Friday, November 28, 2014

DC aagiza watendaji kujiunga CHF kuvutia wananchi.

Kaimu meneja mfuko wa taifa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Singida, Adamu Salum,akizungumza siku ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi wa kijiji cha Simbanguru wilayani Manyoni kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF),juzi.Amedai kwamba ugonjwa haubagui wala hautoi taarifa ya ujio wake,hivyo kujiweka upande salama,ni kujiunga na mifuko ya afya ukiwemo wa CHF.
Mganga mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida,Dk.Raphael Hangai,akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) uliofanyika katika kijiji cha Simbangurum, ili waweze kujijengea mazingira ya kupata matibabu wakati wote hata ule wasiokuwa na fedha.

CHADEMA walia kuchezewa rafu Singida Kaskazini.


Mjumbe wa kamati ya utendaji CHADEMA jimbo la Singida kaskazini,Theodory Hango,(kulia anayeangalia kamera) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya CHADEMA kulaani vikali ukiukwaji wa kanuni na taratibu za uendeshaji wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaoendelea nchini kote.Hango amedai CCM wameanza mchezo mbaya dhidi ya CHADEMA  ikiwa ni pamoja na kukaa kutoa fomu kwa waombaji uongozi kutoka CHADEMA,hadi waonyeshe stakabadhi za kulipa michango ya ujenzi wa maabara. Kulia ni mwenyekiti Elia Sima,mwenyekiti wa jimbo la Singida kaskazini.

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) jimbo la Singida kaskazini,kimeanza kulia kuchezewa mchezo mchafu na CCM kwenye mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaoendelea nchini kote.

CHADEMA kimedai kwamba baadhi ya waombaji wa nafasi mbalimbali za uongozi katika serikali za mitaa,wananyimwa fomu hadi waonyeshe stakabadhi ya kulipa michango ya ujenzi wa maabara.

Chama hicho ambacho kimejisifu kwamba kwa sasa ni mwiba mkali kwa CCM jimbo la Singida kaskazini,kimedai CCM kimeanza kutoa rushwa kwa baadhi ya waombaji wa CHADEMA,ili

Wednesday, November 26, 2014

TRA Singida wakusanya bilioni 4.14/-

Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mlipa kodi mkoa wa Singida yaliyofanyika kwenye stand ya askofu Mabulla mjini Singida.Wa kwanza kulia ni kaimu meneja wa TRA mkoa wa Singida, Samwel Shula na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.
Kaimu meneja wa TRA mkoa wa Singida, Samwel Shula, akitoa taarifa yake kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mlipa kodi mkoa wa Singida.Maadhimisho hayo yamefanyika kwenye stand ya askofu Mabula mjini Singida.Wa pili kulia (waliokaa) mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,anayefuata ni mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mlozi na katibu tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan.

Mazingira yasiyo rafiki yakwamisha masomo mabinti wanaobalehe.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda,akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani, matumizi ya vyoo bora duniani na usafi wa mazingira kwa mkoa wa Singida.Maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha Mgongo kata Shelui wilaya ya Iramba.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda,akimpongeza meneja wa shirika la SEMA, Ivo Manyanku (aliyekaa) kwa kazi nzuri ya kuhamasisha wananchi wa wilaya ya Iramba kujenga vyoo bora na kuvitumia.

Tuesday, November 25, 2014

Basi la kampuni ya Hajis lanusurika kuteketea kwa moto!




23 washikiliwa na Polisi kwa mauaji ya watu 4.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobias Sedoyeka.

JESHI la polisi mkoa wa Singida, linawashikilia watu 23 wakazi  wa kijiji cha Nkyala kata ya shelui wilaya Iramba mkoa wa Singida, kwa tuhuma ya kudaiwa kuuawa kwa makusudi wezi wanne wa madume ya Ng’ombe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobias Sedoyeka, alisema watu hao kati yao 21 wanatuhumiwa kwa mauaji na wawili wanatuhumiwa kuiba ng’ombe watatu.

Aliwataja watu hao waliouawa kwa tuhuma ya wizi wa madume matatu ya ng’ombe ni Magupa Ngelela (32), Hemedi Masasi (29), wote wawili ni wakazi wa kijiji cha Nkyala.Wengine ni Saidi Hamisi (32) mkazi wa kijiji cha Kinkungu na Didas Mwigulu (36) mkazi wa kijiji cha Mgongo.

