Wednesday, December 11, 2013

Unyanyapaa bado ni tatizo mkoani Singida.

Meneja mradi wa Global Fund uliopo chini ya AMREF Tanzania, Andulile Kanza, akitoa maelezo juu ya mradi wao wa uhamasiahaji wa upimaji wa afya wenye lengo la ifikapo mwaka 2015 maambukizi mpya ya Virusi vinavyosababisha UKIMWI,kiwango kifikie 0, vifo vitokanavyo na UKIMWI, 0 na unyanyampaa ufikie kiwango cha 0. Andulile alikuwa akitoa maelezo hayo  kwenye kituo kikuu cha mabasi mjini Singida.
Mkazi wa Singida mjini, akishikiriki kupima Afya yake kwenye zoezi lililokuwa likiendeshwa na shirika la AMREF lililofanyika katika kituo kikuu cha mabasi mjini Singida.
Mwanakikundi maarufu cha ‘Mtaa wa saba’ cha Majengo mjini Singida, akitoa burudani katika hafla ya zoezi la upimaji wa afya lililoendeshwa na AMREF kwenye kituo cha mabasi cha mjini Singida.
Kikundi cha sarakasi kutoka jijini Dar-es-salaam, kikitoa burudani wakati wa kampeni ya uhamasishaji upimaji wa afya iliyokuwa ikiendeshwa na shirika la AMREF katika kituo cha mabasi mjini Singida.

UNYANYAPAA na woga wa baadhi ya watu unachangia watu wengi zaidi kupima afya zao nyakati za usiku wakati wa kampeni za upimaji afya zinazofanyika nyakati hizo, imeelezwa.

 Hayo yamesemwa na Meneja Mradi wa Global Fund uliopo chini ya AMREF Tanzania, Andulile Kanza, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kauli mbiu ya ‘Getting zero’ katika masuala ya UKIMWI.

 Amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakiogopa kupima afya zao asubuhi au mchana kwa hofu kwamba watu watawaona na hivyo wataanza kuwanyanyapaa na kuwatenga.

 “Ndio maana sisi AMREF kwenye kampeni hii ya kuhakikisha Tanzania ifikapo 2015, kiwango cha maambukizi mapya ya Ukimwi kitakuwa sifuri vifo vitokanavyo na ukimwi vitafikia sifuri  tunapima afya hadi saa tatu usiku na malengo yetu yanaenda vizuri”,alifafanua Andulile.

 Katika hatua nyingine, Maria Edward aliyepima afya yake baada ya kuhamasishwa na AMREF, ametoa wito kwamba  watu na hasa wanawake wajitokeze kwa wingi kupima afya zao ili waweze kujitambua endapo wameambukizwa au laa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI.

“Natoa wito kwa wanawake wenzangu kwanza waelewe kwamba baadhi ya wanaume wetu wana mitandao ya ngono tofauti na wanawake Hivyo tunalazimika kupima afya zetu mara kwa mara ili kujua kama tumeathirika au la”,amesema.

 Amesema faida ya kutambua afya yako zipo nyingi ikiwemo endapo utagundulika una maambukizi uweze kupata ushauri nasaha utakaokuwezesha kuishi maisha marefu.


 Kwa upande wake Bakari Ramadhani, amesema kazi yake ya kusafiri sehemu nyingi hapa Tanzania , imechangia awe na  mtandao mingi ya hatari ya ngono lakini baada ya kupima na kugundulika
hana maambukizi ya VVU sasa atavunja mitandao ya ngono na atajilinda zaidi.

No comments:

Post a Comment