiyo umeme wa gridi ya taifa.
Amesema hivi sasa shirika la umeme limesambaza nguzo za umeme kuanzia mji mdogo wa

Hospitali ya Rufaa Singida yakabiliwa na uhaba wa watumishi wa afya.


Sehemu ya Majeengo ya Hospitali ya Rufaa mkoani Singida inayokabiliwa na uhaba wa Watumishi wa Afya.

HOSPITALI ya Rufaa mkoani Singida,inakabiliwa na uhaba wa watumishi zaidi ya mia mbili wa kada mbalimbali,kitendo kinachochangia huduma kutokukidhi mahitaji.

 Hospitali hiyo ambayo ipo nje ya mji wa Singida katika barabara ya Sepuka,kwa sasa imeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.Huduma zingine ikiwemo ya akina mama kujifungua,bado hazijaanza.

Hayo yamesemwa na Afisa Muuguzi wa hospitali hiyo, Pendaeli Masai wakati akitoa taarifa yake kwa mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone aliyetembelea hospitali hiyo kujua maendeleo yake.

Amesema  kuwa licha ya hospitali hiyo kuwa  na vifaa   vya kisasa,huduma mbalimbali hazijaanza kutolewa kutokana na uhaba mkubwa wa watumishi.        

 “Tumeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje Desemba mwaka jana na kwa kuanzia tumeanza na watumishi

Utekaji wa magari katika kijiji cha Kisaki washika kasi

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SACP.Geofrey Kamwela, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya tukio la utekaji wa magari katika eneo la Kisaki manispaa ya Singida. Naibu Waziri wa Afrika Mashariki Abdula J. Abdula ametoa wito kwa madereva kuacha mara moja vitendo vya kuziba barabara kwa madai ya kudai haki zao kuwa vinachangia kusababisha madhara mengi.



Mkulima akamatwa na Bhangi misokoto 888 yenye uzito gramu 44

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela.

JESHI la Polisi mkoa wa Singida linamshikilia Mariamu Songeraeli (32) mkulima mkazi wa kijiji cha Nselembwe wilaya ya Iramba kwa tuhuma ya kumiliki madawa ya kulevya aina ya bhangi misokoto 88 yenye uzito wa gramu 44.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema mtuhumiwa Mariamu amekamatwa juzi saa 11.30 jioni nyumbani kwake katika kijiji cha Nselembwe kata ya Shelui wilaya ya Iramba.

Amesema askari polisi waliokuwa kwenye doria siku ya tukio,walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa Mariamu anajihusisha na biashara haramu ya kununua na kuuza bhangi.

Kamwela amesema askari hao waliweza kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa na kuipekua na kisha kuikuta

Tuesday, March 11, 2014

Serikali yashauriwa kuajiri Waganga wa Jadi kupunguza uhaba wa watumishi wa Afya.

Kaimu meya mstahiki wa manispaa ya Singida, Hassan Mkata akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Singida kilichofanyika mkoani Singida.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Singida. Robert Mahili na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida,Hamisi Nguli.
Diwani wa kata ya Unyamikumbi,Mosses Ikaku, akichangia hoja katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Singida kilichofanyika mjini Singida.
Afisa  Ardhi manispaa ya Singida, Angelus John  Camara,akitoa ufafanuzi juu ya sheria ya Ardhi mbele ya kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika mkoani Singida.
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Singida waliohudhuria kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Singida.

KUTOKANA na uhaba mkubwa wa watumishi wa sekta ya afya katika vituo mbalimbali vya afya vikiwemo zahanati,serikali imeshauriwa kuajiri waganga wa jadi ili kupunguza uhaba huo.

Ushauri huo wa bure,umetolewa hivi karibuni na Diwani wa kata ya Unyambwa (CCM) Manispaa ya Singida,Shaban Satu wakati akichangia hoja ya diwani wa kata ya Unyamikumbi,Mosses Ikaku ambaye alidai zahanati ya kata yake imekuwa na mhudumu moja tu kwa kipindi kirefu.

Amesema uzoefu unaonyesha kuwa uhaba wa wahudumu wa afya una athari nyingi ikiwemo ya utoaji wa huduma usiokidhi mahitaji.

“Diwani mwenzetu ametueleza kwamba kwa muda mrefu amefikisha tatizo la uhaba wa wahudumu katika ngazi husika mara nyingi,lakini juhudi zake hazijazaqa matunda hadi sasa”,amesema.

Amesema endapo serikali imeshindwa kulitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo hilo,basi ni bora ikatoa nafasi kwa waganga wa jadi kuziba mapungufu hayo”,alifafanua.

Katika hatua nyingine,imedaiwa kuwa shule ya msingi ya kijiji cha Mwankoko,inakabiliwa na uhaba wa madawati 316.

Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo,Robert Mahili aliiomba serikali ya kijiji hicho kuongeza juhudi zaidi kuhamasisha wananchi