Saturday, January 10, 2015

Baba mzazi wa Nyalandu afagilia mwanae kutaka Urais.

Baba yake Waziri wa Maliasili na Utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini,(Lazaro Samwel Nyalandu), mzee Samwel Nyalandu akizungumzia uamuzi wa mtotowake  Lazaro kuwania urasi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani. Amedai amepokea uamuzi huo kwa mikono miwili akiamini kuwa Lazaro atamudu nafasi hiyo nyeti ya urais.
Waziri wa Maliasili na Utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini,Lazaro Nyalandu, akitangaza rasmi kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

BABA mzazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini, Samwel Nyalandu (70), alisema amepokea kwa mikono miwili kusudio la mtoto wake kuwania nafasi nyeti ya urais, kwa madai kwamba anao uwezo wa kumudu nafasi hiyo.

Amemwasa kwamba endapo atafanikiwa kupata nafasi hiyo na kuwa mkazi wa Singida wa kwanza kuwa rais, ahakikishe anafuata nyayo za watangulizi wake.

“Pia namwomba akifanikiwa aje kuwa karibu zaidi na wananchi. Sikio lake liwe jepesi kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi atakaokuwa akiwaongoza au kuwatumikia.

Akifafanua zaidi,mzee Samwel alisema kuwa Lazaro alianza kuonyesha kuwa mbele ya safari ya maisha yake atakuwa kiongozi wa watu kwani alipokuwa mtoto mdogo, alikuwa anapenda kukusanya wenzake na kuanza kuwaongoza katika mambo mengi ikiwemo michezo.

Alisema pia alipokuwa shule ya msingi kijiji cha Pohama, alikuwa akiongoza kuanzia darasa la kwanza hadi anamaliza darasa la saba na kuwa mwanafunzi pekee
kufaulu mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi.


Mzee Samweli alisema kuwa alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya wanafunzi wenye vipaji maalum ya Kibaha, baadaye Eliboru kidato cha tano na sita na amesoma chuo kikuu nchini Marekani.

Katika hatua nyingine,Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Singida, kimekanusha vikali kwamba vijiji nane vilivyochukuliwa na upinzani  kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji kati ya 84 vya wilaya hiyo,kushindwa huko kumechangiwa kwa kiwango kikumbwa na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini,Lazaro Nyalandu.

Chama hicho tawala,kimesema kimepta ushindi wa kujivunia wa asilimia 91.9 kwenye uchaguzi huo wa serikali za mitaa,hivyo ni jambo la kipuuzi kwa mtu/kundi la watu kumnyooshea kidole kiongozi au mwanachama ye yote kuwa amechangia vijiji hivyo nane kuchukulia na upande wa upinzani.

Akifafanua zaidi,mwenyekiti wa CCM katika wilaya hiyo, Narumba Haje, alisema CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika katikati ya  mwezi huu, CCM imeshinda katika vijiji 76,CHADEMA ,8.Vitongoji CCM 386,Chadema 41, CUF 7 na TLP kimoja.

Alisema katika nafasi za wajumbe wa halmashauri za vijiji na kundi la jumla,CCM imenyakua nafasi 921 kati ya nafasi 1,000 na nafasi za wajumbe wa viti maalum544 kati ya wajumbe 574.

“CHADEMA kundi la jumla wajumbe 71 sawa na aslimia 7.1 na viti maalumu nafasi 28 sawa na asilimia 4.8.CUF kundi la jumla nafasi 7 sawa na asilimai 0.7 na viti maalumu nafasi 2 sawa na aslimia 0.3,NCCR Mageuzi kundi la jumla nafasi moja sawa na aslimia 0.1 na viti maalumu 0. sawa na asilimia 0.Wakati UDP kundi la jumla nafasi moja sawa na asilimia 0.1 na TLP haikuambulia nafasi ya wajumbe wa halmashauri haikuambulia nafasi za wajumbe wa halmashauri za vijiji”,alisema kwa kujiamini Hanje.

Mwenyekiti huyo alisema kwa ushindi huo mkubwa,hapakuwa na sababu yo yote kwa mtu,kiongozi au kundi la watu kuanza kunyooshea kidole kiongozi/mwanancha ye yote kuwa kasababisha wilaya hiyo kupoteza vijiji nane tu.

Wakati huo huo,Mwenyekiti Hanje,aliwavunja mbavu mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo uliovunja rekodi ya kuhudhuriwa na watu wengi,baada ya kutambulisha wageni mbalimbali na kumalizia  kwa kumtambulisha askofu wa dhehebu la Wapangani na diwani wa CCM kata ya Ikhanoda,Mnyawi Higa.


Mkutano huo wa hadhara ulihudhuriwa na mamia ya wananchi kutoka katika jimbo la Singida kaskazini na ulipambwa na vikundi mbalimbali vya burudani. Walikuwemo waimbaji mahiri wa nyimbo za injili nchini  akina Rose Muhando na Christina Shusho.

No comments:

Post a Comment