Saturday, April 25, 2015

Wizara ya afya yafuta vibali vilivyotolewa na maafisa utamaduni kwa waganga wa tiba mbadala.

Mkuu wa kituo kidogo cha polisi Ndago, Bw.Richard Kimolo (kushoto), Diwani wa kata ya Mbelekese, Bi Monica Samweli (wa pili kutoka kushoto), Katibu mkuu CHAWAMAMU Mkoa wa Singida, Dk.Tano Mika Likapakapa wakiwa kwenye semina ya operesheni tomomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na vikongwe inayoendelea tarafa ya Ndago, wilayani Iramba.
Mratibu wa Tiba Asilia kutoka Hospitali ya wilaya ya Iramba, Bi Dora Yona(wa pili kukulia) akijiandaa kutoa mada ya waganga wa tiba mbadala kufuata sharia,kanuni na taratibu za utoaji tiba kwa wateja wao.

 Polisi kata ya Mbelekese, Bw.Juma Seif( kulia) na afisa kilimo kata ya Ndago, Bi Perpetua Pius (kushoto).

Polisi kata ya Mbelekese, Bw.Juma Seif( kulia) na afisa kilimo kata ya Ndago, Bi Perpetua Pius (kushoto).

WIZARA ya Afya na Ustawi wa jamii imefuta vibali vyote vilivyotolewa na maafisa utamaduni katika Halmashauri za wilaya,Miji,Majiji pamoja na Manispaa nchini vinavyowaruhusu waganga wa tiba mbadala kuendelea kufanya shughuli zao za tiba kuanzia sasa na badala yake vibali hivyo vitakuwa vikitolewa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Watafiti wa Maleria Sugu,Ukimwi na Mazingira Tanzania(CHAWAMAMU).

Aidha kutokana na wizara hiyo kufuta vibali hivyo,wizara ya afya na ustawi wa jamii pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kushirikiana na chama cha Watafiti wa Maleria Sugu,Ukimwi na Mazingira Tanzania (CHAWAMAMU),ndiyo watakaokuwa wakitoa vibali hivyo.

Katibu mkuu wa CHAWAMAMU Mkoa wa Singida,Dk.Tano Mika Likapakapa alitoa kauli hiyo kwenye semina elekezi kwa waganga wa tiba mbadala katika kata ya Kaselya,tarafa ya Ndago wilayani Iramba iliyofanyika kweneye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Kijiji hicho.

Hata hivyo Dk.Likapakapa ambaye pia ni Mjumbe maalumu wa operesheni tokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na vikongwe kitaifa alifafanua kuwa vibali vitakavyoendelea kutolewa na idara ya utamaduni ni vile tu vitakavyohusika na sekta ya michezo,ikiwemo ngoma,mpira wa miguu na mchezo wa rede.

“Lakini wizara ya afya na ustawi wa jamii na wizara ya mambo ya ndani kwa kushirikiana na Chama cha Watafiti wa Maleria Sugu,UKIMWI na Mazingira Tanzania (CHAWAMAMU) ndivyo ambavyo vitatoa vibali vya kuendelea kutoa huduma za tiba mbadala kwa wananchi,tuko pamoja…kwa hiyo hata ninyi wenye vibali vya idara ya utamaduni kama mpo hapa kila mmoja tutaangalia vibali vyake na majina yenu yote tunayo hapa”alisisitiza Dk.Likapakapa.

Hata hivyo Dk.Likapakapa hakusita kuwatahadharisha watendaji wa serikali watakaoonyesha udhaifu katika utekelezaji wa zoezi hilo muhimu lililotolewa na kiongozi mkuu wa nchi kuwa nao hawatasita kuchukuliwa hatua za kisheria kama ambavyo waganga wa tiba mbadala watakavyoshughulikiwa kwa kutotii agizo hilo.

Wakichangia hoja ya kufutwa kwa vibali vyote vilivyotolewa na idara ya utamaduni katika Halmashauri za wilaya,Miji,Majiji pamoja na Manispaa baadhi ya viongozi wa vitongozi,vijiji,waganga wa tiba mbadala na wakunga walitaka kufahamu watawahudumiaje wateja wao bila kupiga ramli kwa kutumia nyara za serikali wakati hata wateja wao wamezoea kuelezwa matatizo yao kwa kupitia ramli inayotumia vifaa hivyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Ndala juu,Kijiji cha Kaselya,Nandi Jumanne alihoji kwamba endapo mganga wa tiba mbadala ataletwa katika Kitongoji chake bila yeye kufahamu na hata kuhusishwa na aliyemleta,na baada ya kutoa huduma zilizoleta madhara na kuondoka wananchi wakatoa taarifa polisi,je yeye kama kiongozi itakapotokea jambo kama hilo itakuwaje.

Holoji Lolelo ambaye ni mganga wa tiba mbadala kata ya Kaselya alikwenda mbali zaidi kwa kuhoji je wateja wanaokwenda kuhudumiwa na baada ya kupona wanawadhulumu malipo waliyokubaliana nao kulipia gharama za matibabu,je serikali itawasaidiaje maana watu kama hao wanachangia kupunguza mapaato yao.


Akifunga semina hiyo elekeze diwani wa kata ya Kaselya,Eliasi Kitalama alitumia fursa hiyo kuwashauri viongozi wa ngazi zote kurejesha utamaduni uliokuwepo miaka ya nyuma ambapo kila nyumba iliyofikiwa na mgeni mwenyeji wake alilazimika kutoa taarifa kwa kiongozi wake wa shina.

No comments:

Post a Comment