Akifafanua,alisema novemba 19 mwaka huu saa saba usiku,watu hao wanne kwa pamoja inadaiwa

Singida wajipanga kufanikisha uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mkurugenzi wa manispaa ya Singida, Joseph Mchina, akitangaza ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka huu,mbele ya waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi wa habari mjini Singida, wakimsikiliza mkurugenzi wa manispaa ya Singida, Joseph Mchina (hayupo pichani) wakati akitangaza ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa ulioanza Novemba 16 mwaka huu.

Round about ya manispaa ya Singida iliyopo barabara kuu ya Singida-Mwanza eneo la Peoples klabu.

HALMASHAURI  ya manispaa ya Singida,imejipanga vema kwa ajili ya kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa 2014, unakuwa huru,haki  na wa amani.

Hayo yamesemwa na msimamizi wa uchaguzi wa manispaa hiyo, Joseph Mchina, wakati akitangaza ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu mbele ya waandishi wa habari.

Mchina ambaye ni Mkurugenzi wa manispaa ya Singida,alisema nafasi zitakazogombewa ni pamoja na uenyekiti wa mtaa/kijiji,ujumbe wa kamati ya mtaa, ujumbe wa halmashauri ya kijiji na uenyekiti wa kitongoji.

Alisema fomu zilianza kuchukuliwa na kurejeshwa  juzi (16/11/2014) na mwisho wa zoezi hilo ni novemba 23 mwaka huu saa 10.00 jioni.


“Fomu zitaanza kuchukuliwa kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa 10.00 jioni kutoka

Auawa na kuchomwa moto kwa tuhuma za ujambazi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobias Sedoyeka, akitoa taarifa ya wananchi kumuua kijana Hussein Jumanne Kisuke (31) anayedaiwa kuwa ni jambazi sugu. Baada ya kumshambuliwa kwa silaha za jadi na kufariki dunia na kisha kumchoma moto.

Mtuhumiwa wa Ujambazi mkazi wa Misuna Hussein Jumanne Kisuke (31) juzi  alipigwa na wananchi wa Misuna mjini Singida kwa kutumia silaha za jadi na kuuwawa na kisha kuchomwa moto.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobias Sedoyeka, alisema tukio hilo limetokea juzi saa 5.15 asubuhi huko katika maeneo ya Kipungua kata ya Misuna tarafa ya Mungumaji manispaa ya Singida.

Alisema Kisuke alikuwa akitafutwa muda mrefu kuhusiana na tuhuma mbalimbali za ujambazi na wizi wa pikipiki.

“Kwa ujumla Hussein Kisuke  alikuwa mzoefu wa matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha katika mji wa Singida. Siku ya tukio wananchi walimuona akipita katika maeneo ya Kipungua na hivyo

Wadau waliohudhuria kongamano la Nyuki mjini Arusha, watembelea shamba la darasa la Nyuki wilayani Ikungi.

Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Nyuki Gladness Mkanda,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mahambe wilaya ya Ikungi muda mfupi baada ya kuongoza wadau wa nyuki kutoka sehemu mbalimbali duniani,kutembelea shamba darasa la ufugaji bora wa nyuki linalomilikiwa na shirika la Future Development Initiatives (Fu-DI).Mkamba alitoa wito kwa wananchi kujiunga katika vikundi vya ufugaji Nyuki ili waweze kujikomboa kiuchumi.
Meneja wa shirika la Future Development Initiatives (Fu-DI), Jonathani Njau, akitoa ufafanuzi juu ya uendeshaji wa shamba darasa la ufugaji nyuki kisasa, kwa mmoja wa wadau wa Nyuki waliohudhuria kongamano la Nyuki duniani lililofanyika mjini Arusha hivi karibuni.
Baadhi ya wadau wa nyuki kutoka sehemu mbalimbali duniani,wakipiga picha mizinga ya nyuki iliyopo kwenye shamba darasa la ufugaji Nyuki kisasa katika kijiji cha Mahambe wilaya ya Ikungi.

Thursday, November 20, 2014

Serikali kutoajiri wahitimu wa vyuo visivyosajiliwa.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma,Celina Kombani, akizungumza kwenye mahafali ya 20 ya chuo cha uhazili Tanzania mjini Singida. Kombani aliwaasa wahitimu hao 4,960, kwamba wasiridhike na elimu waliyopata, bali waongeze bidii zaidi katika kujiendeleza.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi, akizungumza kwenye mahafali ya 20 ya chuo cha uhazili Tanzania yaliyofanyika mjini Singida. Jumla ya wahitimu 4,960 walitunukiwa vyeti vya fani mbalimbali.

Serikali yaonya ubadhilifu wa wahitimu.

