Mahakama kuu Kanda ya Dodoma inaendelea na vikao vyake mjini Singida, imemwachia huru kijana Elikana Selemani (28) mkazi wa kijiji cha Sefunga wilaya ya Singida vijijini, baada ya kukiri kosa la kumuuwa Omari Muna bila kukusudia.
Imedaiwa kuwa Elikana alitenda kosa hilo la mauaji, wakati akimuokoa mama yake mzazi asibakwe na kina Omari Muna.
Mapema mwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Masanja, alidai mbele ya Jaji Rehema Mkuye, kuwa mnamo Januari 31 mwaka jana saa 4:00 asubuhi huko katika kijiji cha Sefunga wilaya ya Singida vijijini, mshitakiwa Elikana alimpiga fimbo moja kichwani Omari Muna na kusababisha kifo chake baada ya siku mbili.
Masanja alisema siku ya tukio, mshtakiwa Elikana akiwa nyumbani kwao, alisikia yowe kutoka kwa mama yake mzazi akiomba msaada kutoka ndani ya shamba lao la mahindi.
Alisema Elikana akiwa amebeba fimbo, alipofika eneo la tukio, alishuhudia Omari Muna, akiwa amemlalia juu mama yake........