Mkuu wa wilaya mpya ya Mkalama mkoani Singida,Edward Ole Lenga,akihimiza shughuli za maendeleo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Gumanga kata ya Nduguti.
MKUU wa wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Edward Ole Lenga ameipongeza serikali kwa juhudi zake ya kutekeleza kwa wakati ahadi yake ya kuipatia umeme wilaya hiyo.
Lenga amesema ujio huo wa umeme wilayani humo, pamoja na mambo mengine, utaharakisha mno, upatikanaji wa maendeleo endelevu.
“Wakati wilaya zingine zilizoanzishwa siku nyingi zimepiga hatua kubwa kimaendeleo,wakati pengine wao kwa sasa zinatembea,sisi wachanga tunatakiwa kukimbia ili tumeze kuzifikia na ikiwezekana tuzipite.Kwa hiyo ujio wa umeme utatusaidia sana katika kufikia hayo malengo”,amesema.
Mkuu huyo wa wilaya, amesema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake, juu ya ahadi ya serikali ya kuipatia wilaya hiyo umeme wa gridi ya taifa.
Amesema hivi sasa shirika la umeme limesambaza nguzo za umeme kuanzia mji mdogo wa
Iguguno na linaendelea vizuri kuzichmbia katika vijiji vyote ya kando kando ya barabara inayoelekea Nduguti makao makuu ya wilaya.
“Wananchi kwa ujumla wilayani kwetu baada ya kuona kasi ya uchimbaji wa nguzo za umeme, na wao pia wanakwenda na na kasi hiyo hiyo katika kuweka nyaya za umeme (wiring) kwenye nyumba zao za kuishi na za biashara. Nawapongeza sana kwa hilo”,amesema Lenga.
Akifafanua,Mkuu huyo wa wilaya,amesema kutokana na nguzo za umeme kusambazwa katika vijiji vingi na pamoja na kasi ya uchimbiaji muda mfupi ujao, huduma ya umemme itakuwa inapatika wilayani humo bila shida yoyote.
“Aidha,nitumie fursa hii kuwahimiza wananchi kujiandaa mapema kutumia fursa ya huduma ya umeme, katika uhakikisha wanajipatia maendeleo yao binafsi na ya wilya yetu kwa ujumla” ,alifafanua zaidi.
Katika hatua nyingine,Lenga anawapongeza wananchi wa Nduguti makao makuu ya wilaya ambao wameanza kuweka nyaya za umeme (Wiring) kwenye majengo yao wanayotarajia kuanzisha viwanda vidogo ikiwemo vya kukamua mafuta ya alizeti.
Wakati huo huo,Lenga amesema amefarijika mno kwa ujio wa huduma ya umeme kwa madai kwamba utasaidia wialya hiyo kuondokana na nyumba za tembe katika muda mfupi ujao.
“Kwa muda sasa wilaya yetu ya Mkalama imekuwa inatekeleza vizuri programu ya kuondoa nyumba za tembe na kujenga nyumba bora na za kisasa. Ujio wa umeme, utakuwa chachu kwa wananchi kujenga nyumba bora, kwa sababu umeme sio rahisi kuingizwa kwenye nyumba za tembe”,alisema mkuu huyo wa wilaya.
No comments:
Post a Comment