Friday, April 4, 2014

Wafanyabiashara watekwa na maafisa usalama feki.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.

WAFANYABIASHARA wa Manyoni mjini mume na mke,wametekwa na watu watatu waliojifanya kuwa ni maafisa usalama wa taifa makao makuu jijini Dar-es-salaam.

Waathirika wa utekaji huo ni Methew Dominik @ Cheupe (46) na mke wake Selina Methew (42).

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea juzi saa tisa alasiri Manyoni mjini.

Amesema Faraja George (35) mfanyabiashara wa Dodoma mjini,mganga wa tiba asilia na mkazi wa mkoa wa Tanga,Saidi Mgolola @Pesa mbili (49) Michael Peter  na Michael Peter (26) mkazi wa Moshi mjini na dereva wa gari lililotumika katika utekaji huo.

Amesema siku ya tukio watuhumiwa wakiwa na gari T.242 CBM aina ya toyota prado,walifika dukani kwa Methew baada ya kudai kuwa wao ni maafisa usalama taifa,walimwamuru mwenye duka kuwa wanamhitaji Singida mjini kwa ajili ya mahojiano.

“Methew aliwaomba maafisa hao bandia kuwa aambatane na mke wake huko kwenye mahojiano hayo.Baada ya waathirika hao kuingia ndani ya gari,gari hilo badala ya kuelekea Singida mjini,lilibadili na kuelekea Dodoma”,amesema.

Kamwela amesema bahati nzuri polisi Manyoni mjini walipata taarifa ya tukio hilo mapema na wakawasiliana na wenzao wa Bahi mkoani Dodoma ambao walifanikiwa kuwanasa watuhumiwa hapo kwenye kizuizi.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo,ni watuhumiwa kutaka

Singpress yapata katibu mtendaji mpya.

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida, Seif Takaza akifungua mkutano mkuu wa kawaida wa klabu hiyo uliofanyika mjini Manyoni mwishoni mwa wiki.Kulia ni makamu mwenyekiti Damiano Mkumbo na kulia ni kaimu katibu mtendaji,Emmanuel Michael.
Baadhi ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,wakifuatilia mkutano mkuu wa kawaida wa (mwaka 2013) klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa Katoliki mjini Manyoni.

KLABU ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida imemchagua kwa kishindo Pascal Tantau (32),kuwa katibu wake mtendaji kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Abby Nkungu ambaye anadai kwa sasa afya yake ina mgogoro.

Pascal kijana aliyemaliza chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) alipata kura 15 za ndio,mbili zilimkataa na moja iliharibika.

Pascal atakuwa madarakani hadi mwishoni mwakwani (2015) uchaguzi mkuu utakapofanyika kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.

Pascal aliwashukuru wanachama wenzake kwa kumwamini na kumkabidhi nafasi hiyo nyeti. Ameahidi kwamba atawatumikia kwa nguvu zake zote na kwa maarifa lengo kuu ikiwa ni  klabu hiyo iweze kupaa kimaendeleo katika kipindi chake cha uongozi.

“Niwaahidi pia kwamba katika uongozi wangu nitatumia mbinu shirikishi ili kila mwananchama aweze kutoa mchango wake mbalimbali kuendeleza klabu na kuboresha ustawi wa wananchama.Nitajitahidipia kuhakikisha klabu inakuwa na mahusiano mazuri na wadau wake mbalimbali”, alisema kwa kujiamini.

Abby Nkungu amelazimika kujiuzulu nafasi ya ukatibu mtendaji wa Singpress,kwa madai kwamba ameagizwa na daktari wake aishiye nchini

Queen Mlozi ashiriki operasheni ya kuondoa mawe makubwa yaliyokuwa yakitumiwa kuteka magari barabara kuu ya Singida-Dodoma.

Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi akipasua jiwe kubwa ili liweze kupandishwa kwenye lori kwa lengo kuondolewa kando kando ya barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida. Mawe hayo makubwa kwa kipindi kirefu yametumiwa na watu wanaodhaniwa ni majamabazi watekaji wa malori na kupora mali na fedha.
Mkazi wa kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida, Juma akipasua jiwe kubwa lililokuwa likitumiwa na majambazi kwa ajili ya kuteka magari na kisha kupora abiria.
Askari Polisi, Jeshi na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida,wakipandisha jiwe kubwa kwenye lori. Zoezi hilo la kuondoa mawe makubwa kando kando ya barabara kuu ya Singida yaliyokuwa yakitumiwa na watu wanaodhaniwa ni majambazi katika kuteka magari na kupora abiria. Mawe hayo mwishoni mwa mwaka jana yalitumika kuteka gari la chuo cha SUA Morogoro na kisha maiti ndani ya sanduku. 

