Saturday, April 25, 2015

CHAWAMAMU waendesha mafunzo Singida kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Mratibu wa Tiba Asilia kutoka Hospitali ya Wilaya ya Iramba, Bi Roda Yona(kushoto) na Mkuu wa Kituo kidogo cha polisi Ndago, Bwana Richard Kimolo (kulia) wakishiriki mafunzo ya kutoa elimu juu ya operesheni tokomeza mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na vikongwe.
Katibu Msaidizi wa CHAWAMAMU Mkoa wa Singida, Bwana Omari Majengo (kulia) wakiwa kwenye ukumbi wa shule ya msingi Urughu, tarafa ya Ndago wilayani Iramba wakitoa elimu juu ya operesheni tokomeza mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na vikongwe na Kushoto ni Afisa tarafa wa tarafa ya Ndago, Bwana Anthoni Magesa Ntarle.

 Afisa tarafa wa tarafa ya Ndago,Bwana Anthoni Magesa Ntarle.
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Watafiti wa Malaria sugu, Ukimwi na Mazingira Tanzania (CHAWAMAMU) Mkoa wa Singida,Bwana Tano Mika Likapakapa.
Waganga wa tiba mbadala,Wakunga,Wenyeviti wa vijiji, Maafisa watendaji wa vijiji,Maafisa watendaji wa kata,Wenyeviti wa vitongoji pamoja na baadhi ya watumishi wa serikali waliopo katika kata ya Urughu wakihudhuria semina ya operesheni tokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na vikongwe.

CHAMA cha Watafiti wa Maleria Sugu,Ukimwi na Mazingira Tanzania (CHAWAMAMU) Mkoa wa Singida kimeanza kutoa mafunzo kwa waganga na wakunga wa tiba mbadala waliopo Mkoani hapa yanayolenga kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino ) na vikongwe hapa nchini.

Aidha mafunzo hayo yanayotolewa kwa waganga na wakunga wa tiba mbadala,vile vile yanalenga juu ya kuwahamasisha waganga wa tiba ambadala ambaao hawajasajiliwa katika chama hicho waweze kujisajili na kutambulika kisheria ikiwa ni sambamba na kuachana na vitendo vya kupiga ramli chonganishi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CHAWAMAMU Mkoa wa Singida,Dk.Tano Mika Likapakapa kwenye semina elekezi ya siku sita kwa waganga wa tiba mbadala na wakunga  yaliyofanyika katika Kijiji cha Urughu,tarafa ya Ndago,wilayani Iramba,Mkoani Singida.

Alifafanua Dk.Likapakapa kwamba elimu hiyo itolewayo kwa waganga wa tiba mbadala na wakunga hao ni mfululizo wa operesheni maalumu ya kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi,yaani albino pamoja na vikongwe hapa nchini, agizo lililotolewa na Rais Dk.Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa katibu mkuu huyo wa CHAWAMAMU imebainika kwamba idadi kubwa ya waganga wa tiba mbadala  wamekuwa wakiishi na vitu vinavyoashiria dalili za kujihusisha na upigaji ramli chonganishi na kuvitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni pamoja na mapembe ya wanyama,ngozi za wanyama,ngozi za wadudu na kwamba vitu hivyo ndivyo viashiria vikubwa vya waganga hao kujihusisha na upigaji wa ramli.

Akimkaribisha kuwasilisha mada katika semina hiyo kwa waganga wa tiba mbadala na wakunga,afisa tarafa wa Ndago,Anthoni Magege aliweka wazi kwamba kutokana na wimbi kubwa la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na vikongwe kuongezeka kwa kasi nchini,serikali imelazimika kuchukua hatua za haraka za kuwaelimisha wananchi kuachana na tabia ya kupiga ramli chonganishi.

Alisema afisa huyo wa tarafa kwamba kati ya waganga wa tiba mbadala mia moja waliopo katika tarafa ya Ndago lakini awali walipoandaa semina makao makuu ya tarafa na kumwalika mkuu wa polisi wa wilaya hiyo,lakini walioweza kuhudhuria ni waganga 87 tu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Urughu,Omari Abdallah Mitigo alisema ili kuondokana na visa kati ya mtoa taarifa na mganga anayeendeleza vitendo vya ramli chonganishi ni vyema kukawepo usiri mkubwa wa watu wanaowafichua watu wa aina hiyo.


Naye Afisa mtendaji wa kijiji cha Mang’ola,Mussa Ismaili Kitila alitumia fursa hiyo kuliomba jeshi la polisi kutojihusisha na utoaji wa vibali kwa waganga wa tiba mbadala wanaodai wana uwezo wa kufufua watu waliokufa pamoja na kutoa misukule kwenye nyumba za watu kwa madai kwamba kumekuwepo tabia kwa baadhi ya waganga wanapoulizwa walipopatia vibali,nao hudiriki kulitaja jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment