Friday, October 10, 2014

Tamasha la Fiesta 2014 laiteka Singida.

Baadhi ya mwashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 wakishangilia kwa hisia,wakati shoo ikiendelea jukwaani ndani uwanja wa Namfua mjini Singida.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kampuni ya No Fake Zone,Linah Sanga ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Oletemba,akiimba jukwaani mbele ya umati wa watu wakati wa tamasha la Fiesta lililofanyika jana katika uwanja wa Namfua,kulia ni mmoja wa wacheza shoo wake akiwajibika jukwaani.
Kundi mahiri la muziki wa kizazi kipya litambulikalo kwa jina la Makomando wakilishambulia jukwaa la Fiesta hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya Uwanja wa Namfua hapo jana mjini Singida.

 Mmoja wa mashabiki akishangilia huku akiwa amebebwa.
Msanii wa muziki wa bongofleva,Mr Blue a.k.a Kabyssal akiimba mbele ya umati wa wakazi wa mji wa singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua.
Sehemu ya umati wa watu ndani ya tamasha la Fiesta mjini Singida hapo jana katika uwanja wa Namfua


Ilikuwa ni shangwe tu ndani ya uwanja wa Namfua wakati tamasha la Fiesta likiendelea.
Msaniii mwingine anaefanya vyema katika anga ya muziki wa bongofleva,kupitia kundi la WEUSI,Niki wa Pili akiwaimbisha mashabiki wake.
 Shabiki kapagawa na yaliyokuwa yakijiri jukwaani.
Badala ya kuwa watazamaji tu,nao pia walikuwa wakijimwaya mwaya taratiibu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Rachael akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani),wakati wa tamasha la Fiesta likendelea ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes anaetamba na wimbo wake wa Togola akiwaimbisha mashabiki wake,kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kizazi kipya atambulikae kwa jina kisanii Mwana-FA akiimba mbele ya umati wa wakazi wa Singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2014,lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Namfua.
Msanii Mwana-FA na Linah wakiimba kwa pamoja jukwaani,huku miluzi na makelele ya mashabiki yakiwa yametawala kila kona ya uwanja wakati wa tamasha la Fiesta likiendelea.

Wasanii mahiri wa muziki wa Bongofleva, Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kupitia wimbo wao unajojulikana kwa jina la Huko kweni Vipi,ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Singida wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya tamasha la Fiesta.

No comments:

Post a Comment