China kuwekeza kwenye kilimo mkoani Singida.

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone (wa kwanza kulia) akimwonyesha Balozi wa Jamhuri ya watu wa China,Dk.Lu Youqing (katikati) eneo lililopo katika kijiji cha Kisasida manispaa ya Singida mahali umeme wa nishati ya upepo utazalishwa  na kampuni kutoka nchini China. Kushoto ni mwakilishi mkuu wa uwakilishi wa kiuchumi na kibiashara wa Jamhuri ya watu wa China nchini, Lin Zhiyong.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone (mwenye suti nyeusi) akibadilishana mawazo na Balozi wa Jamhuri ya watu wa China (katikati) wakati Balozi huyo alipotembelea eneo la kijiji cha Kisasida manispaa ya Singida mahali kampuni ya Kichina, inatarajiwa kuanza kuzalisha umeme wa nishati ya upepo.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone (kulia) akizungumza ofisini kwake na baadhi ya viongozi waliokuwa wameambatana na Balozi wa Jamhuri ya watu wa China hapa nchini, Dk.Lu Youqing katika ziara ya balozi huyo mkoani Singida.

BALOZI wa Jamhuri ya watu wa China hapa nchini, Dk.Lu Youqing amesema nchi yake inatarajia kuwekeza kwenye sekta mbalimbali mkoani Singida ikiwemo sekta ya kilimo na ufugaji, ili kuharakisha kukuza uchumi wa mkoa huo.

Balozi Youqing aliyasema hayo wakati akizungumza ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo.

Amesema uwekezaji huo utawanufaisha wakazi wengi wa mkoa wa Singida ambao ni wakulima na wafugaji.

Balozi Youqing alifafanua zaidi kwa kusema kuwa kwa kuanzia,China kupitia kampuni yake moja imeonyesha nia ya kuwekeza katika kufua umeme wa kutumia nishati ya upepo.


“Tanzania ina hitaji kubwa la umeme wa upepo ambao utakuwa wa gharama ndogo na hauchafui mazingira”,amesema.

Akisisitiza zaidi, amesema kuwa kutokana na historia ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China, sekretarieti za mikoa na serikali za mitaa, zina fursa ya kushirikiana na mamlaka za serikali za mikoa nchini China ili kujifunza teknolijia mbalimbali.

Akiijengea nguvu hoja yake hiyo, Balozi Youqing amesema

Mamlaka ya maji Singida yadai zaidi shilingi milioni 210.

Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya maji manispaa ya Singida.Wa kwanza kulia (walioketi) ni Kaimu Mkurugenzi wa SUWASA ,Eng.Kombe Mushi, anayefuatia ni Meya Mstahiki manispaa ya Singida na Sheikh mkoa wa Singida, Salum Mahami na Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya Masi safi na mazingira safi (SUWASA) Singida mjini, Eng.Kombe Mushi,akitoa taarifa yake ya utendaji wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya maji.
Mkurugenzi wa manispaa ya Singida, Joseph Mchina, akitoa nasaha zake kwenye maadhimisho ya wiki ya maji katika manispaa hiyo yaliyofanyika Mandewa mjini Singida.
Mwenyekiti wa bodi ya SUWASA, Kisenge akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi wa wiki ya maji manispaa ya Singida.
Tanki la maji la SUWASA lililopo Mandewa mjini Singida.

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (SUWASA) Singida mjini, inadai wateja wake mbalimbali zaidi ya shilingi 210.9 milioni, kitendo kinachochangia kudhoofisha utendaji wa mamlaka hiyo.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji SUWASA, Eng. Kombe Mushi wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya maji uliofanyika Mandewa nje kidogo ya mji wa Singida.

Amesema kati ya madeni hayo, wateja binafsi wanadaiwa zaidi ya shilingi 123.7 milioni, wakati wafanyabiashara mbali mbali, wanadaiwa zaidi ya shilingi 12.9 milioni.

