Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela.
WATU wawili mkoani Singida wamefariki dunia katika matukio tofauti, likiwemo la Mwalimu wa shule ya msingi Kigogo jijini Dar-es-salaam, Hawa Idd (34) baada ya kuchomwa kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na mdogo wake Ramadhan Iddi (24) anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela alisema tukio hilo limetokea Septemba 23 mwaka huu saa 9.30 alasiri huko katika hospitali ya mkoa mjini Singida.
Alisema Septemba 22 mwaka huu saa 5.30 asubuhi kijana Ramadhan ilidaiwa alitoka nyumbani kwao kwa mazingira ya kutatanisha na ndipo mwalimu Hawa ambaye alikuja kwa ajili ya kushughulikia matatizo ya mdogo wake huyo,walianza msako wa kumtafuta katika maeneo mbalimbali mjini Singida.
“Baada ya kumtafuta katika mitaa mbalimbali hapa mjini na kumkosa, Hawa alirejea nyumbani kwao Kibaoni na kumkuta mdogo wake Ramadhan,ameisha rejea nyumbani. Haikuchukua muda wanandugu hao walianza

