Wahitimu 1,808 wa fani mbalimbali wa vyuo vya uhasibu tawi la Mwanza na Singida, wakiwa kwenye maandamano ikiwa ni sehemu ya mahafali yao ya 12 yaliyofanyika mjini Singida.

Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Mwigullu Lameck Nchemba, akizungumza kwenye mahafali ya 12 ya tawi la Mwanza na Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha uhasibu mjini Singida. Mwigulu aliwaasa wahitimu hao waweke mbele uadilifu,uaminifu na kuchapa kazi kwa bidii na maarifa ili kujijengea mazingira ya kuaminika mbele ya jamii.

Katibu tawala Singida ataka mikakati kuwekwa kuongeza wakulima wanaotumia mbegu bora.

Katibu Tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan, akizungumza kwenye ufunguzi wa semina juu ya kuongeza upatikanaji wa mbegu bora na mbolea kwa wakulima wadogo wadogo kwa kuimarisha masoko ya pembejeo katika mikoa ya Singida na Dodoma.
Baadhi ya wakulima wadogo wadogo mkoa wa Singida na Dodoma,wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina ya siku mbili iliyohusu kuongeza upatikanaji wa mbegu bora na mbolea.

Agizo la kukabidhi vyumba vya maabara kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida bado kutekelezwa.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari kata ya Ikungi wilayani Ikungi mkoa wa Singida,wakishiriki ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara jana kama walivyokutwa na mpiga picha wetu. Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone, aliagiza akabidhiwe vyumba vitatu vya maabara kwa kila shule ya sekondari 153 za kata za mkoa huo kabla ya oktoba 15 mwaka huu.Mambo yamekuwa tofauti kwa shule ya sekondari ya kata ya Ikungi ambayo hadi sasa bado ujenzi upo ngazi ya msingi.

135 wafa katika ajali Singida.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobias Sedoyeka ,akitoa taarifa ya utendaji kazi mkoani Singida kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu.

Baadhi ya waandishi wa habari na askari polisi waliohudhuria hafla ya kamanda wa polisi mkoa wa Singida kwa ajili ya kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi tisa.

Halmashauri ya Ikungi yakusanya zaidi ya shilingi billion 2 ndani ya miezi 3 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Celestine Yunde, akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani.Kulia ni makwamu mwenyekiti, Ali Mwanga na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi,Hassan Tanti na anayefuatia ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri wilaya Ikungi, Mahammud Nkya.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Mahammud Nkya, akitoa taarifa yake mbele ya kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika Ikungi. Kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Ikungi, Celestine Yunde na kushoto ni mwenyekiti CCM wilaya ya Ikungi, HassanTanti.

Picha za tukio la kuuwawa kwa Fisi mjini Singida ziko hapa!

Baadhi ya askari polisi wakishiriki kumtoa Fisi ambaye alikuwa amejificha ndani ya duka la mitumba mjini Singida.
Baadhi ya wananchi wa mji wa Singida wakishuhudia kutolewa nje Fisi aliyekuwa amejificha ndani ya duka la mitumba mjini Singida.

Tuesday, November 11, 2014

Wazalishaji wadogo wahimizwa ubora katika bidhaa zao.

Mwakilishi wa mkurungezi wa usala wa chakula (TFDA), Lazaro Mwambole, akitoa taarifa yake muda mfupi kabla hajamkaribisha mgeni rasmi Katibu Tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan kufungua mafunzo ya siku mbili yaliyohudhuriwa na wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Singida.Wa pili kulia (waliokaa) Katibu Tawala mkoa wa Singida Liana Hassan na Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk, Doroth Gwajima (wa pili kulia).
Katibu Tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyohudhuriwa na wasindikaji wadogo mkoani Singida.Mafunzo hayo yalihusu usindikaji wa vyakula unaozingatia ubora na usalama wa chakula.Kulia ni mganga mkuu wa mkoa, Dk.Doroth Gwajima na kushoto ni Mwenyekiti wa wasindikaji wadogo mkoa wa Singida, Kisenge.

Rais aagiza kufunguliwa kwa mgodi wa dhahabu wa Mattany Ikungi.

Rais wa Shirikisho la wachimba madini Tanzania, John Bina, akizungumza na wachimbaji madini wa machimbo ya dhahabu kijiji cha Mhintiri tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi .Rais Bina pamoja na mambo mengine, aliagiza kufunguliwa kwa mgodi wa dhahabu unaomilikiwa na Mattany Khalifa uliofungwa baada ya kuvamiwa na wachimbaji wadogo.
Mmiliki wa Mattany Gold mine, Mattany Khalifa, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa maalum kwa ajili ya kufunguliwa kwa mgodi wake uliofungwa baada ya kuvamiwa na wachimbaji wadogo.Mwenye kofia ya pama ni Rais wa shirikisho la wachimbaji madini Tanzania, John Bina.

