Wednesday, February 5, 2014

Shirika lisilo la Kiserikali latumia zaidi ya shilingi 562 milioni kugharamia sekta ya maji na usafi wa mazingira

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Association (HAPA) la mjini Singida, David Mkanje, akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Health Action Promotion Association (HAPA) la mkoani hapa limetumia zaidi ya shilingi 562 milioni kugharamia sekta ya maji na usafi wa mazingira katika mkoa wa Singida na Morogoro.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na mkurugenzi wa HAPA,David Mnkaje wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi katika kipindi cha kuanzia januari hadi desemba mwaka jana.

Amesema kati ya fedha hizo,zimetumika kwenye ujenzi wa vyoo bora na vya kisasa katika shule za msingi tano wilayani Iramba.Shule hizo zilizonufaika na mradi huo ni Dominiki,Midimbwi,Munguli,Nyahaa na Lugongo.

Aidha,Mnkeje amesema kupitia projecti ya WFP,wamejenga matenki 48 ya kuvunia maji ya mvua katika baadhi ya shule za msingi zilizopo wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga,Kondoa (Dodoma),Iramba,Singida vijijini na Ikungi zote za mkoa wa Singida.

“Pia katika mwaka uliopita,tumeweza kujenga zahanati na kusaidia baadhi ya vitendea kazi katika vijiji vya Kinampundu na Milade vya wilaya ya Mkalama.Kazi hii ya kujivunia,tumesaidina na vijana wa kujitolea (volunteers) kutoka nje ya nchi (ulaya) na wakazi wa vijiji husika”,amesema Mnkeje kwa kujiamini.

Katika hatua nyingine,Mkurugenzi huyo amesema kupitia project nyingine iliyofadhiliwa na Care,alisema kujenga vyoo bora kabisa katika shule za msingi za Mkundi,Chaumbele na Madege vya wilaya ya Mvomero katika mkoa wa Morogoro.Shule hizo pia zilijengewa matanki ya kuvunia maji ya mvua.

“Kwa mkoa wa Morogoro,kupitia mradi mwingine wa WADA,tumeweza kujenga
vyoo vya kisasa na huduma ya maji katika vijiji vya Mtamba,Duthumi,Kisaki gomero na Kisaki station katika wilaya ya Morogoro vijijini”,amesema Mkurugenzi huyo.


Mkanje ametumia fursa hiyo,kuwahimiza walengwa wa miradi hiyo,kwamba waitunze vizuri ili iweze kutumika kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment