Sunday, March 16, 2014

Wanawake washauriwa kuanzisha ufugaji wa Kuku wa kienyeji.

Mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida.Fatma Hassan Toufiq, akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya siku tatu inayohudhuriwa na viongozi wa UWT wilaya ya Manyoni.Pamoja na mambo mengine, mada ya ujasiriamali itatolewa.Wa kwanza kushoto ni katibu wa UWT wilaya ya Manyoni, Defroza Lucas na kulia ni mwenyekiti wa UWT, Mwanaidi Issa.

Baadhi ya viongozi wa UWT wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida,wakaifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM wilaya ya Manyoni.Mada zinazotolewa kwenye semina hiyo ni pamoja na Ujasiriamali,Ukimwi na uendeshaji wa jumuiya hiyo ya CCM.

MKUU wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida, Fatma Hassan Toufiq amewaagiza wanawake wilayani humo, kuanzisha ufugaji wa kibiashara wa kuku wa kienyeji, ili waweze kuharakisha kujikomboa kiuchumi.

 Mkuu huyo wa wilaya, ametoa changamoto hiyo hivi karibuni wakati akifungua semina ya siku tatu inayohudhuriwa na vingozi wa jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Manyoni.

Amesema kuwa uzoefu unaonyesha wazi kwamba wanawake wengi hawana mali inayokubalika na taasiis za kifedha yakiwemo mabenki, kuweka dhamana ili waweze kupata mkopo.

Toufiq amesema kutokana na ukweli huo, njia rahisi kwa wanawake kujikomboa kiuchumi, ni kuanzisha ufugaji wa kibiashara wa kuku wa kienyeji pamoja na kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa.

“Kuku wa kienyeji wa mkoa wa Singia wakiwemo na wa wilaya ya Manyoni, wanapendwa sana hapa nchini. Soko lake ni kubwa kila mahali ikiwemo miji mikubwa kama Dar es salaam na Arusha.  Tukianzisha ufugaji bora wa kuku wa kienyeji, nina hakika familia husika zitaondokana na umaskini na hivyo kuishi maisha bora.wilaya”,alifafanua Dc huyo.

Aidha, mkuu huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wanawake kuwa gonjwa hatari la
ukimwi bado lipo na halijapta chanjo wala dawa.

“Ukiangalia takwimu zote za maambukizi na wagonjwa wa ukimwi, zinaonyesha wanawake ndio waathirika wakubwa.  Kwa hiyo wanawake wenzangu, nawaombeni sana tuchukua tahadhari ya hali ya juu, ili kukepukana na vitendo vinavyochangia maambukizi mapya ya virusi vinavyosababisha gonjwa la ukimwi”,amesema.


Awali katibu wa UWT wilaya ya Manyoni, Mwanaidi Kalegela alitaja mada za semina hiyo kuwa ni pamoja na elimu ya ujasiriamali, namna ya kujikinga na ukimwi na kubadilishana uzoefu utakaosaidia kuimarisha UWT wilayani humo.

No comments:

Post a Comment