Wednesday, December 18, 2013

Wilaya ya Ikungi kuvuna tani 144,826 ya mazao ya chakula.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Bw.Protace Magayaye, akitoa taarifa yake kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha)  ya utekelezaji wa shughuli za kilimo msimu wa 2013/2014 ambapo wanatarajia kuvuna tani 144,826 mazao ya chakula na hivyo kuwa na ziada tani 83,090.Mahitaji ya wakazi wa wilaya hiyo 225,521,ni tani 61,736 kwa mwaka.
Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Ayubu Sengo.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida inatarajia kulima hekta 84,014 za mazao ya chakula msimu huu wa 2013/2014 na wanatarajia kuvuna tani 144,826.

Halmashauri hiyo ya Ikungi yenye jumla ya wakazi 225,521 ambao mahitaji yao ya chakula kwa mwaka ni tani 61,736, kwa matarajio ya mavuno ya msimu huu ya tani 144,826, halmashauri hiyo mpya itakuwa na ziada ya tani 83,090 ya mazao ya chakula.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Protace Magayane wakati akitoa taarifa yake ya utekelezaji wa shughuli za kilimo msimu wa 2013/2014.

Alitaja mazao hayo na hekta zake kwenye mabano kuwa ni mtama (34,498), uwele (35,629), mounga (3,012), mhogo (1,500) na viazi vitamu (4,500).

Magayane alitaja mazao mengine ya chakula kuwa ni maharage (2,875), kunde (1,500) na njugumawe (500).

Mkurugenzi huyo amesema mafaniko hayo yatatokana na upatikanaji wa mvua yenye mtawanyiko mzuri kanuni bora za kilimo ikiwemo matumizi ya mbolea na mbegu bora.

Kwa upande wa mazao ya biashara, Magayane amesema wamejiwekea lengo la kulima hekta 22,097 na matarajio ni kuvuna tani 45,431.3.


Wakati huo huo, Mkurugenzi huyo, amesema wamesambaza
pembejeo za hati punguzo kilo 14,228 za mbegu ya pamba aina ya UK.MO8 kwenye maeneo yanayolima zao la pamba.

No comments:

Post a Comment