Saturday, August 24, 2013

Mapato katika halmashauri ya Singida yaporomoka kwa sababu mbalimbali ikiwemo bodaboda kugomea ushuru.

 Makamu Meya wa manispaa ya Singida na Diwani wa kata ya Mungumaji Bw. Hassan Mkata (kushoto) akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani.Kulia ni kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida.
 Diwani wa kata ya Misuna manispaa ya Singida, Hamisi Kisuke akichangia mada wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa manispaa ya Singida kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi mjini Singida.
Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Singida wakifuatilia kwa makini kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi mjini.

Makusanyo ya mapato ya baadhi ya vyanzo vya mapato vya halmashauri ya manispaa ya Singida, yameporomoka kutokana na sababu mbalimbali na kusababisha manispaa hiyo kushindwa kufikia malengo yake.

Imedaiwa katika vyanzo hivyo vilivyoporomoka kwa makusanyo ya mapato, manispaa ilijiwekea lengo la kukusanya mapato ya zaidi ya shilingi milioni 797.5 kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013, lakini hadi Februari mwaka huu, ilikuwa imekusanya zaidi ya shilingi milioni 217.6 tu.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meya wa manispaa ya Singida Hassan Mkata, mbele ya kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Singida.

 Ametaja baadhi ya vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na ushuru wa pikipiki (bodaboda) ambao lengo lilikuwa ni kukusanya shilingi milioni 24, lakini zilizokusanywa ni shilingi 235,000 sawa na asilimia moja ya lengo.

Amesema  “Wamiliki wa bodaboda wamegoma kulipa ushuru huo. Magogoro huu umewasilishwa mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Singida na ofisi ya mkurugenzi inafuatilia ili kupata muafaka juu ya suala hili”.

Mkata ametaja chanzo kingine ni cha kodi ya thamani ya majengo ambacho kilikuwa kiipatie manispaa zaidi ya shilingi milioni 118.8, lakini zilizokusanywa ni zaidei ya shilingi milioni 22.3 sawa na aslimia 19 tu,

Amesema sababu iliyosababisha kuporomoka kwa kodi ya thamani ya majengo ni mwamko  mdogo wa wananchi kulipa kodi za majengo kwa hiari.

Mkata amesema “Tulijipangia kukusanya zaidi ya shilingi
milioni 18 ikiwa ni lengo kutoka  kwenye ushuru wa mchanga katika kipindi hicho, lakini tumekusanya shilingi 1,302,000 sawa na aslimia saba tu ya lengo”.


 Mkata ametaja sababu ya kuporomoka kwa mapato ya ushuru huo wa mchanga ni migogoro iliyopo kati ya halmashauri na serikali za vijiji/mtaa husika ambapo kuna chanzo cha mchanga.

No comments:

Post a Comment