Tuesday, September 16, 2014

Kampuni ya Shanta ya uchimbaji wa dhahabu yakabidhi hundi ya milioni 41.5 kwa kikundi cha Aminika Gold Mine cha Sambaru,

Meneja mkuu wa shanta akizungumza kwenye mkutano wa makabidhiano ya hundi hiyo jana.
Kaimu Katibu Mkuu wa kikundi cha Aminika Antony Muhenyi akisoma agenda ya mkutano huo maalumu kwa wanachama wa Aminika.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Shanta, Gold Mining  Limited, Zone Swanepoel (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 41.5 Mwenyekiti wa kikundi cha Aminika Gold Mining Cooperative Society Limited, Francis Mbassa kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya hundi hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Sambaru.

Wawili wapoteza maisha na 52 wajeruhiwa ajali ya basi Singida.

Askari wa usalama barabarani wilaya ya Ikungi, akikagua basi la kampuni ya KISBO, T.534 CHX baada ya kupinduka katika eneo la kijiji cha Kambi ya mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 52.
Basi la kampuni ya KISBO T.534 CHX linavyoonekana baada ya kupasuka tairi la mbele kulia na kuacha barabara na kisha kupinduka katika kijiji cha Kambi ya mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi.
Mwili wa abiria wa kike anayedaiwa kuwa na umri katika ya miaka 20-23 aliyefariki dunia kwenye ajali ya basi la KISBO iliyotokea katika kijiji cha Kambi ya mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi.

Dereva Gabreil Joseph wa basi la ABC apongezwa na abiria.

Basi la ABC T.433 CVL linaloendeshwa na dereva mbunifu,Gabriel Joseph.
Dereva wa basi la kampuni ya ABC,Gabriel Joseph ifanyayo safari zake kati ya Singida-Dar-es-salaam apongezwa kwa nidhamu yake ya kuwajali wateja wake kwa kuwaita ni sehemu ya familia ya kampuni ya ABC. Pichani ni Dereva Gabriel,a kitoa matangazo mbalimbali wakati wa safari ikiwemo kuwahimza wanafamilia kuhakikisha wamefunga mikanda ya usalama.

DEREVA wa kampuni ya mabasi ya ABC yafanyayo safari zake kati ya Singida na Dar-es-salaam, Gabriel Joseph, amepongezwa kwa hatua yake ya kupandisha hadhi ya wateja wake kwa kuwabatiza jina la wanafamilia wa ABC, badala ya jina la abiria lililozoeleka kwenye vyombo mbalimbali vya usafiri.

Gabriel pamoja na kupandisha hadhi ya abiria wake na kuwaita wanafamilia ya ABC, pia amebuni mbinu mpya ya kuwavutia wanafamilia wa ABC,kwa kuwapa taarifa za mara kwa mara pindi wanapomaliza wilaya na mkoa husika na kuwaarifu wanaingia wilaya nyingine na kutaja mkoa na kilometa za kutembea katika wilaya hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafamilia hao waliokuwa wakisafiri na basi T.433 CVL lililokuwa likiendeshwa na Gabriel,wamedai kwamba kuitwa

Tuesday, September 2, 2014

Mfanyabiashara wa madini apata ajali mbaya ya gari lake iliyopelekea kupasuka kichwa na kufariki papo hapo.

Gari lililokuwa limebeba mwili wa mfanyabiashara wa madini ya Coper Henrico Kairuki likiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.
Hii ni sehemu ya kichwa cha marehemu Kairuki kilichopasuka hadi Ubongo kutoka nje.
 Ndugu jamaa wakishusha mwili wa mpiganaji Kairuki kwenye gari katika chumba cha maiti.

Afariki baada ya kutibiwa na daktari feki Singida.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela.

MKULIMA na mkazi wa kijiji cha Iyumbu tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Jubulu Mahende,amefariki dunia muda mfupi baada ya kupewa matibabu na mtu anayedaiwa kuwa ni daktari feki.

Imedaiwa kuwa Jubulu aliyekuwa akisumbuliwa na kifua, kiuno na mgongo alizidishiwa dawa kitendo kilichopelekea hali yake kuwa mbaya zaidi.

Daktari huyo ambaye amekiri hana cheti cha aina yo yote kutoka vyuo vya afya,Prospa Simson,baada ya kubaini hali ya mteja wake inakuwa mbaya,alimpa

Waandishi waaswa kuhimiza Afya ya Uzazi na Jinsia.

Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Fedes  Mdala, akizindua uhamasishaji wa masula ya ushiriki sawa wa masuala ya Afya ya Uzazi na Ujinsia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mandewa mjini Singida.
Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la YMC la mjini Singida, Fidelius Yunde, akihamasisha wananchi wakiwemo vijana na wanaume wa Mandewa mjini Singida, umuhimu wa ushiriki sawa wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.
Kikundi cha uhamasishaji cha YMC cha mjini Singida, kikitoa burudani ya sarakasi kwenye mkutano wa hadhara  uliofanyika katika viwanja vya  Mandewa mjini Singida kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha wanaume kushiriki masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.

Binti wa kazi ajeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa uji wa moto na mke wa bosi wake, kisa wivu wa kimapenzi.

Msichana Jackline Lasway akiwa amelazwa katika wodi ya kina mama namba mbili katika hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kujeruhiwa kwa kumwagiwa uji wa moto wakati akiwa dukani kwa bosi wake eneo la soko kuu Manispaa ya Singida.
 Waandishi wa habari wakimchukua maelezo msichana huyo.
 Msichana Jackline akilia wakati akiwaonesha waandishi wa habari jeraha alilomwagiwa uji na mke wa bosi wake.