“Taasisi mbali mbali za serikali, tunazidai shilingi 70,750,185 na madhehebu ya dini tunayadai zaidi ya shilingi 3.6 milioni.  Fedha hizi nyingi, endapo tutalipwa zote, zitatusaidia mno kuboresha utoaji wa huduma zetu”,amesema Kaimu Mkurugenzi huyo.

Aidha, Eng.Kombe amesema mbaya zaidi ni kwamba badhi ya wadaiwa hao, hushindwa kurejesha huduma ya maji na badala yake, kununua maji kutoka kwa majirani au kujiunganishia maji na kuchepusha dira za maji.

“Changamoto zingine tunayokabiliana nayo ni, upotevu wa maji kupitia mifimo chakavu ya maji.  Kwa wastani upotevu huo ni asilimia 43.  Hata hivyo tumejipanga vizuri kwa ajili ya kulimaliza tatizo hilo”,alifafanua.

Katika hatua nyingine, Eng. Mushi amewataka wananchi kuwafichua watu wanaojiunganishia maji kiholela na wanaochepusha dira ya maji.  Bingo ya shilingi

Soko la Nyuki ni mkombozi wa kiuchumi kwa Wafugaji – Dk. Kone.

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, (wa nne kulia) akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa utundikaji wa mizinga ya Nyuki mkoani Singida.Wa pili kushoto ni mkuu wa wilaya ya Mkalama Edward Ole Lenga.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida, Edward Ole Lenga, akizungumza kwenye hafla ya utundikaji mizinga ya nyuki kimkoa zilizofanyika katika kijiji cha Nkungi wilayani Mkalama.Wa pili kulia walioketi,ni mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone na (wa kwanza kulia) ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama,James.Kushoto (aliyekaa), ni Katibu tawala mkoa wa Singida Liana Hassan.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akiweka nta kwenye mzinga wa Nyuki kama njia moja wapo ya kuwavutia Nyuki ili waweze kupanga kwenye mzinga huo.

MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone ameziagiza Halmashauri na Manispaa ya Singida, kuanzisha au kuunda ushirika utakaosaidia wafugaji kupata soko zuri la mazao ya nyuki ili waweze kuharakisha kujikomboa kiuchumi.

 Dk.Kone ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya taifa ya utundukaji mizinga ngazi ya mkoa yaliyofanyika kimkoa wilayani Mkalama.

Amesema utundikaji huo wa ushirika wa wafuga nyuki ni agizo lililotolewa na Waziri Mkuu kuwa kila mkoa uwe na ushirika huo.

Akifafanua zaidi,Dk.Kone amesema ushirika wa wafugaji nyuki,una faida nyingi ikiwemo wafugaji kupata soko zuri na la uhakika.

Kuhusu siku ya utundikaji mizinga,amesema lengo lake ni kuhamasisha ufugaji nyuki ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa kuzingatia ubora na teknolojia sahihi.

 “Kwa kutumia teknolojia sahihi,wananchi watazalisha

Albino mbaroni kwa kumchuna Ngozi Mtoto sehemu yake ya siri.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida SACP, Geofrey Kamwela.

MKULIMA mkazi wa kijiji cha Nkalankala kata ya Mwanga,tarafa ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) ,Hidaya Omari (20),anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumnyonga hadi kufa, mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka moja na nusu,na kisha kumchuna ngozi katika sehemu yake ya siri.

Mtoto aliyenyongwa na kuchunwa ngozi ya sehemu yake  ya siri na kutupwa kwenye kisima cha maji chenye kina cha mita moja,ni Richard Paulo.

Imedaiwa pia mama yake mzazi na mtuhumiwa Hidaya,Neema Paulo (35), naye anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kuhusika  kumnyonga Daudi Richard na kumsababishia kifo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida,SACP,Geofrey Kamwela,alisema tukio hilo la kusikitisha,limetokea machi 13 mwaka huu saa moja na nusu asubuhi huko katika kijiji cha Nkalankala wilayani Mkalama.

Alisema mtoto huyo Daudi,aliokotwa akiwa anaelea juu ya maji ya kisima chenye urefu wa mita moja.

Kamwela alisema uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi,umebaini kuwa Daudi (marehemu) aliuawa na kuchunwa