Sunday, December 1, 2013

Wakulima Singida wahimizwa kulima Mihogo.

Diwani wa kata ya Ikungi wilaya ya Ikungi, Haji Mukhandi akitoa nasaha zake kwenye mkutano wa uchaguzi wa kamati ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko uliofanyika kwenye viwanja wa shule hiyo kongwe iliyojengwa mwaka 1944.Wa kwanza kulia waliokaa,ni mwalimu mkuu wa shule hiyo,Olivary Kamilly na anayefuata ni mwenyekiti wa kamati ya shule inayomaliza muda wake, Naftali Gukwi.
Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko anayemaliza muda wake, Naftali Gukwi (ata tetea nafasi yake hiyo), akifungua mkutano wa uchaguzi wa kamati ya shule hiyo uliyofanyika shuleni hapo.Wa kwanza kulia ni mwalimu mkuu Olivarry Kamilly na kushoto ni diwani wa kata ya Ikungi, Haji Mukhandi.
Baadhi ya wazazi/walezi wakipiga kura kuchangua kamati ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi katika uchaguzi uliofanyika shuleni hapo.
Baadhi ya wazazi/walezi wakifutatlia kwa makini mkutano wa uchaguzi wa kamati ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko.

DIWANI (CCM) Kata ya Ikungi wilayani Ikungi Haji Mukhandi amewaagiza wakulima kulima mashamba ya kutosha ya muhogo, ili pamoja na mambo mengine, kupunguza makali ya uhaba wa chakula.

 Haji ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye mkutano wa uchaguzi wa kamati ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko, uliofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo iliyojengwa mwaka 1944.

Amesema zao la muhogo ni zao ambalo limepewa kipaumbele na mkoa kwa vile linastahimili ukame na ni kwa ajili ya kinga ya njaa.

 Aidha, amesema zao la muhogo lina soko kubwa kutokana na matumizi yake ambayo ni pamoja na kuliwa kama ugali, vitafunwa mbalimbali na majani yake hutengenezwa mboga (Kisamvu).

 “Matumizi mengine ni kutengeneza vinywaji vya aina ya togwa na pombe. Viwandani muhogo hutumika kutengeneza biskuti, wanga na huchanganywa na mazo mengine kupata chakula cha mifugo”,alifafanua zaidi diwani huyo.

 Amesema kutokana na matumizi hayo, muhogo una soko kubwa ambalo lina mkubwa wa kumwezesha mkulima kuinua kipato chake.

 Mkutano huo wa uchaguzi uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Kamati inayemaliza muda wake,Naftal Gukwi, ulimchagua mwalimu mstaafu Rashidi Msaru kutoka kijiji cha Ikungi kuwa mjumbe wa kamati ya shule hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia januari mwakani.

 Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Olivary Kamilly, Msaru anaugana na wajumbe wengine  waliochaguliwa kutoka vijiji vya Muungano na Mbwajiki, ambao ni Selemani Ng’amo na Yoel Isingo.

 Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Hamisi Mdachi, Mwajuma Sambe na Deodatus Mtaturu ambao wamechaguliwa na serikali ya kijiji cha Ikungi.

 “Pia kwenye kamati hiyo watakuwepo
walimu Pili Mpinga, Stephano Nyangi na mimi menyewe (Kamilly) nitaingia kwa wadhifa wangu, na nitakuwa katibu kwa mujibu wa sheria”,amesema Mwalimu Kamilly.


 Aidha, mwalimu mkuu huyo, amesema Dk. Mariam Nkumbi wa taasisi ya pembejeo jijini Dar es salaam, amechaguliwa kwa kishindo kuwa melezi wa shule hiyo kongwe wilayani Ikungi.

No comments:

Post a Comment