Tuesday, March 11, 2014

Serikali yashauriwa kuajiri Waganga wa Jadi kupunguza uhaba wa watumishi wa Afya.

Kaimu meya mstahiki wa manispaa ya Singida, Hassan Mkata akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Singida kilichofanyika mkoani Singida.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Singida. Robert Mahili na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida,Hamisi Nguli.
Diwani wa kata ya Unyamikumbi,Mosses Ikaku, akichangia hoja katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Singida kilichofanyika mjini Singida.
Afisa  Ardhi manispaa ya Singida, Angelus John  Camara,akitoa ufafanuzi juu ya sheria ya Ardhi mbele ya kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika mkoani Singida.
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Singida waliohudhuria kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Singida.

KUTOKANA na uhaba mkubwa wa watumishi wa sekta ya afya katika vituo mbalimbali vya afya vikiwemo zahanati,serikali imeshauriwa kuajiri waganga wa jadi ili kupunguza uhaba huo.

Ushauri huo wa bure,umetolewa hivi karibuni na Diwani wa kata ya Unyambwa (CCM) Manispaa ya Singida,Shaban Satu wakati akichangia hoja ya diwani wa kata ya Unyamikumbi,Mosses Ikaku ambaye alidai zahanati ya kata yake imekuwa na mhudumu moja tu kwa kipindi kirefu.

Amesema uzoefu unaonyesha kuwa uhaba wa wahudumu wa afya una athari nyingi ikiwemo ya utoaji wa huduma usiokidhi mahitaji.

“Diwani mwenzetu ametueleza kwamba kwa muda mrefu amefikisha tatizo la uhaba wa wahudumu katika ngazi husika mara nyingi,lakini juhudi zake hazijazaqa matunda hadi sasa”,amesema.

Amesema endapo serikali imeshindwa kulitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo hilo,basi ni bora ikatoa nafasi kwa waganga wa jadi kuziba mapungufu hayo”,alifafanua.

Katika hatua nyingine,imedaiwa kuwa shule ya msingi ya kijiji cha Mwankoko,inakabiliwa na uhaba wa madawati 316.

Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo,Robert Mahili aliiomba serikali ya kijiji hicho kuongeza juhudi zaidi kuhamasisha wananchi
kuchangia ununuzi wa madawati.

Amesema pia juhudi zilifanyika za za kuzishawishi benki ya NBC,CRDB,NMB na CIP,ili ziweze kusaidia kuondoa uhaba huo mkubwa wa madawati.


Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi,Mahili,manispaa hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu 298.

No comments:

Post a Comment