Tuesday, January 13, 2015

Baadhi ya wabunge mkoa wa Singida wapumulia mashine kwenye nafasi zao majimboni.

Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Mh. John Chiligati pamoja na Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Dewji wakipungia mikono wakazi wa Singida wakati wa mikutano ya chama cha Mapinduzi mkoani humo.


                                                      JIMBO LA MKALAMA.

Hili kwa sasa linafananishwa na ‘mzoga’ kwa madai hadi sasa kuna dalili ya watu 12 wanaonyesha dalili la kuliwania jimbo hilo ambalo zamani lilikuwa likijulikana kwa jina la Iramba mashariki.

Mbunge wa sasa Salome Mwambu wa CCM ambaye anamaliza kipindi chake cha kwanza mwakani,anatarajiwa kutetea nafasi yake hiyo.Hata hivyo anatarajiwa kupata upinzani mkubwa kutoka kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa sasa na mbunge wa zamani wa jimbo la Iramba mashariki,Mgana Msindai.


Baadhi ya watu wengine waliojitokeza ni pamoja na Alan Mkumbo wa TRA makao makuu,Dc wa wilaya ya Nchemba,Francis Izack,Emmanule Mkumbo,mkandarasi Nakei na Emmanuel Mbasha.Hii ni
orodha fupi tu ya watu wanaoliwania jimbo hilo linalopakana na mkoa wa Manyara.


 Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi na Naibu Waziri wa Fedha Mwigullu Lameck Nchemba.


JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI.

Jimbo hili ambalo kwa sasa Naibu Waziri Wa Fedha Mwigullu Lameck Nchemba,ndiye mbunge anayemaliza kipindi chake cha kwanza mwakani, Inadaiwa jimbo hilo lina kawaida ya kuwakilishwa kipindi kimoja tu (miaka 5) na wapiga kura wanabadilisha mwakilishi mwingine.

Kwa sasa licha ya Mwigullu kuonyesha dalili ya kutetea nafasi yake hiyo na pia kuna minong’ong’o kuwa atagombea nafasi ya urais, anakabiliana na upinzani kutoka wabunge wa viti maalum wawili wa mkoa huu (CCM) ,wanatajwa kulimezea mate jimbo hilo.Pia yupo ndugu moja ametambulika kwa jina moja, Nkurlu, Profesa Kitila Mkumbo ambaye kwa sasa hana chama na Juma Kilimba aliyewahi kuwa mbunge kabla ya kuangushwa na Mwigullu.

JIMBO LA SINGIDA MAGHARIBI.

Jimbo hili kwa sasa linashikiliwa na Mohammed Missanga wa CCM kwa vipindi vitatu. Jimbo hili ambalo limemegwa sehemu na CHADEMA,ninawaniwa na Missanga mwenyewe kwa lengo la kuweka rekodi ya kuliwakilisha kwa miaka 20 (vipindi vinne).

Pia wapo wanaCCM ambao kwa sasa wanapiga jaramba la kumwangusha Missanga ambao ni pamoja na Eliwaja Mtinda (mbunge viti maalum CHADEMA),wanatajwa vile vile wakuu wawili wa wilaya akiwemo Khambako wa wilaya ya Kishampu mkoa wa ShinyangaLissu Mahanju na daktari wa binadamu ambaye jina lake halijaweza kupatikana mara moja.


Mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, John Paulo Lwanji.


JIMBO LA SINGIDA MJINI.

Jimbo hili ambalo makao makuu ya mkoa yalipo, kwa vipindi vitatu sasa linawakilishwa vema na Mohammed Gullam Dewji (44).

Hata hivyo,Dewji inadaiwa anakabiliwa na upinzani wa karibu kutoka kwa mwana CCM mwenzake katibu mwenezi CCM mkoa na mwalimu wa shule ya msingi, Mussa .Pia mwandishi wa habari, Josephat Isango na  ndugu yake na mbunge wa jimbo la Singida mashariki kupitia CHADEMA,Tundu,Vicent Mughwai wote wa CHADEMA,wapo kwenye maandalizi makali lengo likiwa ni kuing’oa CCM katika jimbo la Singida mjini.

JIMBO LA MANYONI MASHARIKI.

Jimbo hili kwa kindi kirefu,linashikiliwa na John Chiligati wa CCM.Anatajwa mwanaCCM mmoja amabye ametambulika kwa jina moja la Mtuka,ameonyesha kila dalili ya kumg’oa Chiligati.Pia yupo afisa mwanadamizi wa benki moja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja,kuwa naye analitaka kwa udi na uvumba jimbo hilo kupitia tiketi ya CHADEMA.

JIMBO LA MANYONI MAGHARIBI.

John Paulo Lwanji,ni mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM kwa vipindi vitatu sasa.Lwanji ambaye ni mmoja wa watoto wa hayati mzee Lwanji ambaye katika uhai wake aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo,anatajwa kuwa ataitetea nafasi yake hiyo kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.Inadaiwa anataka kuhakikisha ndoto yake ya jimbo hilo kupandishwa hadhi na kuwa wilaya,inatimia.

Kwa sasa bado hawajajulikana watu wengine wanaolitaka jimbo hilo lenye hifadhi ya wanyama pori la Rungwa.Hata hivyo,uwezekano wa CHADEMA kuweka mtu wake,ni asilimia mia moja kwa madai kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2010,kilifanya vizuri katika nafasi hiyo ya ubunge.

No comments:

Post a Comment