Milioni 16/- zatolewa na CIP Trust ujenzi wa madarasa.


Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi, (mwenye mgorore wa bluu) akishiriki kutoa burudani na kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Kinyamwenda kwenye sherehe ya kukabidhi vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu wa shule ya kijiji hicho.

Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,akiwa amevikwa nguo na kukabidhiwa zana za ushujaa na wananchi wa kijiji cha Kinyamwenda,kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mchapa kazi wa kupigiwa mfano katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Watoto zaidi ya 66,442 mkoani Singida kupatiwa chanjo mpya ya Malaria na Rubella.

Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi, akizindua zoezi la chanjo mpya ya Malaria na Rubella kwa manispaa ya Singida.Uzinduzi huo umefanyika kwenye kituo cha afya cha Sokoine mjini Singida. Pamoja na chanjo ya Malaria na Rubella, pia dawa za minyoo na mabusha zilitolewa.
Meya wa manispaa ya Singida Sheikh Salum Mahami, akizungumza kwenye zoezi la uzinduzi wa chanjo ya Malaria na Rubella  kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo cha afya Sokoine mjini Singida.Wa pili kulia (waliokaa) ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi na anayefuata ni kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Singida.

TUNAJALI wawajali wanawake na vifaa tiba vya mil 155/-

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la TUNAJALI, Dk.Gottlieb Mpangile (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya kuzindua mpango wa kutokomeza vifo vya wajawazito na watoto wachanga mkoani Singida, Pia hafla hiyo ilitumika kutoa msaada wa vifaa tiba vikiwemo vitanda vya kujifungulia vyote kwa pamoja  vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 155 milioni.Wa pili kushoto (waliokaa) ni mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone na wa kwanza ni katibu tawala mkoani Singida, Liana Hassan.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye hafla ya kuzindua mradi wa kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kukabidhiwa vifaa tiba na shirika la TUNAJALI. Wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan na Kulia ni Mkurugenzi wa shirika la TUNAJALI, Dk. Gottlieb Mpangile.

Wanafunzi waaswa kutokufaulu kidato cha nne, sio kufeli maisha.

Rais wa shirikisho la wachimba madini Tanzania na mgeni rasmi wa mahafali ya sita ya shule ya sekondari kata Mandewa,John Bina,akizungumza kwenye mahafali hayo. Kulia ni mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari ya Mandewa.Bahati Shagama na kushoto ni mkuu wa  wa shule hiyo, Margreth Missanga.
Mkuu wa shule ya sekondari kata ya Mandewa manispaa ya Singida, Margreth Missanga, akitoa taarifa yake kwenye mahafali ya sita ya wahitimu wa kidato cha nne yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo. Kulia ni rais wa shirikisho la wachimba madini Tanzania (mgeni rasmi) John Bina, na Kushoto mwalimu wa shule hiyo.
Rais wa shirikisho la wachimba madini Tanzania, John Bina akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari kata ya Mandewa mjini Singida,wakati wa mahafali ya sita.

Thursday, November 6, 2014

Kikongwe apigwa risasi na polisi na kufariki dunia.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela.

KIKONGWE mmoja mkazi wa kitongoji cha Ilolo kata ya Iglansoni tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi, Joyce Maragabu (65),amefariki dunia baada ya kupigwa kwa risasi na askari polisi waliokuwa wakijihami dhidi ya kundi kubwa la wananchi waliokuwa wakitaka kuwavamia,ili wasiweze kumkamata mhalifu.

Askari hao walikuwa wakitaka kumkamata Nkida Gwisu, aliyekuwa akituhumiwa kumshambulia mtu mwingine.

Kikongwe huyo alipigwa risasi kichwani wakati akiwa anaendelea

RC Singida akataza warsha kuendeshwa kwa kiingereza.

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye ufunguaji wa warsha ya wadau kujadili rasimu ya mwisho ya taarifa ya mpango wa usimamizi na uendelezaji wa pamoja wa rasilimali za maji wa bodi ya maji ya bonde la kati, liyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aquar Vitae hotel mjini Singida.
Baadhi ya wadau waliohudhuria warsha ya wadau kujadili rasimu ya mwisho ya taarifa ya mpango wa usimamizi na uendelezaji wa pamoja wa rasilimali za maji wa bodi ya maji ya bonde la kati,iliyofanyika mjini Singida.